abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
Posted Ijumaa,Novemba23 2012 saa 9:4 AMKwa ufupi
Kesho (leo) na keshokutwa (kesho) uamuzi mgumu utatolewa ambao utalitatua tatizo la Kongo moja kwa moja, alisema Waziri Membe na kuongeza;
Tunailaumu UN kwa kutokuchukua maamuzi hayo magumu ya kuweza kuzuia vita nchini Kongo.
SERIKALI ya Tanzania imesema iko tayari kutoa bataliani moja ya wanajeshi 800 ili waweze kuingilia kati vita vinavyoendelea nchini Kongo kama Umoja wa Mataifa (UN), utatoa kibali cha kuruhusu kufanyika hivyo.
Msimamo huo wa Serikali umetolewa huku juhudi za kutafuta namna ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo zikiendelea mjini Kampala, Uganda, ambapo viongozi wa nchi zinazopakana na DRC wakikutana kutafuta msimamo wa pamoja.
Kauli hiyo ya Membe imetolewa wakati wapiganaji wa M23 wanaoipinga Serikali ya Kongo wakisisitiza kwamba sasa hivi wanajipanga kupambana kuelekea Bukavu, Kisangani kisha mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa.
Pia, imeitaka UN kutoa kibali cha kuyaruhusu majeshi ya umoja huo yanayolinda amani nchini Kongo kupambana waasi hao wa M23 ili kuweza kuwangoa na kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Sisi nchi za SADC na maziwa makuu tukiruhusiwa tukienda tuna uwezo wa kupambana na kuwaondoa hao M23 wanaosumbua lakini tunachohitaji ni ruhusa kutoka UN kwani wanajeshi wanaohitajika kufanikisha hilo ni 4,000, alisema Membe na kuongeza;
Hivi sasa majesi ya UN yaliyopo Kongo yanafanya kazi chini ya kibali namba sita cha UN ambacho kinawataka wao kulinda amani tu, tunaomba katibu mkuu wa umoja huo atoe kibali namba saba ili majeshi hayo yapambane na waasi wa M23 na kuwaondoa.
Membe alisema kuwa hivi sasa Serikali inasikitishwa kwa kushindwa kwa majeshi ya UN kuwazuia waasi wa M23 wasiteke mji wa Goma kwani kitendo hicho kinawapa nguvu waasi kuendelea na mapambano.
Tunawataka waasi wote waiachie Goma kwa kuwa kilichotokea hakikubaliki, tunasikitika vikosi vya UN kushindwa kuzuia hilo, tunamuomba katibu mkuu wa UN atoe kibali kuruhusu wanajeshi wake wapambane ili kuzuia waasi wasiendelee na vita, alisema Membe na kuongeza;
Hatukubaliani na utekaji huo na kwamba kama wakiendelea na kuiteka Bukavu, tutapata wakimbizi wengi kutoka Kongo.
Alisema wakati Serikali ya Tanzania ikitoa tamko lake kuhusu waasi hao leo viongozi wa nchi za maziwa makuu watakutana nchini Uganda na kufanya mazungumzo ambayo yatatoa uamuzi mgumu kama UN haitaruhusu majeshi yake au ya maziwa makuu kuingilia kati vita hivyo.
Kesho (leo) na keshokutwa (kesho) uamuzi mgumu utatolewa ambao utalitatua tatizo la Kongo moja kwa moja, alisema Waziri Membe na kuongeza;
Tunailaumu UN kwa kutokuchukua maamuzi hayo magumu ya kuweza kuzuia vita nchini Kongo.
Alisema vita hivyo vinavyoendelea Mashariki mwa Kongo vinasababisha wananchi wengi kukimbia maeneo yao na kufanya kwenda nchi za jirani na kuwa wakimbizi.
Membe alisema waasi wa M23 wanaofanya hivyo ni wale 1,000 ambao walikataa makubaliano yaliyofanyika Machi 23, 2009 ambayo yaliwataka askari wote waasi wajiunge na Serikali na kuwa kitu kimoja.
Alisema kati ya askari 4,000 waliokuwa waasi, 3,000 walikubali kujiunga na Serikali na 1,000 waligoma na kuendelea na uasi wao chini ya Jenerali Bosco Ntaganga.
Wanajiita M23 kutokana na kukataa makubaliano hayo na kwa muda wote tangu mwaka huo wamekuwa wakiishikilia Kivu chini ya Ntaganda, alisema Membe.
Kwanza kunatakiwa kuwepo majadiliano na Kabila na lazima yafikiwe makubaliano ya suluhu kabla ya kuchukua hatua nyingine yoyote, mmoja wa makamanda wa M23, Jean-Marie Runiga Lugerero alikaririwa akisema jana.
Msemaji rasmi wa M23, Vianney Kazarama alisema: Hatuishii Goma tu, sasa hivi tunaelekea Bukavu, Kisangani kisha Kinshasa.
Hadi kufikia jana, alisema kuwa wameshauteka mji mwingine wa Sake ulioko karibu na mpaka wa kaskazini mashariki wa Goma, ambao uko jirani na mji North Kivu wenye utajiri mkubwa wa madini.
Alisema pia kwamba kwa sa awanaelekeza nguvu zai pia katika mji wa Bukavu ambao uko mpakani mwa Kongo na Rwanda.
Taarifa zilizotolewa katika baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa jana zilieleza kwamba Rais Kabila anafanya tathmini kuhusu madai ya M23.
Chanzo Mwananchi