Tanzania: Lake Babati to be leased to Chinese investors

TIBIM,

Nimetoa mfano wa Sangara kwa sababu wamekwishaonesha kwamba wanaweza kufugwa kibiashara mpaka biashara ya kimataifa. Tunahitaji samaki wanoweza kufugwa kibiashara. Kama mumi, ngege, ningu n.k. wanaweza kufugwa kibiashara basi tuwafuge kibiashara badala ya kusubiri kudra za Mwenyezi Mungu ambaye alitupa akili za kupambana na mazingira yetu.
 
kabla ya yote ufanyike upembuzi yakinifu kujua athari za kimazingira hususan ni kwa aina asilia za samaki na viumbe wengine. lingine ni athari za kijamii kama vile uhuru wa JAMII inayozunguka kulitumia ziwa lao bila vizuizi!!? wataruhusiwa kuvua, kuogelea, kupita na boti, kuchota maji!!? pia gharama za uwekezaji ziwe halisi. ili tusiwe na mzigo wa DENI ambalo litakuwa mzigo kwetu.
 
Mji wa Babati uko katika mchakato wa kulikodisha ziwa Babati kwa kampuni toka China ya XIN SI LUCO Ltd, kuwekeza katika mradi wa ufugaji samaki.

Hatua hiyo inalenga kufufua ziwa hilo ambalo kina chake na viumbe waishio vimeendelea kupungua na kuathiri utalii na maisha ya watu.
Ghafla utasikia liMagu linazuia uwekezaji huo hadi lipewe mgao wake!
 
Mji wa Babati uko katika mchakato wa kulikodisha ziwa Babati kwa kampuni toka China ya XIN SI LUCO Ltd, kuwekeza katika mradi wa ufugaji samaki.

Hatua hiyo inalenga kufufua ziwa hilo ambalo kina chake na viumbe waishio vimeendelea kupungua na kuathiri utalii na maisha ya watu.

XIN SI LUCO Ltd ni mali ya serikali ya China na siyo private company. Yaani hapo ni kukabidhi ziwa Babati kwa serikali ya China na siyo kampuni!! Ni kama SUKITA ya Tanzania ya enzi hizo!
 
XIN SI LUCO Ltd ni mali ya serikali ya China na siyo private company. Yaani hapo ni kukabidhi ziwa Babati kwa serikali ya China na siyo kampuni!! Ni kama SUKITA ya Tanzania ya enzi hizo!
Wachina sio Wa kuwaamini. Yaani Afadhali ya Mzungu kuliko Mchina. Yaani Rais Magufuli alipoukataa mradi Wa Bandari ya Bagamoyo ilikuwa bonge la decision. Nategemea na huu ujinga ataukataa.
 
HIvi hakuna wa taalamu wa kuandaa na kutekeleza programu ya fish stocking Lake Babati pamoja nazuio uvuvi kwa muda fulani. Tatizo sisi wenyewe.
 
Viboko na perege! labda hata mamba!
Anyway hii ingekuwa ni investment nzuri sana kwa babati na mkoa wa Manyara kwa ujumla lakini kulease/ kulikodisha ziwa kwa wachina ni kosa kubwa sana. Yaani serikali imekosa wabia wa kuwekeza kwenye like ziwa mpaka wakaamua kukodisha. Myopic!
Leasing haijawahi kuwa na shida,leasing si mkopo na hilo likiwezekana ni zuri kwa sisi wenyeji!Walau tutajifunza!Watanzania tunahitaji kuona kitu kikistawi mahali fulani ndo tuerevuke!Wasiwasi wangu ni ukaribu wao(hao wachina) na mbuga...!
 
Kwa mchina tunajichanganya mno, bola hata Mpeleke ng'ombe za Msukuma na Mmasai wakanyweshe apo
 
Mji wa Babati uko katika mchakato wa kulikodisha ziwa Babati kwa kampuni toka China ya XIN SI LUCO Ltd, kuwekeza katika mradi wa ufugaji samaki.

Hatua hiyo inalenga kufufua ziwa hilo ambalo kina chake na viumbe waishio vimeendelea kupungua na kuathiri utalii na maisha ya watu.
Ivi lake Manyara ndo hilohilo lake bahati??
 
Kwa kweli nimeanza kukosa imani na wachina kama vile ambavyo sina imani na wazungu. Ni bora tukae tunaliangalia hadi tupate akili ya kulitumia kujiingizia kipato.
 
1. litawekwa uzio
2. hakuna wavuvi binafsi tena
3. hakuna kuingia kabisa.
4.Hadi maji mamlaka ya maji babati watakuja kuuziwa na wachina!
muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Back
Top Bottom