Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,495
- 5,532
Habari za wakati huu,
Katika suala la ujenzi wa uchumi na maendeleo moja kati ya vitu muhimu sana katika labour force ni skills.Mfumo wa elimu unalenga kuwapatia watu skills and knowledge.
Skills ni uwezo wa kufanya jambo kikamilifu na Knowledge ni uwezo wa kuelewa jambo kikamilifu. So ninaposema kama taifa tuna uhaba wa skills namaanisha kwamba tuna idadi kubwa ya watu ambao hawana uwezo wa kufanya jambo lolote kikamilifu/hawajua wanaweza kufanya jambo gani kikamilifu.
Ninaposema kwamba watu wengi hawana skills simaanishi kwamba watu wote ila asilimia kubwa.Kwa mtazamo wangu kuna aina mbili za skills (Transferable skills na Non-Transferable skills) Sasa kwa taifa letu wengi wamepawaya katika aina zote mbili za skills na mbaya zaidi mfumo wetu wa elimu haujaaangalia namna sahihi ya kuhakikisha kwamba labour force inakuwa na skills zote muhimu ili waweze kujiajiri au kuajiriwa.
Katika semina moja tuliwahi kuambiwa kwamba. Kama kazi ambayo unatafuta huwezi kuifanya mwenyewe bila kuajiriwa basi huna competency ya kutosha. Mfano kama wewe ni mwalimu unatafuta kazi ya ualimu na hujaweza hata kufungua tution centre basi kuna walakini juu ya uwezo wako wa kufundisha.Kwa lugha nyepesi kama huwezi kujiajiri katika fani yako basi hufai hata kuajiriwa.
Leo niwakaribishe tujadili iwapo mfumo wetu wa elimu na malezi una muaandaa mtu kikamilifu kuweza kuajiriwa au kujiajri katika fani yake.
Karibuni