Virusi vya corona: Anna Mghwira atangaza malori ya Kenya kutovuka mpaka wa Tanzania wa Holili

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,312
Virusi vya corona: Anna Mghwira atangaza malori ya Kenya kutovuka mpaka wa Holili
17 Mei 2020


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amesema kwamba malori ya mizigo kutoka Kenya hayataruhusiwa kupita katika mpaka wa Holili.

Katika muongozo mpya unaolenga malori ya mizigo ya mataifa mengine yanayoingia na kutoka nchini humo, Mkuu huyo wa mkoa amesema kwamba masharti hayo mapya yanalenga kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

''Malori yote yanayobeba mizigo na yanayomilikiwa na raia wa Tanzania, na yangependelea kuingia Tanzania ama yanamilikiwa na raia mwingine wa kigeni lakini bidhaa hiyo iliagizwa na Mtanzania , tafuta lori jingine ili kusafirisha mizigo hiyo inakoelekea.''

Malori kutoka mataifa mengine hayataruhusiwa kuingia'', alisema. Bi Mghwira

Amesema kwamba serikali ya Tanzania haitakubali mazingira ya kibiashara kuwekwa katika hali ya ambayo haihusiani na ambayo inaleta utata mkubwa. 'Tusiendelee kuharibiana biashara na kuweka mazingira ya kiabiashara katika hali ambayo inaleta utata'. Alisema Bi.Mghwira

Bi Mghwira hususan alizungumzia kuhusu malori ya mizigo kutoka Kenya baada ya tangazo la rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumamosi kwamba amefunga mpaka na Tanzania pamoja na Somalia kwa madai kwamba maambukizi mapya nchini Kenya yanapitia mpaka wa Holili.

Maelekezo hayo ya Mghwira yamechukuliwa katika mkanda wa video ambao umesambaa mitandaoni nchini Kenya na Tanzania. Mkuu huyo wa mkoa ameithibitishia BBC kuwa ni kweli ametoa maelekezo hayo.

Hata hivyo, mapema hii leo Rais Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania haitafunga mipaka yake na nchi jirani.

Kenya ilifunga mpaka wake na Tanzania pamoja na Somalia kwa muda wa siku 30 kuanzia saa sita usiku wa Jumamosi Mei 16.

Kenya ilifunga mpaka wake na Tanzania pamoja na Somalia kwa muda wa siku 30 kuanzia saa sita usiku wa Jumamosi Mei 16.
Je rais Uhuru Kenyatta alisemaje?

Katika hotuba yake kwa taifa Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumamosi alisema hatua hiyo inajumuisha udhibiti wa usafiri wa watu kutoka mataifa hayo kuingia nchini Kenya.

Hatahivyo alisema kwamba usafirishaji wa mizigo utaendelea kati ya Kenya na mataifa hayo mawili.

Marufuku hiyo ya kuzuia watu kutoka Tanzania kuingia nchini Kenya ilianza siku ya Jumamosi kuanzia saa 6 usiku ambapo ni mizigo tu itakayoruhusiwa kupita.

Kwa upande wa Somalia alisema kwamba masharti ni hayo hayo, mizigo peke yake ndio itakayoruhusiwa.

Vilevile alisema kwamba madereva watakaoingia nchini Kenya kuleta mizigo watatakiwa kupima corona kwanza.

Rais Uhuru Kenyatta alitoa uamuzi huo wakati wa mkutano na vyombo vya habari kutangaza kuhusu masharti mapya pamoja na idadi ya wagonjwa wapya waliopatikana.

Je ni kwanini Kenya ilichukua uamuzi huo?

Hatua hiyo ya Kenya inajiri baada ya kutangaza kwamba kati ya wagonjwa wanaothibitishwa nchini humo, 43 waliingia Kutoka Somalia na Tanzania.

Kati ya hao 14 waliingia kupitia mpaka wa Wajir, 16 waliingia kupitia mpaka wa Namanga , 10 kupitia mpaka wa Isebania, 2 kupitia Lunga Lunga na mmoja kupitia mpaka wa Loitoktok.

Uhuru Kenyatta alisema kwamba madereva wa malori 78 ambao ni raia wa kigeni walikutwa na virusi vya ugonjwa huo. Uhuru anasema madereva hao walizuiwa kuingia Kenya katika mipaka tofauti.

Kumradhi, taarifa hii awali ilimnukuu kimakosa Waziri wa Afya wa Tanzania Bi Ummy Mwalimu badala ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira. Tunamuomba radhi Waziri Ummy Mwalimu, Serikali ya Tanzania na wasomaji wetu kwa usumbufu uliotokea.

Chanzo: BBC

 
Kenya ndio nchi ya kiafrika yenye uwekezaji mkubwa zaidi Tanzania.

Uwekezaji wa Kenya ni zaidi ya Trillion 2 za kitanzania hapa Tanzania.

Losers sio Kenya ni Tanzania.

Miaka kibao tumekua na surplus balance of payments na Kenya maana yake tunauza zaidi kenya kuliko tunavyonunua kwao kwa mujibu wa reports za BOT.

Hapa maana yake Tanzania wazalishaji wake wanakosa masoko ya walaji au wateja wao wa Kenya.

Kwenye biashara sio kwamba Kenya alikua hawezi kupata bidhaa kutoka Tanzania mahala pengine bali ni mikataba ya nchi na nchi hivyo basi bado Kenya anaweza kupata bidhaa zetu mahala pengine bila shida.

Ni jambo la Muda Uganda, Rwanda watafunga mipaka na sisi. Hii Dunia hatuna kitu unique kwamba bila sisi hizo nchi watakufa, bado wana altenative nyingi.

Kama ni bandari bado uganda na rwanda wanaweza kutumia ya Mombasa, kama ni chakula kama mahindi wanaweza kupata zambia ambao wana commercial farming ya mahindi na kwingineko. Zambia anaweza kutumia beira au durban.

Siasa za miaka ya 60,70 hazima naana dunia ya leo. Siasa za vita, sijui uadui, sijui mabeberu zilishapitwa na wakati ila naona siai ndio tunazikumbatia sasa, matokeo yake tutayaona soon.
 
Back
Top Bottom