Tanzania na awamu za uongozi, ya Kwanza hadi ya Sita

MwajabuOmary

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
236
209
Kumekuwepo na mjadala mkali juu ya kutaka kujua watanzania tuko awamu ya sita au bado tuko awamu ya tano?

Mtanzania mwenzetu Ndugu Polepole ametanabaisha kwamba tuko awmu ya tano(5) bado.

Watanzania walio wengi wameaminishwa kwamba tuko awamu ya sita (6)

Nimejaribu kutafakari kwa kupitia hoja za pande zote mbili bado sijapata upande upi upo sahihi.

Ili kupata usahihi wa nani yuko sahihi tungejiuliza maswali yafuatayo:-

1. Ni kitu gani kinatabainisha kwamba hii ni awamu fulani:

Je, ni Uchaguzi Mkuu?
Je, ni Katiba ya Nchi?
Je, ni ilani ya CCM?
Je, ni mabadiliko ya uongozi wa JuNa

Najaribu kutafakari na huu ni mfano tu kwamba kwa uchaguzi uliofanyika mwaka jana kwanza ndani ya CCM kama ingekua fair katika uchaguzi wa ndani kwamba wanaccm wangeruhusiwa kuchukua fomu na mwana CCM mwingine angechukua nchi badala ya JPM. Je, tungeendelea kujinadi kwamba tuko awamu ya tano au ya sita?

kwaje, kwa mfano angeshinda Tundu Lisu tungesema tuko awamu ya sita au ya tano?
Ni tafakari yangu tu bandugu.

Nawakaribisha kwa mawazo na michango yenu.
 
... japo kwa mwananchi wa kawaida awamu is NONSENSE; suala hili lemeshafafanuliwa tena na tena lakini sijui kwanini halieleweki. Soma Ibara ya 40(4) ya Katiba ya JMT quoted hapo chini. Suala la awamu limefafanuliwa vizuri sana kwenye ibara hiyo;

"Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu".
 
Awamu ya 6 boss

Awamu ya sita boss
 
Awamu ya 6 boss

Awamu ya sita boss
Exactly! The matter closed!

Iko hivi, kwa mujibu wa Katiba, kwa kuwa Samia atashika kiti cha Rais kwa kipindi kinachozidi miaka mitatu (which is the fact), haendelezi utawala uliopita; rather ni muhula wake mwenyewe na ndio maana hataruhusiwa kugombea zaidi ya mara moja! Angeshika kiti cha urais chini ya miaka mitatu hapo ingekuwa ni extension ya urais uliopita! Mambo ya wazi namna hii watu wazima wanageuza kuwa mjadala wa kitaifa! NONSENSE!
 
Tunataka katiba mpya sio huu ugoro
 
Tunataka katiba mpya sio huu ugoro
... kutaka Katiba Mpya hakuzuii au kuondoa facts zilizopo Chief. Tatizo sijui uzuri historia ikiandikwa imeandikwa; iwe mbaya au nzuri haibadiliki.
 
Hii ni awamu ya 6 kikatiba.

Namshukuru mama awe makini Na wahuni akina Nape wataivuruga nchi yetu. Hi Nape angekuwa mtoto wa Hayati Nyerere au Karume hivi ingekuwaje si angekuwa anatukana watu hovyo ndani ya Chama Na serikalini kwa kusema Baba yake ndo Mwenye Chama Na nchi hii?

Lazima tuwakemee hawa wahuni.
 
Mimi niwashukuru kwa michango yenu mizuri na kitu ambacho nimejifunza ni kwamba kwa mujibu wa katiba yetu kama ilivyonukuliwa hapo juu, awamu ni kama kipindi fulani cha utawala wa mtu fulani. Hapo nimekubali na salamu zimfikie Polepole.
Na kwa mantiki hiyo basi kipindi cha awamu ya tano kilianza Novemba,2015 hadi March, 2021, nadhani niko sawa.
 
Back
Top Bottom