Tanzania: Lake Babati to be leased to Chinese investors

Hawa Wachina nao sio Watu Wazuri.

Kwa nini wasituuzie ujuzi/elimu tufuge wenyewe?

Hii ni sawa na TBC kusaidiwa na China kutafsiri tamthilia zao badala ya kuomba Watu wetu wapewe ujuzi tutengeneze za kwetu.

Na tunakaa pembeni na kuona hii ni sawa tu.

Hao Wachina tunawaamini kiasi gani mpaka tuone kila kitu ni nia njema?
 
......
.......Tuache upuuzi na siasa katika mambo Muhimu hilo ni ziwa sio bwawa la kufugia samaki Mge harmonize Utalii na conservation agriculture with return profit to communities sorrounding the Lake ingekuwa na Tija
 
Sipendagi watu wanaopiga picha articles kwenye magazeti bila kuhakikisha kua itasomeka
 
Mji wa Babati uko katika mchakato wa kulikodisha ziwa Babati kwa kampuni toka China ya XIN SI LUCO Ltd, kuwekeza katika mradi wa ufugaji samaki.

Hatua hiyo inalenga kufufua ziwa hilo ambalo kina chake na viumbe waishio vimeendelea kupungua na kuathiri utalii na maisha ya watu.
Kwa nini wasikodi Victoria tukapa fedha zaidi?
 
Itakuwa vizuri kama tuki-lease Ngorongoro na Serengeti pia. Itasaidia sana kudhibiti ujangili.
 
Viboko na perege! labda hata mamba!
Anyway hii ingekuwa ni investment nzuri sana kwa babati na mkoa wa Manyara kwa ujumla lakini kulease/ kulikodisha ziwa kwa wachina ni kosa kubwa sana. Yaani serikali imekosa wabia wa kuwekeza kwenye like ziwa mpaka wakaamua kukodisha. Myopic!
Kipi tunaweza zaidi ya kurudia chaguzi
 
Kwanza watuambie China wanatudai bei gani?? Isije ikawa figisu.. China sasa hivi ni mkoloni mpya wa nchi za Afrika
Sio mda tutawaachia Bandari na VIWANJA vya ndege vya Africa waendeshe Miaka 100 hadi wamalize deni lao
 
Haya ndiyo yanamkera Mkulu. Hivi sisi tunashindwa kupandikiza samaki hapo kweli?!? Tunabaki eti samaki wamekwisha! Wekezeni sangara muone baada ya miaka miwili mtapata nini. Kwani Ziwa Victoria wale sangara ni wa asili si walipandikizwa tu.
Sangara uuwa Samaki asili waliopo mfano mumi, ningu, ngege,nk
 
Back
Top Bottom