Tanzania kupeleka battalion moja Congo

We kama mimi nilipata jazba ila mwishoni nimemuelewa. Kikubwa hata hao 850 hawatoshi pili tutaungana na majeshi ya S.Africa kwenda mashariki ya Congo kuwatokomeza MR23.

Ila mkuu ujue hapa mgogoro ni mkubwa zaidi ya unavyofikiri. Hapa kuna Rwanda na Uganda ambao M23 ni mtoto wao!
 
Ila mkuu ujue hapa mgogoro ni mkubwa zaidi ya unavyofikiri. Hapa kuna Rwanda na Uganda ambao M23 ni mtoto wao!

Hilo ni kweli mkuu na kunauwezekano wa kuzigusa hizi nchi mbili yaani Uganda na Rwanda, ila ni pale tu kama kutakuwa na ulazima wa wakuwafuata waasi MR23 pale watakapovuka mpaka na kuingia Rwanda kuepuka mashambulizi. Na watakapokuwa wakishambulia kutokea ndani ya Rwanda hatuna jinsi zaidi ya Jeshi la umoja [ Tanzania na S. Africa] kuishambulia Rwanda katika location ambayo hao waasi watakuwepo kwa muda huo.
 

Thank You Brother.
 
Kajembe mwidiwe chambu? Abha bhantu bhalatumila muwu mwaka, jewe mva manyaovu, abha bhaloko bhalatumala.
 
mkuu si kuingia tu bali hawa jamaa wana backing ya Rwanda na Uganda hivyo kuwafurusha ni kuzifurusha Rwanda na Uganda kutoka DRC ambako wana maslahi kwenye madini mashariki mwa Kongo. Nina shaka na RSA kwa kuwa nao nadhani wana maslahi huko kama ilivyokuwa CAR ambako walienda kumlinda Bozize. Hivyo basi kupeleka majeshi huko hawa jamaa zetu hawatafurahi na hawajafurahi.
 

kuna wanajeshi pale uganda wamekuwa mamilionaire kwa hii vita ya congo..
 
kuna wanajeshi pale uganda wamekuwa mamilionaire kwa hii vita ya congo..

Hakika watu kama Salim Salehe (mdogo wa M7) na Mugisha Muntu walipata mali kibao huko DRC na wengine wanaendelea kujipatia mali kwa mgongo wa vita ya mashariki mwa DRC.
 
kama ulikuwepo kichwani kwangu. naona jamaa ameandika kilevi, kwa sababu maswali aliyouliza, majibu yake hayahitaji shule, bali common sense.
alitakiwa tu atupe taarifa ilikuwa inatosha na tungemshukuru.

Alieandika alishatangulia kusema hana uelewa wowote na mambo hayo, si vyema kusema kaandika kilevi. Yeye ufahamu wake umefikia hapo, kinachotakiwa ni kumueleweshwa so be positive ktk kumjibu au kumuelewesha. Watu tuko tofauti, kielimu, ki-uelewa, fani tulizobobea, hobi na mengineyo. Nachokijua mimi unaweza kuwa hufahamu hata kidogo na ukiuliza swali na mimi nikiwa na mtazamo wako nitajiuliza huyu jamaa mbona kilaza, kumbe sivyo na wewe waweza kuwa na eulewa ktk nyanja nyingine tofauti. Heshimu kila wazo la mwana JF, ukiona halikuingii unapotezea.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
wanajeshi wetu kwenda congo kupigana ni sehemu ya uzoefu kwao na inaowaongezea weledi wao katika vita kuliko kukaa bure tu
 
Bora wende ni muda mrefu wanakula bure na wanaonesha wana nguvu nyingi mpaka wanaingia mitaani kutuua sisi raia wa nchi yetu wenyewe, hapa ndio tutapata nafasi ya kuwapima hiki kiherehere chao.
 
Kajembe mwidiwe chambu? Abha bhantu bhalatumila muwu mwaka, jewe mva manyaovu, abha bhaloko bhalatumala.

Imanyovu hehe se? imnanila? au Mkatanga? umenikumbusha Nyamasovu aisee na nyamihini! hahahahaha!
 

Nashukuru ndugu
 

Naunga mkono kupeleka batallion.
ushauri wangu ni kuwa wasiende kupigana bali kulinda raia na upande mwingine waanzishe mazungumzo ya kusaka amani. wale jamaa ni wazoefu wa vita na pia ni wenyeji wa mazingira. misitu mingi ya congo drc ni kikwazo kikubwa kwa jeshi lolote la kulinda amani. darfur, lebanon na somalia jiografia yake ni tofauti. baba yangu mdogo aliongoza battalion huko msumbiji enzi za frelimo lakini alirudi na watu si zaidi ya kumi. sasa hivi yupo kambi ya kaboya na anastaafu mwaka huu huku akiwa hana hata nyumba aliyojenga.
wakati mwingine ingetosha kulinda mipaka yetu tu ingawa tunahitaji kujifunza matumizi ya zana za kisasa na mazingira tofauti. la sivyo mabomu yataoza na kutulipukia.
 

Tunashukuru kwa kutupa practical experience
 
waende tu wakapate uzoefu,mwenzao rais wa malawi anatrot tu anapima upepo,hata wakindei wote barida tu si mazoezi hayo!
 
Bora wapelekwe policcm tumeshachoka nao huku kitaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…