Nani mkombozi wa Elimu yetu?

lulu za uru

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,181
2,680
Tusizunguke sana. Kuna mabadiliko ya mtaala inasemekana ni ya SITA katika mfumo wa Elimu. Mimi nami ni mdau hivyo nilipata wasaa wa kuhudhuria Warsha ihusuyo mabadiliko hayo.

Cha kushangaza kikubwa nilichotoka nacho ni jinsi au namna gani mwalimu anapaswa kujaza lesson plan, scheme of work iweje na blabla kama hizo.

Sikatai Lesson plan na Scheme zina percentage zake lakini sidhani kama ni kipaumbele saaaana. Kuna tatizo la ajira kubwa Sana, mabarobaro wanapomaliza vyuo wengi wanaogopa kujiajiri, wanataka kuajiriwa, watu wanawacheka eti unafikaje chuo ushindwe kujiajiri.

Hivi tangu lini shamba lililolimwa mahindi likatoa maharage, ukipanda maharage utavuna maharage mahindi utavuna mahindi, mtoto tangu Yuko chekechea mind set yake anasoma Ili aajiriwe ndivyo inavyosetiwa.

Akimaliza chuo analaumiwa kwanini asijiajiri, jamani kwenye hizi Warsha hebu tujaribu kuchomekea masuala mtambuka kama hayo. Mtoto aanze kuambiwa ukweli at least kuanzia darasa la pili kuwa anasoma lkn ajira ni 20/50 kwahivo wanapewa ukwl kidogo kidogo mpaka aje amalize chuo kama ni wa kijiongeza naye atajiongeza.

Masuala makubwa yenye matokeo chanya, kukazana na lesson plan iandikwe vipi siyo poa na huku Kuna mambo kibao ya kuwafeed hawa watoto. Ninaamini kitovu kikuu cha mabadiliko ni kuifanya Elimu ya Tanzania, imuwezeshe kijana kutoka na life skill itakayomsaidia maisha.

Lakini wawezeshaji wa semina wanakazana na scheme na lesson plan, haya bhana sisi tupo. Labda Kuna siku mkombozi atatokea, hivi China walihangaika na hayo Malesson plan au walifanyaje?
 
Back
Top Bottom