Tanzania ikifunga mpaka wa Namanga na Taveta-Holili, hakika watakiri kuwa Kilimanjaro ipo Tanzania

Huwa nakerekwa sana na haya wafanyayo wakenya
Lakini kuna siku itakula kwao
Mlima ule upo
Siku viongozi wetu watashituka naona utakuwa mvutano mkubwa
 
Kwanza ni kukubali kuwa Wakenya wametuzidi kiujanja, baadae tutafute njia ya kujitoa hapa tulipo sio kufunga mipaka huko ni kushindwa kabisa. Kwanini wao wameweza sisi wenye mali tushindwe? Hao wasimamizi wa utalii wajitathimi kama wanaweza kuendelea na majukumu au waachie nafasi.
 
Nashangaa hawa wakenya sijui wanatumia nini kujitangaza. Mfano India ukionekana mtu mweusi wanakuuliza unatoka Kenya au South Africa? Yaani hizo ndio nchi wanazozijua Africa
 
kwa hyo unawaonea huruma? mbona wao hawaoni huruma kuingiza watalii na kuwadanganya mt kilimanjaro upo kenya? bora mh anguefunga hilo boda ili heshima iwepo
Sins huruma na hawa jamaa. Mi naona njaa zao zingekuwa fursa ila Ngosha. Ilibidi tuwauzie unga badala ya mahindi ila Ngosha hajaliona kwenye mkakati wa viwanda.
 
.
Hivi majuzi kuna mwandishi huko Ulaya alipotosha dunia kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya, TANAPA walipo mfuata akadai waende kwenye Media aliyoitumia kutolea habari hiyo ili wakanushe na sio kumfuata kienyeji.

Nilisoma uzi ule kwa uchungu mkuu (nadhani ilikuwa ni HuffPost News). Wengi walidai kuwa Tanzania ina viongozi ambao hawajali soko la Utalii.

Mchangiaji mmoja akasema, I quote "Kenyans, Tanzania don't care if you are dragged into our business or not, sisi kwetu #HapaKaziTu).

Mwingine ambaye ndio chanzo cha mimi kufungua uzi huu ni aliyedokeza kwamba kama tukifunga mpaka wa Namanga na ule wa Taveta-holili watalii wasiingie, hakika wakenya, watalii na wengi waliolishwa maneno kuwa Kilimanjaro ipo Kenya wataisoma namba na kujua kuwa kumbe kweli #Kili ni Tanzania na Tanzania ni #kili.
..huu Uzi tutafute namna ya kufikisha ujumbe, tungejali Sana diplomatic relations Na Kenya endapo wangetuheshimu, lakini upo wazi kabisa kuwa hawatuheshimu na wamekuwa wakituchokonoa Sana kwenye rasilimali zetu. Sasa huo mpaka ufungwe Tu, Kama mbwai mbwai
 
..
Pale kuna biashara nyingi zinaendelea zaid ya mlima kilimanjaro. Na hata tukifunga yawezekana Tz tukapoteza zaid....cz hao watalii hawaji tu kuutembelea mlima kilimanjaro.....kumbuka kenya nao wanavivutio na wanajua kujitangaza kuliko sisi. Kwahyo tukifunga yawezekana watalii wanaokuja kenya wakaishia kenya hapo then wakageuza. Tatizo lipo kwetu, kwanini mkenya akisema mt kilimanjaro ipo kenya anaaminika kuliko sisi? Kwahyo. Afu kumbuka mt kilimanjaro iko karibu na Nairobi kuliko dar.
.issue siyo Kuwa Na Nairobi kwa maana pale Klm Kuna international Airport so ndege yoyote inatua moja kwa moja, Na si kweli kuwa mpaka ukifungwa sisi ndo tutakaopoteza Sana, kiufupi Kenya inaitegemea Sana Tz kuliko sisi tunavyoitegemea, hata nikikuuliza kuwa sisi tunategemea nini frm Kenya nafikiri ntakuwa nimekupa assignment
 
...
Sasa mpaka ufungwe halafu iweje ??kazi ya mpaka ni kupitisha watalii tu ?? Serikali iandae program maalumu ya kuitangazia dunia vivutio vyetu sio kila siku tunawalaumu Wakenya na pia waweke mazingira rafiki kwenye vivutio vyetu ,kuwe na paramedics unit na standby helkopters kwa ajili ya emergency ,huenda kungekuwa na Helkopter basi kifo cha yule dereva bingwa wa magari SA kingehepukika
.unajua maana ya mpaka kufungwa?
 
...e
Mipaka hiyo ikifungwa tutashtakiwa kwa kosa la kuua wakenya kwa njaa. Mahindi, mbaazi, ngwara, vitunguu n.k vitaendaje Kenya? Na kwa jinsi walivyotufanya solo lao la sabuni, biscuits, maziwa ya brookside, spices za tropical n.k watauza wapi? Ukitaka Kenya iwe maskini na utapiamlo wafungie hiyo mipaka.
umesema kiutani lakini Ni ukweli mtupu
 
...
Mnalalamika wakati hamna shirika la ndege la kwetu lakuwatoa huko ulaya kuja hapa wakati kq mshirika wa star alliance anawatoa huko mpaka Kenya wanawambia njoo uone Mt Kilimanjaro baadae wanapelekwa maasai Mara wakimaliza wanamleta tz kuona mlima kwa siku chache kabla awajawarudisha kwao.Kuna uhusiano mkubwa wa uimara wa shirika la ndege na kukua kwa sekta ya utalii.
...ni kweli, lakini suala la kufungiwa mipaka litaenda sambamba Na uimarishaji wa ATCL
 
hapa ndo naona umuhimu wa mtu kama trump kwenye ishu tamu kama hizi za kufunga mipaka... LOWASSA please Make bongo Great Again 2020
 
Tatizo lililopo sisi watanzania sio wazalendo wa nchi yetu km walivyo wakenya!wenzetu wanafanya hayo yote kuivutia nchi yao sababu wanaipenda.usishangae hata mtanzania hajui mlima kilimanjaro uko mkoa gani?!sisi watanzania binafsi hatupendani tutapenda nchi yetu na kufa kwa ajili yake la hasha hatuwezi abadani.
Sisi tunataka na tunapenda na tunakalia umbea tu.imebaki watangaze sasa na tanzania iko kenya!
 
Tufufue kwanza shirika letu la ndege.
Lakini kufunga mpaka sio suluhisho.
East Afrika ni moja!
Tuhubiri amani upendo na mshikamano jamani hawa wakenya wana utoto na usavage na sisi tukifuata mkondo huo who will be the voice of reason in EA?
 
..
.issue siyo Kuwa Na Nairobi kwa maana pale Klm Kuna international Airport so ndege yoyote inatua moja kwa moja, Na si kweli kuwa mpaka ukifungwa sisi ndo tutakaopoteza Sana, kiufupi Kenya inaitegemea Sana Tz kuliko sisi tunavyoitegemea, hata nikikuuliza kuwa sisi tunategemea nini frm Kenya nafikiri ntakuwa nimekupa assignment
Nani ana uchumi imara kati ya hizo nchi mbili......go and work on that assignment.....mi nshamaliza yang
 
Nani ana uchumi imara kati ya hizo nchi mbili......go and work on that assignment.....mi nshamaliza yang
Kenya wanauchumi siyo imara ila Ni mkubwa ukilinganisha Na Tz, lakini Tz Ni suala la muda Tu, Tz Ina assets nyingi kuliki Kenya, yaani at very big difference, so Tz Ina uwezo wa kuipiga gap kubwa Sana Kenya coz Kenya uchumi wake siyo guaranteed, Na soon Tanzania inakuwa big competitor wa Kenya Na baadaye kuiacha Kenya mbali, so Kenya siyo nchi ya kuipa headache Tz hata kidogo, one day you will realise hata wakenya wenyewe wame focus hili
 
Kenya wanauchumi siyo imara ila Ni mkubwa ukilinganisha Na Tz, lakini Tz Ni suala la muda Tu, Tz Ina assets nyingi kuliki Kenya, yaani at very big difference, so Tz Ina uwezo wa kuipiga gap kubwa Sana Kenya coz Kenya uchumi wake siyo guaranteed, Na soon Tanzania inakuwa big competitor wa Kenya Na baadaye kuiacha Kenya mbali, so Kenya siyo nchi ya kuipa headache Tz hata kidogo, one day you will realise hata wakenya wenyewe wame focus hili
Kenya is the 3rd biggest investor in our economy after Uk and USA kwahyo kodi na ajira tunayopata ni kubwa sana zaid ya ugomvi wa kufungiana mipaka cz ya mt kilimanjaro....
 
Kenya is the 3rd biggest investor in our economy after Uk and USA kwahyo kodi na ajira tunayopata ni kubwa sana zaid ya ugomvi wa kufungiana mipaka cz ya mt kilimanjaro....
My point Ni kuwa we shouldn't depend on Kenyans kwa sababu we had enough to depend on ourselves. Ni ujinga Tu wa serikali zilizopita kubweteka mpaka Kenya ikatupiga gap, Na historia Inachangia pia, lakini Mimi ninaamini kwa namna yoyote Ile Kenya Ina msaada Mdogo kwa Tz, hakuna cha maana walicho invest huku zaidi ya supermarkets, banks, Na kutuuzia sabuni.

Besides bidhaa nyingi zitokazo Kenya siyo za wakenya Ni za makampuni ya kimataifa yaliyowekeza kenya
 
Watu duniani wanajaribu kufungua mipaka yao ila nyie watani wetu mnafikiria kufunga mipaka, it's 2016 for Christs sake, we shouldn't embrace these colonial borders, market your country out there instead of always whining like a bunch of sore losers. Going through this thread just shows how much you guys are close minded, you have a very long way to go.
 
Back
Top Bottom