TANZANIA MOJA YA NCHI CHACHE DUNIANI ZENYE HALI YA HEWA NZURI SANA

Princemwalejr

JF-Expert Member
Nov 9, 2017
496
488
6ee372c8e05acfcfe6e51fd6f772ce93.jpg


“Dar es Salaam: Annual Weather Averages. January is the hottest month in Dar es Salaam with an average temperature of 27°C (81°F) and the coldest is July at 23°C (73°F) with the most daily sunshine hours at 10 in September.

January ndio mwezi wa joto zaidi. Wastani wa joto la mwezi huo ni nyuzi 27 (81F). Wape watu wa Marekani na Ulaya joto hilo kwa mwaka mzima watafanya sikukuu mwaka mzima.

Mwezi wa baridi sana ni July wenye joto la nyuzi 23 (73F). Kaka tafadhali. Hapo ndio utakuta wazungu wa nchi kama Ujerumani wanachanganyikiwa. Ni vibukta tu barabarani na kwenye mapaki wakiota jua.


Lakini watanzania hatuachi kulalamika jua kali. Jua kali nendeni Libya ambako joto linafikia nyuzi 56 (173F). Miji ya joto ya Marekani kama Las Vegas na Phoenix joto la zaidi ya nyuzi 37.8 (100 F) Ukienda kimasihara unapigwa homa ya joto kali (heat stroke)

Tanzania hakuna joto. Kuna watu wasiojua kudhibiti joto. Utakuta mtaa mzima nyumba zimesongamana, madirisha yamezibana na hakuna hata mwenye feni la mezani.

Wanaojimudu kidogo wana mafeni ya darini. Matajiri na maofisini ndio kuna viyoyozi vya ndani au vya kuning’ing’inia nje. Viyoyozi hivi havina raha kwa sababu ni baridi sana na vinaleta magonjwa ya baridi bila ya watumiaji kujishtukia.

Joto la Tanzania linadhibitika kwa madirisha makubwa bila hata ya kuhitaji kiyoyozi. Lala kwenye chumba kisicho kwenye msongamano, kuwa na madirsha mawili yanayoingiza hewa kwa mbele na ubavuni uone kama utahitaji kiyoyozi.

Njia nyingine ya kulimudu joto la Tanzania ni kuishi nyumba za gorofani na kuwa na madirisha yanayopitisha hewa. Gorofani upepo wake umepoa kuliko nyumba ya chini.

Najua watapiga kelele pesa, pesa, pesa. Sio pesa ni mipango au wanasema miundo mbinu. Wakazi wote wa Magomeni wanaweza kuishi kwenye magorofa mawili au matatu yenye nafasi na kuacha eneo la wazi kubwa kwa kupanda miti na kuleta hewa safi.

Vilevile tubadilishe mfumo wetu wa viyoyozi. Viyoyozi vyetu ni vya kufunga katika kila chumba. Wenzetu wanatumia Central Cooling System. Mashine ya kiyoyozi ni moja inakaa nje ya nyumba. Halafu inasambazwa kama mabomba ya maji kufikisha hewa katika kila chumba ndani ya nyumba. Haina mzizimo wa friji kama viyoyozi vyetu vya Tanzania.

10cce0b1ac462f02d2de342245f5e355.jpg



55baea341f330311bf95685a2f861fd9.jpg



545991502683a8db0f7593677666b2a4.jpg



Watu wote wa Magomeni wanaweza kuishi kwenye huu mjengo mmoja. Sehemu iliyobaki tukatengeneza gadeni.


21d96defc625bc600415e0a4e04fdf6f.jpg
 
Cha muhimu ni watu wajue wanavyofanya wenzetu. Hivyo vya gharama na teknolojia vinafuata baada ya wazo la kufanya kitu fulani.

Watu wakijua kuwa kwenye central cooling system mashine moja inatumika kupoza nyumba nzima watagundua kuwa inaweza kuwa ni nafuu kigharama kuliko kununua kiyoyozi cha kuweka katika kila chumba ndani ya nyumba. Wenye gesti na hoteli watanielewa haraka.
 
naona mipango miji nako kuna shida endapo Tukiamua kupima viwanja kuanzia 35*40 au 45*55 unaweza kupata eneo la kujenga nyumba na kupanda miti ya kivuli hivyo kuburudisha mji!! hata jito lingepungua!
 
11450e8e2f8517d59ca5d5c0168b866f.jpg


Namna hiyo utalaani hali ya hewa ni mbaya?
Kwani tatizo ni nini mbona nchi bado ina ardhi kubwa? Wenzetu wanapanua miji na wanajenga magorofa kudhibiti utumiaji wa ardhi na kupata hewa safi.
 
Back
Top Bottom