TANZANIA imetajwa kuoongoza kwa urasimu na ukiritimba kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hususan nyanja za usafirishaji na huduma, ripoti imeeleza.
Kaw mujibu wa ripoti hiyo iliyozinduliwa juzi, dereva wa lori anasimamishwa mara mbili ya askari wa usalama barabarani, mara tatu kwenye vituo vya kupimia uzito wa magari na mara nne Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Ripoti hiyo iliyozinduliwa na Katibu wa EAC, Richard Sezibera, inaeleza kuwa baada ya Tanzania zimefuata nchi za Kenya, Uganda na Burundi.
Inafafanua kwamba ukiritimbawa utendaji katika bandari, vizuizi vya barabarani visivyo vya lazima na masuala ya utawala, ni miongoni mwa vikwanzo katika uendeshaji biashara kwa ufanisi kwa kanda ya EAC.
Vituo vingi vya kupima uzito wa magari katika kanda za Kaskazini na Kati, taarifa hiyo imeeleza, hufanya biashara zisifike kwenye maeneo husika kwa wakati.
Baadhi ya maeneo yanayoathiriwa na hali hiyo ni Burundi, Rwanda na Uganda zikiwa na vituo 36 kati ya Mombasa na Kigali, vituo 30 kati ya Dar es Salaam na mpaka wa Rusumu nchini Rwanda. Uganda nayo ina vituo tisa kati ya Malaba na Gatuna.
Nchi za Rwanda na Burundi ndizo zinazotambulika EAC kwamba zinafanya kila linaloweza kuondoa vizuizini vyote vya barabarani kuliko nchi nyingine wananchama za Kenya, Uganda na Tanzania.
Ripoti hiyo inaeleza kwamba taratibu ndefu za kupata kibali cha kufanyakazi miongoni mwa nchi wanachama wa EAC, hususan Tanzania pia ni changamoto.
Mambo mengine yaliyoripotiwa ni ukosefu wa maeneo ya kuegesha magari mpakani, rushwa kwa kanda za Kaskazini na Kati na pia kuzuiwa kwa magari kusafiri zaidi ya saa 12:00 jioni nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda wa Rwanda, Emmanuel Hategeka, alisema hivi karibuni mjini Kigali kwamba yapo majadiliano yanaendelea kuhakikisha vikwazo vyote vya biashara vinaondolewa.
Tanzania imekubali kuondoa ushuru wa dola 200 za Marekani zinazotozwa kwa malori toka Kenya na pia kuondoa malipo ya viza kwa wafanyabiashara kutoka Kenya.
E-mail:
meezy@youngmaster.co.tz