Tanzania hatuna Comedians bali tuna waropokaji tu. Comedians wa Kitanzania humwelewi kama hujui lugha anayotumia jukwaani

Hebu eleza upeo wako kama ushauri, sio maneno tu kana kwamba una chuki na mtu fulani.

Au eleza kitengo cha fani yako ili tukukosoe bila kukushauri
 
Mimi kwenye standup comedy namkubali Deogratius.
Yule nakubali anavyojua kuunga matukio halafu yaka make sense. Standup comedy lazima ujue lugha inayozungumzwa ndo utaelewa. Hata akina Kelvin Hart au Basket Mouth kama hujui lugha huwezi kucheka kwakuwa hutoelewa.
Mimi naenjoy zaidi standup comedy.
Chris Rock
 
Kwa hakika siwezi kupoteza muda wangu au data kumtazama mchekeshaji wa Kibongo. Hawa wachekeshaji wetu mimi ninawaita waropokaji.

Comedy ya wenzetu wengi utacheka na kufurahi hata usipoielewa lugha wanayoitumia jukwaani.

1. Comedy ya Kibongo imekosa ubunifu.

2. Wanadhani mpaka leo mavazi yanaweza kumchekesha mtu.

3. Komedi ya Bongo ni kwa Watanzania tu kwani inabeba mazingira ya Kibongo tu.

4. Imejaa kelele(uropokaji) tu haijulikani inahusu nini.

Hebu cheki hii clip chini ujionee comedy ya wenzetu.
View attachment 2040040

Mpe heshima yake king majito
 
Lakini Joti anajitahidi sana ukweli usemwe,
Hao wengine sijaona ila kwa Joti angalau anaweza kukufanya ucheke, napenda anavyoweza kubadilika badilika kuanzia Mtoto, kijana mtukutu, kijana wa makamo, dada wa mjini hadi mzee kikongwe,

I love that.
Joti anakosa team nzuri tu ya kufanya nayo kazi ila joti ni legend wa level za kimataifa. Kuweza kuwa na character zaidi ya tano si kazi ndogo.

1.Mzee mwalubadu
2. Hami J
3. Asha ngedere
4. Yule character anaigiza kama dalali mara nyingi
5. Character akiigiza kama mtoto


Hii kitu ni wachache sana huweza.
 
Starter pack ya comedian wa kibongo;

Kuvaa nguo za kike.
Kubadilisha sauti, kuongelea puani.
Kuifanya hamnazo.
Kuropoka ovyo.

Wakishapata umaarufu kidogo kama Mpoki ni kuanza kutukana watu kwa kisingizio cha kuchekesha.

Waliopata exposure kidogo, kama Idris Sultan wao hujichekesha wenyewe kwa kuongea upumbavu usiochekesha.

In short ma comedian wa kibongo wana mwendo mrefu mno mpaka kujua maana halisi ya comedy.
And its a load of crap.

Halafu wote wanaigana and end up being even more disgusting.
 
Kwa hiyo wana jf..... Baada ya juz masanja kuongea pumba ndo akawa siyo Comedian mzur???

Yaan miaka yote hiyo kwenye game masanja hajawah kuwachekesha????wanafik nyinyi

Kama mtu amekosea mkosoe maisha yaendelee ila nitakuwa wa mwisho kuamin et Masanja siyo mchekeshaj mzur
 
Imenilazimu kuangalia clip ya masanja aisee ameongea mashudu tupu pale taifa na yale mamiatu Kama yakike
 
Ma commedian wabongo wanasikitisha kweli wengine wanaume mpaka wavae vijora wapake na wanja ndio wanachekesha
 
Huwa nawaekewa sana comedians kutoka Kenya ndo wananmaliziaga mb zangu kule mjini yutubu
 
Back
Top Bottom