Tanzania ikifunga mpaka wa Namanga na Taveta-Holili, hakika watakiri kuwa Kilimanjaro ipo Tanzania

...dugu angu MK254 ona hii kitu iko correct sure?

TODAYS asante kwa kuniita huku lakini haya masuala ya mlima Kilimanjaro huwa hayaniumizi kichwa tena, tumeyajadili hadi tumechoka. Mkitaka na nyie mseme mlima Kenya upo Bongo uone kama kuna Mkenya atalalamika, kwanza itakua raha sana kama tunaweza kupata watalii kadhaa wanaokuja kwa njia hiyo.

Tatizo nyie mpo mpo tu, watu wanapiga hela wakati vivutio vyenu vipo kama maua na haviwafaidishi. Leo hii Tanzania ndio inaongoza Afrika yote kwa ubora wa vivutio, lakini hamna bidii ya kuvitangaza. Wazungu wengi wanashukia Kenya halafu wanakuja huko na sio kwa Kilimanjaro tu, wanatangaziwa vivutio na Wakenya kama packages, kwamba aje kenya ashangae vichache vilivyomo kwetu, ashushe mzigo halafu hatimaye aishie Bongo, halafu wanakuja kwa mamia ya maelfu. Badala ya nyie kutia bidii, mumekaa hapo mnalalamika kwanini wapitie Kenya kwanza.

Mtaishi kulalamika kila siku kuhusu mlima, mtafuata na kugombana na magazeti ya dunia yote, lakini hakuna mtu ana shughuli.
Nataka niwape siri, leo hii mjikite katika kutangaza mlima Kilimanjaro, uzuri wake, umuhimu wake na masuala yote yanayouhusu, mtangazie hadi na Watanzania wenyewe ili kila mmoja akitoka kule nje awe anaongea kuhusu uzuri wa huo mlima. Msipoteze hela nyingi kutangaza mahali ulipo mlima, maana watalii hawana haja, wengi hutaka kujua nini watafaidi wakija. Taratibu mtashangaa kuona matokeo.

Halafu kikubwa, Wabongo hampendi kuitalii nchi yenu, nimeishi nanyi kwa muda mrefu, unakuta wengi mnataja taja Kilimanjaro lakini hamna habari kuihusu, ukiuliza Mtanzania akutajie mambo machache kuhusu huo mlima wala hana habari, yeye anaishia kutumia hela nyingi kwa raha za Dar.
Wakenya tunatokea kwetu na tunakuja vikundi kulipia kuukwea huo mlima, tunatembelea mbuga zenu wenyewe tena kwa hela zetu. Tunatembelea mbuga zetu pia. Jifunze kupenda Afrika yako na nchi yako wacha kulalamika ovyo.
 
Back
Top Bottom