Tanzania kupeleka battalion moja Congo

Tanzania kupeleka battalion moja Congo

Ronn M

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2012
Posts
1,279
Reaction score
684
Kwa mujibu wa Membe, Serikali inatarajia kuomba ridhaa ya Bunge kupeleka battalion 1 huko Kongo(Si chini ya wanajeshi 850) kulinda amani. Ikumbukwe kwamba wanajeshi hawa wamepewa mandate ya kupambana na waasi.
Je
1. Wanajeshi wetu wameandaliwaje kupambana na waasi huko Kongo? Any special training?

2.Kwa kuwa Idadi hiyo ni kubwa, je ipo mikakati ya kuhakikisha hatupungukiwi wakati hao wapo huko?

3. Any consideration and special attention to their families?Najua wamekula kiapo cha utii kuilinda mipaka ya Nchi yetu japo cjui kama kiapo hicho kinawalazimu kwenda mission hizi.

Maswali haya yanawezakuwa hayana mantic mana sina ufahamu wakutosha wakijeshi.

Otherwise nawatakia mafanikio mema hasa ukizingati wamekuwa na record nzuri huko Darfur, Syria na Lebanon
 
Naogopa kusema kuwa sasa tukiingiia DRC tumepanua wigo wa Mseveni na mwenzake Kagame kuingilia Tanzania na kuipiga
 
Kwa mujibu wa Membe, Serikali inatarajia kuomba ridhaa ya Bunge kupeleka battalion 1 huko Kongo(Si chini ya wanajeshi 850) kulinda amani. Ikumbukwe kwamba wanajeshi hawa wamepewa mandate ya kupambana na waasi.
Je
1. Wanajeshi wetu wameandaliwaje kupambana na waasi huko Kongo? Any special training?

2.Kwa kuwa Idadi hiyo ni kubwa, je ipo mikakati ya kuhakikisha hatupungukiwi wakati hao wapo huko?

3. Any consideration and special attention to their families?Najua wamekula kiapo cha utii kuilinda mipaka ya Nchi yetu japo cjui kama kiapo hicho kinawalazimu kwenda mission hizi.

Maswali haya yanawezakuwa hayana mantic mana sina ufahamu wakutosha wakijeshi.

Otherwise nawatakia mafanikio mema hasa ukizingati wamekuwa na record nzuri huko Darfur, Syria na Lebanon

Kabla sijaona hiyo ya blue nilikuwa kama nataka kupata jazba lakini nimekuelewa.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni jeshi imara na lenye mafunzo ya kutosha ya kivita. Mimi binafsi naliamini katika mbinu za medani.

Yaani mkuu unasema wanajeshi 850 wasababishe upungufu kweli?
 
Kinachonisikitisha tu ni kwamba kwa mara ya kwanza katika historia ya UN, Security Council wamekuja na Offensive Mandate(to attack) wakati mission zote mandate imekuwa ni defensive (kujilinda).Hii ni kama majaribio ya hiyo mandate na watekelezaji wake watakuwa ni jeshi la tz.Kazi ipo.lakini naliamini Jeshi letu kwa kazi watakayo pewa iwe special force au Recce,sina shaka,vijana wameiva.,na najua m 23 huko waliko baada ya kusikia watz wanakuja mavi yanagonga chupi na kurudi.
 
Kihererehe cha jk na serikali yake kitatufikisha pabaya sana
 
Kabla sijaona hiyo ya blue nilikuwa kama nataka kupata jazba lakini nimekuelewa.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni jeshi imara na lenye mafunzo ya kutosha ya kivita. Mimi binafsi naliamini katika mbinu za medani.

Yaani mkuu unasema wanajeshi 850 wasababishe upungufu kweli?
kama ulikuwepo kichwani kwangu. naona jamaa ameandika kilevi, kwa sababu maswali aliyouliza, majibu yake hayahitaji shule, bali common sense.
alitakiwa tu atupe taarifa ilikuwa inatosha na tungemshukuru.
 
sio pabaya, tunapata uzoefu wa mbinu mpya za kivita katika mazingira tofauti, ni bora kuliko kukaa nyumbani na kujiona bora bila kujipima na wenzetu..i support the move
 
Kabla sijaona hiyo ya blue nilikuwa kama nataka kupata jazba lakini nimekuelewa.Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni jeshi imara na lenye mafunzo ya kutosha ya kivita. Mimi binafsi naliamini katika mbinu za medani. Yaani mkuu unasema wanajeshi 850 wasababishe upungufu kweli?
Nafahamu kuwa wanajeshi wanapatiwa mafunzo ya mara kwa mara. Nafahamu pia mafunzo hayo yanaendana na mazingira husika. Technically, I believe, sio kila mwanajeshi unaweza kumpeleka vita yeyote. Kama mnategemea upinzani mkubwa toka katika bahari, matakwa yake ni tofauti na vita ambayo upinzani mkubwa unatokea angani. Hivyo ndio kusema, kwa mawazo yangu, kuwa nadhani napaswa kuhoji kama wanajeshi wetu wamepata special training ya wanachokiendea. Idadi ya 850 sidhani kama ni idadi ya kupuuzwa hasa nyakati hizi za technolojia ambapo majeshi yanatumia nguvu kazi kidogo kwa big impact!
 
kama ulikuwepo kichwani kwangu. naona jamaa ameandika kilevi, kwa sababu maswali aliyouliza, majibu yake hayahitaji shule, bali common sense. alitakiwa tu atupe taarifa ilikuwa inatosha na tungemshukuru.
Nashukuru kwa kutambua nimeandika kilevi. Wakati fulani wanajeshi wamerakani walikwenda kwenye milima ya Afghanstan(?) kupambana na kina Osama. Walitumia vifaa vya kisasa kusurvey eneo la milima ile na kuona patupu. Waliposhuka ndipo wenzao wakatokea katika mapango. Ndege zao ziliharibiwa vibaya. Walikufa wengi mno. Walikutana na upinzani mzito tena wenye silaha za kisasa kuliko wao. Walikiri hawakuwa wamejipanga vyema kukabiliana na maadui hasa ktk mapango yaliyo kwenye milima na baridi kali! Mlevi yeyote kama mimi alipaswa kujiuliza, watu hawa walikuwa wameandaliwa specifically for such a war? Nadhani kila dereva aliyefuzu udereva anaweza kuendesha gari ingawa anaweza kupata changamoto kuendesha kwenye snow au mud road hasa kama hajawahi kabla!
 
Kinachonisikitisha tu ni kwamba kwa mara ya kwanza katika historia ya UN, Security Council wamekuja na Offensive Mandate(to attack) wakati mission zote mandate imekuwa ni defensive (kujilinda).Hii ni kama majaribio ya hiyo mandate na watekelezaji wake watakuwa ni jeshi la tz.Kazi ipo.lakini naliamini Jeshi letu kwa kazi watakayo pewa iwe special force au Recce,sina shaka,vijana wameiva.,na najua m 23 huko waliko baada ya kusikia watz wanakuja mavi yanagonga chupi na kurudi.
I pray that this be the true position of our army
 
Sipingi, ila Tanzania bwana, amani ndani ya Tz ipo au ndo yale yale ya kuzima moto kwa jirani wakati kwako kaungua?
 
usiwaze kodi tunayotoa kumbuka amani inayopatikana inatoka wapi wenzako hawalali wanalinda mipaka kwa ajili yako wewe unaofanya biashara na kupulizwa upepo ikitokea vita watakaofaidi ni wanajeshi pekee wengine ni vilio tu mwanzo mwisho
 
athali za vita ni wanajeshi kufa. sasa kwanini aifie congo wakati ameapa kuilinda tanzania? Kwanini wanajeshi wetu wasile matunda ya aman ya Tanzania?. hii inanikera sana. mia
 
athali za vita ni wanajeshi kufa. sasa kwanini aifie congo wakati ameapa kuilinda tanzania? Kwanini wanajeshi wetu wasile matunda ya aman ya Tanzania?. hii inanikera sana. mia
Nimeuliza hapa kama kuna wataalamu wa jeshi watujuze. Hivi kiapo chao kinawalazimu pia kwenda kulinda amani nchi za wengine?
 
Wanajeshi wetu watapata uzoefu kidogo kupambana. This is part of field exercises, human costs not withstanding. Haiwezekani nchi inakaa tu bila battle action for decades, jeshi litadumaa kama lile la Malawi. Go, TPDF go!
Kuhusu tishio la Uganda na Rwanda, ambao wako upande wa waasi, sio suala tena. Rwanda iko UN security council na ilipiga kura jeshi lipelekwe, kwani kuwepo kwa jeshi hilo pia kunaisaidia kujikinga na waasi wa FDLR.
Pia Rwanda haiwezi kuthubutu kushambulia au kujenga uhasama wa kijeshi na Tanzania kwasababu kuu mbili: Uhusiano ndani ya EAC na pia bandari ya Dar es Salaam. Hatua hii ni mwanzo wa kumaliza matatizo DRC.
 
Back
Top Bottom