Tanzania kuipa Comoro Msaada wa Ndege

Tanzania kuipa Comoro Msaada wa Ndege

Ki ukweli hii ni aibu inapotokea fursa kama hii kwa taifa kama hili Lililopata uhuru zaidi ya miaka 50iliyopita,lenye idadi ya watu zaidi ya 40 milioni inashindwa kuwa hata na shirika la ndege lenye ndege zinazoruka?
Kenya na Rwanda mbona wao wameweza wana nini? Nasisi tunashindwa kwa nini?
kweli tuna haja ya kujitafakari upya kama taifa na kujua mwelekeo wetu ni upi.
Nikiangalia mbele naona giza totoro,

Kwa ujumla Tanzania hatuwezi kitu. Hata mpira umetushinda tutaweza nini!? Jana nilikuwa naangalia Cocafa cup South Africa tunafungwa mpaka na Lesotho, Swaziland na Madagascar. Hivi Tanzania tunaweza nini zaidi ya UFISADI!!
 
Kwa ujumla Tanzania hatuwezi kitu. Hata mpira umetushinda tutaweza nini!? Jana nilikuwa naangalia Cocafa cup South Africa tunafungwa mpaka na Lesotho, Swaziland na Madagascar. Hivi Tanzania tunaweza nini zaidi ya UFISADI!!

Mimi nafikiri ktk masaibu yote yanayoikumba nchi.hii kiongozi wake mkubwa ni rushwa iloyotamalaki sekta mbalimbali kama sio zote kamatukifanikiwa kupunguza.Rushwa walau kwa asilimia hamsini kama sio kuondoa kabisa tunaweza kushuhudia mabadiliko makubwa.
Lakini nani wa kumfunga paka kengere.
Hakika tujitafakari upya kama taifa.
 
Tz na wa tz kwa kupenda kujitutumua et nanyie mnatakakutoa msaada wa usafili wa anga mbavu znaniuma kwa kicheko kilichojaa kebei/ nyie wakomoro mnamacho lakini hamuon kweli tz inaweza kuwasaidia ktk hili? duuuuuuu

Hahaha,na hivi walimwambia huyo waziri ndege zipo siyo?Hii ndo bongo,raha tupu!
 
Kweli jamani tusiwe wachoyo wa ndege tuwape tu wacomoro ni jirani zetu. Yaani ndege wamejaa maporini halafu wengine Hadi wanaharibu mazao mashambani! Tena naishauri serikali yetu sikivu ianze na kunguru wa zanzibar!

Kuna vindege vinapatikana njia ya Dodoma mjini Kondoa sehemu panaitwa Kelema, vimekaangwa na binzari wanauza watoto. Viko kama chura hivi Ila vitamu balaaah, nadhani hawa waComoro ndo walikuja kuomba nyama ya ndege hiyo and not Piloted Aircraft.


Tanganyika my Motherland I am ashamed of you......
 
Tz na wa tz kwa kupenda kujitutumua et nanyie mnatakakutoa msaada wa usafili wa anga mbavu znaniuma kwa kicheko kilichojaa kebei/ nyie wakomoro mnamacho lakini hamuon kweli tz inaweza kuwasaidia ktk hili? duuuuuuu

ukisikia mgonjwa anachangia damu ndio hii.
lajini fastjet na precision wachangamkie dili hill.
 
Tanzania hii hii yenye ndege 1 wafanyakazi mia ngapi sijui au Tanzania imetumika kama kivumishi au Kitenzi?hahahah
 
Nendeni kenya tanzania ndege zote ccm wameuza.labda mngeomba ufisadi mngepata haraka sana
 
ndege? ndege zipi au ndege mzungu wa shinyanga wakapige jiji chokaa au tuwape ndege kungru wa zanzibar wakawazolee taka
 



SERIKALI ya Comoro imeiomba Serikali ya Tanzania iisaidie kutatua changamoto ya uhaba wa ndege zinazotua nchini humo hali iliyosababishwa na kusitishwa kwa huduma za safari za shirika la ndege la Yemen.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi wa Comoro, Bahia Masoundi, alisema Shirika la Ndege la Yemen lilisitisha huduma zake kufuatia machafuko yanayoendelea nchini Yemen.

“Mchafuko ya nchini Yemen yalipelekea shirika lao la ndege kusitisha huduma zake na kutokana na kwamba ndilo shirika tulilokuwa tukilitegemea kwa kiasi kikubwa ndio maana uhaba umejitokeza baada ya kufunga huduma zao,” alisema Massoundi.

Alisema kwa sasa kuna mashirika manne tu yanayofanya kazi nchini humo na ndege zinazotua ni chache na kwamba serikali ya nchi hiyo haimiliki shirika hata moja hivyo kulazimika kuomba msaada nchini Tanzania.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA), Charles Chacha alisema waziri huyo amefanya mazungumzo na waziri wa Uchukuzi nchini, Samweli Sitta ambaye ametoa maagizo kwa TCAA ili ifanye utaratibu wa kuisaidia nchi hiyo.

“Tayari tumepokea maagizo ya Waziri mwenye dhamana na sisi kama mamlaka inayosimamia safari za anga tunaanza mara moja kuangalia namna ya kuisaidia Comoro kwasababu ni nchi ambayo ina makubaliano ya kusaidiana na Tanzania,” alisema Chacha.

Alisema kwa sasa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) hufanya safari zake mara nne kwa wiki nchini Comoro lakini bado kuna tatizo la mrundikano wa abiria wanaotaka kusafiri kwenda au kuja nchini kwa shughuli za biashara, utalii au kufuata huduma.

Aliongeza kutokana na uwezo mdogo wa ATCL atakutana na uongozi wa mashirika yenye uwezo yanayofanya kazi nchini yaweze kufanya safari nchini Comoro pamoja na kutoa kibali maalumu kwa shirika la ndege la Ethiopia ili ndege zake ziende nchini humo baada ya kutua Tanzania.

Chanzo: Mpekuzi blog
Huenda Mpekuzi blog hajapekua vya kutosha na hivyo taarifa si sahii vinginevyo, nadhani hawa jamaa hawakutamka ndege kwa maana ya aeroplane labda wale wa mbuga za wanyama ???!!! Kama ni kweli basi wana shida maana sisi wenyewe tumekodi halafu wao hawajui kama tuko hoi bin taabani. Ukiwa mgonjwa halafu ukaenda kutafuta dawa kwa fundi viatu si tu kwamba hutapona ila wanaweza wakaanza kufikiria kukupeleka sehemu kama Milembe.
 
Tanzania wana ndege za kusaidia? Atcl wana mgogoro mkubwa Wa kiuendeshaji haohao watoe msaaada Wa ndege ngumu
 
Ni sawa na kumuomba mtu anayeishi chini ya dolla moja kwa umasikin hakununulie Range na hakujengee mansion
 
Wacomoro tunachoweza ni msaada wa majeshi tu haya mengine mnataka kutuona wachoyo bure.
 
Daah!!! Ndugu zetu wa Comoro masikini ya Mungu tulivyowasaidia msaada wa kijeshi wanadhani tutaweza kuwasaidia kila kitu ndege zipo wapo za kuwasaidia waziri kuwa mkweli.
 

Hebu jamani hata kama tunaipenda ccm kiasi hicho, basi angalau tuthubutu kuwapa nchi hawa wenzetu wa upinzani tuone wanafanya nini kizuri.....!

Tuwape Angalau miaka mitano (5).... Ili tuone Kipi kitabadilika..

Maana kila kukicha hapa Tanzania, hatuoni hata jambo jipya ambalo linatia moyo.
 
Daah!!! Ndugu zetu wa Comoro masikini ya Mungu tulivyowasaidia msaada wa kijeshi wanadhani tutaweza kuwasaidia kila kitu ndege zipo wapo za kuwasaidia waziri kuwa mkweli.

Ccm kama kawaida yenu kudanganya ndio sala yenu ya asubuh hadi wewe wasema hivi leo utakuwa umeshika Msaafu au Biblia si bure waogopa sema uongo.
 
Sikufikiria kuwa ombi hilo lilimaanisha wanaomba Tanzania iisaidie Comoro 'NDEGE' kwa maana ya plane, nilidhani ndege wa kufugwa.
 
hivi anaomba ndege gani? Mwewe, kunguru au bundi maana zile za kupanda watu zote tumeshazika labda bundi ngoja niwaarifu bibi zangu kule sumbawanga au kwa shangazi bagamoyo
zote hizo.....
 
Back
Top Bottom