Tanzania ipo tayari kuwaondoa waasi wa M23

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
RAIS%2BJakaya%2BKikwete%2Bakizungumza%2Bna%2Bwaandishi%2Bwa%2Bhabari%2Bbaada%2Bya%2Bkukagua%2Beneo%2Bla%2Btukio%252C%2Bkambi%2Bya%2BJWTZ%252C%2BUkonga..JPG

Posted Ijumaa,Novemba23 2012 saa 9:4 AMKwa ufupi

“Kesho (leo) na keshokutwa (kesho) uamuzi mgumu utatolewa ambao utalitatua tatizo la Kongo moja kwa moja,” alisema Waziri Membe na kuongeza;
“Tunailaumu UN kwa kutokuchukua maamuzi hayo magumu ya kuweza kuzuia vita nchini Kongo.”

SERIKALI ya Tanzania imesema iko tayari kutoa bataliani moja ya wanajeshi 800 ili waweze kuingilia kati vita vinavyoendelea nchini Kongo kama Umoja wa Mataifa (UN), utatoa kibali cha kuruhusu kufanyika hivyo.

Msimamo huo wa Serikali umetolewa huku juhudi za kutafuta namna ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo zikiendelea mjini Kampala, Uganda, ambapo viongozi wa nchi zinazopakana na DRC wakikutana kutafuta msimamo wa pamoja.

Kauli hiyo ya Membe imetolewa wakati wapiganaji wa M23 wanaoipinga Serikali ya Kongo wakisisitiza kwamba sasa hivi wanajipanga kupambana kuelekea Bukavu, Kisangani kisha mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa.

Pia, imeitaka UN kutoa kibali cha kuyaruhusu majeshi ya umoja huo yanayolinda amani nchini Kongo kupambana waasi hao wa M23 ili kuweza kuwang’oa na kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Sisi nchi za SADC na maziwa makuu tukiruhusiwa tukienda tuna uwezo wa kupambana na kuwaondoa hao M23 wanaosumbua lakini tunachohitaji ni ruhusa kutoka UN kwani wanajeshi wanaohitajika kufanikisha hilo ni 4,000,” alisema Membe na kuongeza;

“Hivi sasa majesi ya UN yaliyopo Kongo yanafanya kazi chini ya kibali namba sita cha UN ambacho kinawataka wao kulinda amani tu, tunaomba katibu mkuu wa umoja huo atoe kibali namba saba ili majeshi hayo yapambane na waasi wa M23 na kuwaondoa.”

Membe alisema kuwa hivi sasa Serikali inasikitishwa kwa kushindwa kwa majeshi ya UN kuwazuia waasi wa M23 wasiteke mji wa Goma kwani kitendo hicho kinawapa nguvu waasi kuendelea na mapambano.

“Tunawataka waasi wote waiachie Goma kwa kuwa kilichotokea hakikubaliki, tunasikitika vikosi vya UN kushindwa kuzuia hilo, tunamuomba katibu mkuu wa UN atoe kibali kuruhusu wanajeshi wake wapambane ili kuzuia waasi wasiendelee na vita,” alisema Membe na kuongeza;

“Hatukubaliani na utekaji huo na kwamba kama wakiendelea na kuiteka Bukavu, tutapata wakimbizi wengi kutoka Kongo.”

Alisema wakati Serikali ya Tanzania ikitoa tamko lake kuhusu waasi hao leo viongozi wa nchi za maziwa makuu watakutana nchini Uganda na kufanya mazungumzo ambayo yatatoa uamuzi mgumu kama UN haitaruhusu majeshi yake au ya maziwa makuu kuingilia kati vita hivyo.

“Kesho (leo) na keshokutwa (kesho) uamuzi mgumu utatolewa ambao utalitatua tatizo la Kongo moja kwa moja,” alisema Waziri Membe na kuongeza;
“Tunailaumu UN kwa kutokuchukua maamuzi hayo magumu ya kuweza kuzuia vita nchini Kongo.”

Alisema vita hivyo vinavyoendelea Mashariki mwa Kongo vinasababisha wananchi wengi kukimbia maeneo yao na kufanya kwenda nchi za jirani na kuwa wakimbizi.

Membe alisema waasi wa M23 wanaofanya hivyo ni wale 1,000 ambao walikataa makubaliano yaliyofanyika Machi 23, 2009 ambayo yaliwataka askari wote waasi wajiunge na Serikali na kuwa kitu kimoja.

Alisema kati ya askari 4,000 waliokuwa waasi, 3,000 walikubali kujiunga na Serikali na 1,000 waligoma na kuendelea na uasi wao chini ya Jenerali Bosco Ntaganga.

“Wanajiita M23 kutokana na kukataa makubaliano hayo na kwa muda wote tangu mwaka huo wamekuwa wakiishikilia Kivu chini ya Ntaganda,” alisema Membe.

Kwanza kunatakiwa kuwepo majadiliano na Kabila na lazima yafikiwe makubaliano ya suluhu kabla ya kuchukua hatua nyingine yoyote,” mmoja wa makamanda wa M23, Jean-Marie Runiga Lugerero alikaririwa akisema jana.

Msemaji rasmi wa M23, Vianney Kazarama alisema: “Hatuishii Goma tu, sasa hivi tunaelekea Bukavu, Kisangani kisha Kinshasa.”

Hadi kufikia jana, alisema kuwa wameshauteka mji mwingine wa Sake ulioko karibu na mpaka wa kaskazini mashariki wa Goma, ambao uko jirani na mji North Kivu wenye utajiri mkubwa wa madini.

Alisema pia kwamba kwa sa awanaelekeza nguvu zai pia katika mji wa Bukavu ambao uko mpakani mwa Kongo na Rwanda.

Taarifa zilizotolewa katika baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa jana zilieleza kwamba Rais Kabila anafanya tathmini kuhusu madai ya M23.

Chanzo Mwananchi
 
Mie nadhani pamoja na taarifa kwamba Rwanda na Uganda wanachochea uasi DRC, lazima tujiulize ni lini DRC itakua na kuwa na jeshi lake lenye uwezo wa kupambana na nchi ndogo ndogo kama Rwanda na Uganda. DRC imeendelea kuwa kama mtoto asiyekua. Kabila amekuwa raisi kwa miaka mingi sana, hadi sasa alipaswa kuwa na jeshi ambalo Rwanda wangeogopa hata kuwagusa. Kama unajua nchi yako ina matatizo na jirani zako, unatengeneza jeshi ambalo lina nguvu na uwezo na nidhamu ili kukabiliana na chokochoko toka nje.

Miaka mingi sana Kabila analia kuhusu Uganda na Rwanda, sasa atendelea kulialia na kubebwa na Umoja wa Mataifa na nchi nyingine hadi lini? Kabila anaongoza DRC kama vile nchi yote ya DRC iko pale Kinshasha tu. Jeshi la DRC halina nguvu wala nidhamu, sasa anataka nani aweke nidhamu katika jeshi lake, UN? Kabila amekuwa anafanya nini siku zote hizi? Hebu fikiria kuna wakati ilibidi aokolewe na jeshi la Zimbabwe, pamoja na matatizo waliyonayo Zimbabwe.

Tunataka kuona inafikia mahali Rwanda wakichokoza DRC Kabila anamwambia Kagame ukiendelea na uchokozi wako itanichukua siku mbili kwa jeshi langu kufika IKulu Kigali na kukutoa madarakani ili nije kunywea chai kwenye ikulu yako. (Refer Nyerere kwa Idd Amin; uwezo wa kukupiga tunao, sababu ya kukupiga tunayo na nia ya kukupiga tunayo).

Kwa upande wa Tanzania, ikiwa ni kweli Rwanda na Uganda wanahusika katika kuchochea maasi DRC, basi inabidi tuliweke wazi hili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwamba Tanzania hatuko tayari kuwa na wanachama katika Jumuiya wanaochechea vita na jirani zetu, kwa sababu hilo ndilo lililovunja jumuiya ya kwanza. Tuwaambie wazi Kagame na Museveni, kwamba wakiendelea na uchokozi huu dhidi ya DRC, itabidi eidha wao wajitoe kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, au sisi Tanzania tutajitoa. Lazima JK aelewe kwamba kuwa na msimamo thabiti katika mambo kama haya ni sababu mojawapo ya Nyerere kuheshimika sana kimataifa. Tusiruhusu watu kama kina Kagame na Museveni wafanye michezo ya kitoto yenye kuhatarisha Jumuiya tunayopigania sana kuiimarisha.
 
ningetamani mamluki wa rwanda na uganda wang'olewe hata leo kwani ni balaa na taswira mbaya kwa bara letu linaloendelea kusakamwa na matatizo yasiyoisha!!
 
umenena vyema mkuu, lakini nasikitika kukueleza leo hii kuwakuta viongozi kama nyerere ni sawa na kumtafuta nyangumi jangwani. Aina ya viongozi tulionao sasa ni wachumia tumbo na wanaojali nafsi zao pekee tu! na ndio maana viongozi wahuni kama kagame,joyce banda na museveni wanazidi kushika kazi barani kwetu.
 
Mie nadhani pamoja na taarifa kwamba Rwanda na Uganda wanachochea uasi DRC, lazima tujiulize ni lini DRC itakua na kuwa na jeshi lake lenye uwezo wa kupambana na nchi ndogo ndogo kama Rwanda na Uganda. DRC imeendelea kuwa kama mtoto asiyekua. Kabila amekuwa raisi kwa miaka mingi sana, hadi sasa alipaswa kuwa na jeshi ambalo Rwanda wangeogopa hata kuwagusa. Kama unajua nchi yako ina matatizo na jirani zako, unatengeneza jeshi ambalo lina nguvu na uwezo na nidhamu ili kukabiliana na chokochoko toka nje.

Miaka mingi sana Kabila analia kuhusu Uganda na Rwanda, sasa atendelea kulialia na kubebwa na Umoja wa Mataifa na nchi nyingine hadi lini? Kabila anaongoza DRC kama vile nchi yote ya DRC iko pale Kinshasha tu. Jeshi la DRC halina nguvu wala nidhamu, sasa anataka nani aweke nidhamu katika jeshi lake, UN? Kabila amekuwa anafanya nini siku zote hizi? Hebu fikiria kuna wakati ilibidi aokolewe na jeshi la Zimbabwe, pamoja na matatizo waliyonayo Zimbabwe.

Tunataka kuona inafikia mahali Rwanda wakichokoza DRC Kabila anamwambia Kagame ukiendelea na uchokozi wako itanichukua siku mbili kwa jeshi langu kufika IKulu Kigali na kukutoa madarakani ili nije kunywea chai kwenye ikulu yako. (Refer Nyerere kwa Idd Amin; uwezo wa kukupiga tunao, sababu ya kukupiga tunayo na nia ya kukupiga tunayo).

Kwa upande wa Tanzania, ikiwa ni kweli Rwanda na Uganda wanahusika katika kuchochea maasi DRC, basi inabidi tuliweke wazi hili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwamba Tanzania hatuko tayari kuwa na wanachama katika Jumuiya wanaochechea vita na jirani zetu, kwa sababu hilo ndilo lililovunja jumuiya ya kwanza. Tuwaambie wazi Kagame na Museveni, kwamba wakiendelea na uchokozi huu dhidi ya DRC, itabidi eidha wao wajitoe kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, au sisi Tanzania tutajitoa. Lazima JK aelewe kwamba kuwa na msimamo thabiti katika mambo kama haya ni sababu mojawapo ya Nyerere kuheshimika sana kimataifa. Tusiruhusu watu kama kina Kagame na Museveni wafanye michezo ya kitoto yenye kuhatarisha Jumuiya tunayopigania sana kuiimarisha.

Mkuu Synthesizer, mimi nafikiri suala la DRC ni la siku nyingi sana na limeoteshwa mizizi na mataifa makubwa kwa sababu ya utajiri wake. Hakuna asiyejua kwamba vita ya DRC ni ya mataifa makubwa hasa Marekani kupitia mawakala wake ambao ni Uganda na Rwanda.
Hivi huoni haki za binadamu zinazovunjwa Uganda na Rwanda lakini ndio wanapewa tuzo za uongozi bora? Wandamanaji wanavyopingwa huko Uganda na hakuna taifa lolote linalokemea. Udiktate wa Kagame unaitwa utawala bora kwa kuzima wapinzani. Suala siyo udogo wa nchi, bali nani na nini kipo nyuma ya nchi hiyo?

Kabila anahitaji kuwekeza sana kwenye swala la usalama na jeshi kwa kuvisuka upya kabisa kama amepata uhuru juzi tu. Na hii ni kazi pevu ukilinganisha na mazingira yaliyopo sasa hivi. Umoja wa Afrika unaweza kusaidia lakini hauwezi kufanya vile milele. Kabila suke tu usalama na jeshi lake kwa mbinu kali.
 
Lazima kuwe na sheria, bunge liizinishe 80%+ majority ndio rais awe na uwezo kutudrag kwenye vita visivyotushusu.
 
Tuna matatiZO mengi sana ya kusolve hApa nchini! Membe aache kutafuta sifa za kijinga.....
 
Wanakurupuka kusema. Wanapigana wenyewe kwa wenyewe kutokana na uongozi mbovu sisi tukafanye nini huko. Kama Rwanda na Uganda wapo upande wawaasi situtakuwa tunapigana wenyewe Inhci za EAC.
 
Suala la Kongo linahitaji busara lakini pia ni matokeo ya namna viongozi wa Afrika wanavyoingia madarakani
 
nguvu za kuwaondoa waasi wasiotuhusu mnazo, walioficha ma-billion uswisi na vibaka wa hela za Rada, Wanaouza twiga wetu hao mpaka tupewe taarifa kamili na serikali husika. aisee ukistaajabu ya mussa....

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
Mkuu Synthesizer, mimi nafikiri suala la DRC ni la siku nyingi sana na limeoteshwa mizizi na mataifa makubwa kwa sababu ya utajiri wake. Hakuna asiyejua kwamba vita ya DRC ni ya mataifa makubwa hasa Marekani kupitia mawakala wake ambao ni Uganda na Rwanda.
Hivi huoni haki za binadamu zinazovunjwa Uganda na Rwanda lakini ndio wanapewa tuzo za uongozi bora? Wandamanaji wanavyopingwa huko Uganda na hakuna taifa lolote linalokemea. Udiktate wa Kagame unaitwa utawala bora kwa kuzima wapinzani. Suala siyo udogo wa nchi, bali nani na nini kipo nyuma ya nchi hiyo?

Kabila anahitaji kuwekeza sana kwenye swala la usalama na jeshi kwa kuvisuka upya kabisa kama amepata uhuru juzi tu. Na hii ni kazi pevu ukilinganisha na mazingira yaliyopo sasa hivi. Umoja wa Afrika unaweza kusaidia lakini hauwezi kufanya vile milele. Kabila suke tu usalama na jeshi lake kwa mbinu kali.

Mie nadhani pamoja na taarifa kwamba Rwanda na Uganda wanachochea uasi DRC, lazima tujiulize ni lini DRC itakua na kuwa na jeshi lake lenye uwezo wa kupambana na nchi ndogo ndogo kama Rwanda na Uganda. DRC imeendelea kuwa kama mtoto asiyekua. Kabila amekuwa raisi kwa miaka mingi sana, hadi sasa alipaswa kuwa na jeshi ambalo Rwanda wangeogopa hata kuwagusa. Kama unajua nchi yako ina matatizo na jirani zako, unatengeneza jeshi ambalo lina nguvu na uwezo na nidhamu ili kukabiliana na chokochoko toka nje.

Story ya Rwanda, Uganda na DRC is very complicated na itakuumiza sana kichwa na jibu hautapata. In short sie Watanzania tungejua kusoma alama za nyakati tusingepeleka hata mgombo pale DRC. Rais Kabila ni Mtusi, Rais Mseven ni Mtusi, Rais Kagame ni Mtusi so wale wanacheza ngoma wanayoijua wenyewe na sisi WTZ lazima tufikirie na tuchambue vizuri ili kupeleka majeshi yetu kule maana ile ngoma inayochezwa kule ni ngoma ya Watusi kujenga Hima Empire, so when you see president Kabila crying is not true at all tena kwa taarifa yako naskia majeshi ya DRC yakisonga mbele Kabila anatoa order eti warudi nyuma wajipange vizuri. What hell on earth ushasikia wanajeshi 1000 wakasumbua nchi wewe.Hamna kitu ule ni usanii tu wa hawa marais amboa ni three brothers
 
sasa mambo ya wakongo yanawahusu nini watanzania? Au Membe kuna issue anaitafuta kuelekea 2015,hivi hatuyaoni yaliyowakuta kenya kwa alshabaab?
 
Membe ardhi yetu ya ziwa Nyasa tunaihitaji sana kkuliko madini ya Congo hilo moja
la pili tunayataka mabilion yetu ya uswiss,la tatu uje utueleze zile kashfa wakati ukiwa ofisa ubalozi kule SA zilikuaje
 
JK peleka majeshi congo ili malawi waweze kuazisha vita ya kudai ziwa lao kwa nguvu bila shaka tz haitaweza kuwa na two fronts kwa wakati mmoja hilo litatupeleka katika ugumu wa maisha zaidi na kuamsha hasira mitaani zitakazo pelekea kuanguka serekali ya CCM
USISAHAU MADAI YA ZANZIBAR KUTOKA KTK muungano ......jk azisha vita kwa faida ya malawi,zanzibar na wapizani wata take adventages of yr action..
sifa za kijinga zitaiangamiza nchi soon
 
Hebu fikiria UN ya Congo:wanajeshi Pakstani,Fuel supplier to UN facilities PDL TOLL from India hivi huoni kuwa hawa wako kibiashara zaidi kuliko malengo ya UN?.
 
Back
Top Bottom