Tanzania imeishauri Ethiopia kuchunguza kiini cha raia wake kuondoka nchini humo kinyume na utaratibu na kusababisha mrundikano wa wafungwa Tanzania

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Tanzania imeishauri Ethiopia kuchunguza kiini cha raia wake kuondoka nchini humo kinyume na utaratibu, jambo linalosababisha mrundikano wa wafungwa ambao wanakamatwa katika nchi wanazopita kama wahamiaji ikiwemo Tanzania.

Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, kando ya mkutano wa 33 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mara baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt Workneh Gebeyehu.

Amemueleza Dkt Gebeyehu kuwa mpaka sasa zaidi ya raia 1,300 wa Ethiopia wanashikiliwa katika magereza mbalimbali nchini Tanzania huku idadi ya wanaoendelea kukamatwa ikiongezeka.

Wakati wa mazungumzo hayo ya Profesa Kabudi na Dkt Gebeyehu, Tanzania na Ethiopia zimekubaliana kuchukua hatua za pamoja zitakazowezesha kurejeshwa wafungwa na wahamiaji wa Ethiopia wanaoshikiliwa Tanzania kwa utaratibu utakaokubalika.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Ethiopia amekiri kuwepo kwa tatizo la vijana wa nchi hiyo kuondoka kinyume cha utaratibu na kuitumia Tanzania kama mapito wakielekea katika nchi za Kusini mwa Afrika na Ulaya, hivyo wataendelea kuweka mikakati madhubuti ili kukabiliana na hali hiyo.

Pia ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano wake katika suala la Wahamiaji kwa kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu aaia wa Ethiopia wanaoshikiliwa Tanzania.
 
Huko si ndiyo kuna ma SGR, Viwanda kila kona ,Mandege kama yote na miradi mikubwa mikubwa kuelekea uchumi wa kati na kuwa Dona kantri.

Aache kujibagaza asubiri wabongo watakapoanza kukimbia ndiyo atajua SGR ,sijui Dream liner hazina mpango.
 
Huko si ndiyo kuna ma SGR, Viwanda kila kona ,Mandege kama yote na miradi mikubwa mikubwa kuelekea uchumi wa kati na kuwa Dona kantri.

Aache kujibagaza asubiri wabongo watakapoanza kukimbia ndiyo atajua SGR ,sijui Dream liner hazina mpango.
Ethiopia hali ni tete. Sehemu nyingi ni kukame, wana tribal conflict nyingi na mpaka dakika hii kuna watu zaidi ya laki 8 wapo kwenye kambi za wakimbizi wa ndani (internally displaced persons). Yaani Serikali inajidai kuwa na mpunga na kuna flyovers za ukweli na nyingi ila raia ni choka mbaya. Walipofikia wao ndipo Magufuli anafuata njia hiyo hiyo

In short wamewekeza kwenye vitu na sio watu na hivyo vitu wala haviwasaidii sana raia wanyonge walio wengi. No wonder watu wao wapo radhi warisk maisha wakafungwe nje huko kuliko kupata taabu Nchini kwao
 
Huko si ndiyo kuna ma SGR, Viwanda kila kona ,Mandege kama yote na miradi mikubwa mikubwa kuelekea uchumi wa kati na kuwa Dona kantri.

Aache kujibagaza asubiri wabongo watakapoanza kukimbia ndiyo atajua SGR ,sijui Dream liner hazina mpango.
Hakuna ajira TZ watu lazima wajiongeze. Tatizo ni kwamba wanazingua kutoa passport

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie huyo waziri anachokishauri Ethiopia ndio kinachoenda ikumba nchi yake sooner or later wasipoona namna ya kujenga watu.

Kuna uhakika kuwa RAIA watanzania kwa sasa wakipewa option ya kuukataa utanzania basi watakaoukubali ni wala raha kama Bashite tu wengine wote wanamuunga mkono pompeo BILA kujali tena.
Nchi imepoteza shauku ya wananchi wake kuipenda bila sababu, mwambie waziri arejee dira ya TAIFA 2025 kipengele cha culture ataelewa anachoishauri Ethiopia kwa sasa kwake kuna Bomu linajisokota taratibuuuu
 
Back
Top Bottom