Tanzania kuipa Comoro Msaada wa Ndege

Tanzania kuipa Comoro Msaada wa Ndege

kwa mara ya kwanza nimesikia maiti ikiombwa t
damu
 
Ha ha haa..... Nilivyosoma "heading" nilifikiri ni msaada wa ndege kama "quelea quelea" labda walihitajika kutibu janga flani hivi linalohusiana na mazingira/mabadiliko ya tabia nchi.
 
TZ bana! Eti waziri wa uchukuzi sikui nani nani yule.. ameshatoa agizo kwa tcaa iangalie jinsi ya kusaiodia!!! My foot...

Na Comorro bana yaani wakaona nchi ya kuwasaidia ni TZ... Ama kweli acheni vipofu wavutane wenyewe...
 
Wakati Ethiopia wana 787 dream liner 4 na 52 mchanganyiko wa air bus na boeing za kutosha,,sisi tunakuna Nazi tuu, Ndege zinataka usimamizi wa hali ya juu sana,nadhani hata tungekua na Ndege zipo baadhi ya Nchi zingepigwa ban kwa sababu ya UNGA maana wangeficha hadi ktk engine kama watanzania tuu ndio wanameza iyo ingekua rahisi tuu.
 
He he hii lazima ucheke Tanzania kwa kipindi kile isinge weza kumshauri yeyote juu ya masuala ya ndege
 



SERIKALI ya Comoro imeiomba Serikali ya Tanzania iisaidie kutatua changamoto ya uhaba wa ndege zinazotua nchini humo hali iliyosababishwa na kusitishwa kwa huduma za safari za shirika la ndege la Yemen.


Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi wa Comoro, Bahia Masoundi, alisema Shirika la Ndege la Yemen lilisitisha huduma zake kufuatia machafuko yanayoendelea nchini Yemen.

"Mchafuko ya nchini Yemen yalipelekea shirika lao la ndege kusitisha huduma zake na kutokana na kwamba ndilo shirika tulilokuwa tukilitegemea kwa kiasi kikubwa ndio maana uhaba umejitokeza baada ya kufunga huduma zao," alisema Massoundi.

Alisema kwa sasa kuna mashirika manne tu yanayofanya kazi nchini humo na ndege zinazotua ni chache na kwamba serikali ya nchi hiyo haimiliki shirika hata moja hivyo kulazimika kuomba msaada nchini Tanzania.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA), Charles Chacha alisema waziri huyo amefanya mazungumzo na waziri wa Uchukuzi nchini, Samweli Sitta ambaye ametoa maagizo kwa TCAA ili ifanye utaratibu wa kuisaidia nchi hiyo.

"Tayari tumepokea maagizo ya Waziri mwenye dhamana na sisi kama mamlaka inayosimamia safari za anga tunaanza mara moja kuangalia namna ya kuisaidia Comoro kwasababu ni nchi ambayo ina makubaliano ya kusaidiana na Tanzania," alisema Chacha.

Alisema kwa sasa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) hufanya safari zake mara nne kwa wiki nchini Comoro lakini bado kuna tatizo la mrundikano wa abiria wanaotaka kusafiri kwenda au kuja nchini kwa shughuli za biashara, utalii au kufuata huduma.

Aliongeza kutokana na uwezo mdogo wa ATCL atakutana na uongozi wa mashirika yenye uwezo yanayofanya kazi nchini yaweze kufanya safari nchini Comoro pamoja na kutoa kibali maalumu kwa shirika la ndege la Ethiopia ili ndege zake ziende nchini humo baada ya kutua Tanzania.

Chanzo: Mpekuzi blog
Ni miujiza lakini kweli kipofu kumuomba msaada kiwete!
 
Achana na kuwasaidia ndege; hata wangeomba tuanzishe safari za ndege kwenda kwao uwezo huo hatuna...!!
 
Back
Top Bottom