Tanzania kuipa Comoro Msaada wa Ndege

Tanzania kuipa Comoro Msaada wa Ndege

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,233

SERIKALI ya Comoro imeiomba Serikali ya Tanzania iisaidie kutatua changamoto ya uhaba wa ndege zinazotua nchini humo hali iliyosababishwa na kusitishwa kwa huduma za safari za shirika la ndege la Yemen.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi wa Comoro, Bahia Masoundi, alisema Shirika la Ndege la Yemen lilisitisha huduma zake kufuatia machafuko yanayoendelea nchini Yemen.

"Mchafuko ya nchini Yemen yalipelekea shirika lao la ndege kusitisha huduma zake na kutokana na kwamba ndilo shirika tulilokuwa tukilitegemea kwa kiasi kikubwa ndio maana uhaba umejitokeza baada ya kufunga huduma zao," alisema Massoundi.

Alisema kwa sasa kuna mashirika manne tu yanayofanya kazi nchini humo na ndege zinazotua ni chache na kwamba serikali ya nchi hiyo haimiliki shirika hata moja hivyo kulazimika kuomba msaada nchini Tanzania.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA), Charles Chacha alisema waziri huyo amefanya mazungumzo na waziri wa Uchukuzi nchini, Samweli Sitta ambaye ametoa maagizo kwa TCAA ili ifanye utaratibu wa kuisaidia nchi hiyo.

"Tayari tumepokea maagizo ya Waziri mwenye dhamana na sisi kama mamlaka inayosimamia safari za anga tunaanza mara moja kuangalia namna ya kuisaidia Comoro kwasababu ni nchi ambayo ina makubaliano ya kusaidiana na Tanzania," alisema Chacha.

Alisema kwa sasa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) hufanya safari zake mara nne kwa wiki nchini Comoro lakini bado kuna tatizo la mrundikano wa abiria wanaotaka kusafiri kwenda au kuja nchini kwa shughuli za biashara, utalii au kufuata huduma.

Aliongeza kutokana na uwezo mdogo wa ATCL atakutana na uongozi wa mashirika yenye uwezo yanayofanya kazi nchini yaweze kufanya safari nchini Comoro pamoja na kutoa kibali maalumu kwa shirika la ndege la Ethiopia ili ndege zake ziende nchini humo baada ya kutua Tanzania.

Chanzo: Mpekuzi blog
 
tukio LA aina hiyo kulingana na kichwa cha habari linaweza kutokea mwaka 2050 chini ya usiokuwa utawala wa ccm

Ni Fasjet na Precision ndiyo zimeombwa sasa 6 akatumia mwanya kusema ATC ianze kazi mara moja
 
Heading tu imenifanya kutabasamu japo kwa huzuni: nikahisi ndege ( nyuni) looh
Ina maana hawasomi habari zetu za kifisadi na za kufilisi mashirika ya umma kwa kasi ya kimbunga?
 
SERIKALI ya Comoro imeiomba Serikali ya Tanzania iisaidie kutatua changamoto ya uhaba wa ndege zinazotua nchini humo hali iliyosababishwa na kusitishwa kwa huduma za safari za shirika la ndege la Yemen.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi wa Comoro, Bahia Masoundi, alisema Shirika la Ndege la Yemen lilisitisha huduma zake kufuatia machafuko yanayoendelea nchini Yemen.

"Mchafuko ya nchini Yemen yalipelekea shirika lao la ndege kusitisha huduma zake na kutokana na kwamba ndilo shirika tulilokuwa tukilitegemea kwa kiasi kikubwa ndio maana uhaba umejitokeza baada ya kufunga huduma zao," alisema Massoundi.

Alisema kwa sasa kuna mashirika manne tu yanayofanya kazi nchini humo na ndege zinazotua ni chache na kwamba serikali ya nchi hiyo haimiliki shirika hata moja hivyo kulazimika kuomba msaada nchini Tanzania.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA), Charles Chacha alisema waziri huyo amefanya mazungumzo na waziri wa Uchukuzi nchini, Samweli Sitta ambaye ametoa maagizo kwa TCAA ili ifanye utaratibu wa kuisaidia nchi hiyo.

"Tayari tumepokea maagizo ya Waziri mwenye dhamana na sisi kama mamlaka inayosimamia safari za anga tunaanza mara moja kuangalia namna ya kuisaidia Comoro kwasababu ni nchi ambayo ina makubaliano ya kusaidiana na Tanzania," alisema Chacha.

Alisema kwa sasa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) hufanya safari zake mara nne kwa wiki nchini Comoro lakini bado kuna tatizo la mrundikano wa abiria wanaotaka kusafiri kwenda au kuja nchini kwa shughuli za biashara, utalii au kufuata huduma.

Aliongeza kutokana na uwezo mdogo wa ATCL atakutana na uongozi wa mashirika yenye uwezo yanayofanya kazi nchini yaweze kufanya safari nchini Comoro pamoja na kutoa kibali maalumu kwa shirika la ndege la Ethiopia ili ndege zake ziende nchini humo baada ya kutua Tanzania.

Chanzo: Mpekuzi blog

Hii ni Business Opportunity - halafu tunalalamika hakuna ajira. Kwa nini ATC wasikodishe ndege haraka haraka na kuajiri vijana wafanye kazi? Maana Vita vya YEMEN ndio kwanza vimeanza - wala si vya kwisha leo.
 
Hahahaha...mkuu!

We acha tu...kazi kujisifia eti sisi ni sleeping giant? Kweli? Kwa ari ipi na mkakati upi uliowahi kutekelezeka?
Sometimes hua nahisi sisi sio wazaliwa wa hii nchi, kuna sehemu tumetolewa tukaletwa hapa Tanganyika, wala hatushtuki
We are walking slowly while others running fast for development!!
 
Hii ni Business Opportunity - halafu tunalalamika hakuna ajira. Kwa nini ATC wasikodishe ndege haraka haraka na kuajiri vijana wafanye kazi? Maana Vita vya YEMEN ndio kwanza vimeanza - wala si vya kwisha leo.

watakodisha ndege ipi mkuu? kwani wanayo ndege?
 
Back
Top Bottom