BUBE,
Naona umechukua muda kutoa mchango wako ambao unanifanya kuona una upeo katika maswala ya integrity. Kwanza! Tatizo la ardhi hata sisi tunalo hapa nchini. Utakuta mtu ana tuma mawakili wake kortini na unayezozana naye humuoni na hutawahi muona kamwe. Taking pride in ones country ni sawa tu na uzalendo na hakuna kibaya nacho lakini kuna ule ambao unatetea ujinga unaotekelezwa nchini. Kama kwa mfano kuna hoteliers, security guards, and mining workers wanaoletwa kutoka nje kufanya kazi tanzania si vyema. Je! Workers union na local pressure groups/ rights activists wa tanzania hawaingilii kati kutetea workforce iliyo na vyeti vya masomo?
Kumbuka ninaposema tucommend china, mimi sio perfectionist. Umaskini ni kitu cha kawaida na sidhani ni kitu cha kuondolewa kwa muongo mmoja. China na wale Asian tigers bado hawako kwa hali ya kuripoti kwamba wameumaliza umaskini. Vile vile kuhusu ICC, kile kinaleta mgawanyiko ni mfumo wa siasa ambao ni kind of a
hangover from the former regime ndio walikuwa wanaeneza ukabila na siasa za uridhi na proteges/projects. Wakati huu tunataka siasa kama hii ikomeshwe kupitia civic education na kusisitiza kuundwa kwa
leadership and intergrity bill katika katiba. Ndio unaona wakati huu ambao katiba inatekelezwa, wanasiasa wanakaa ni kama wamepigwa na mhstuko wa moyo.
Tuna njia ndefu ya kuenda, kwanza kuhusu matatu na ulevi wa mchana. Lakini BUBE ni jamii gani utaenda ukose mambo haya? Inawezekana kuyapunguza lakini sidhani uovu wote unaweza koma, . Mauaji haya ya watu wa IDP .nk ni jambo limeletwa na tensions na historical injustices. Mimi nina tatizo tu moja na ICC, hawana jurisdiction ya kuwanasa na kuwafungulia mashtaka wahalifu wa kimbari. Nikupe mifano kama uhalifu wa bosnia ambako waislamu wengi waliuwawa, Rais Al bashir wa Sudan kaskazini na vitendo anafanya na makundi yake ya kigaidi mpaka sasa, Bashar al asad wa kule Syria tutaje tu wachache na hatujaribu kutetea mauaji. Kuna mengi ICC hawajagusia na hawajazungumzia sana sana ukizingatia mifano nimekupatia. Mimi naamini tangu uhuru wa nchi ni wengi waafrika waliouliwa na wabeberu, na wengine kutimuliwa kutoka makwao. Na wale wamejaribu kutaka haki zao kutoka kwa serikali za uingereza zitimizwe bado hawajapata.
Tuangalie scenario kama ya jews and the holocaust, Serikali ya ujerumani kufikia sasa miongo tatu iliyopita imekuwa ikigharamia fidia za holocaust. Alipofariki karl Eichmann ni mwaka gani? Lakini ukifananisha na African colonial injustices ni hadithi tofauti. Nimalizie na kusema, a rent seeker, or a donor both have common interests. Do not expect them to bring anything new other than kuleta capital flights. Kwa muda mrefu imekuwa ni kama
andiko kuwa Afrika ina matatizo mengi na haiwezi jikwamua kutoka kwa shida kama magonjwa njaa, na baadhi ya mengine kama hayo. Ninajua kuna wakati joto za siasa zitapungua Kenya, lakini kwa sasa wacha tuombee taifa hili letu. Najua Tz mwatuchukua in good light isipokuwa
wakereketwa wachache ambao ni asilimia ndogo ukifananisha na wale watanzania ambao ni forward thinking, positive, and optimistic about themselves and their future.
Mzalendo.
Moyo sio Mkenya kwa taarifa nilizonazo! Actually Dambisa Moyo alizaliwa na kukulia Zambia. Sio Mkenya...sina hakika kama wakenya wanaweza kusema hivyo...japo kuna utani kuwa jirani zetu hao hupenda kudhanikuwa kila kitu kizuri kinatoka Kenya...so proud of their country...which is gud!
Otherwise, uko sahihi kuhusu PC. Hapa Tanzania ipo pia njia ya ku-assess wafanyakazi kwenye ofisi za umma (civil servants) but the problem is enforcement so that people are promoted/demoted based on merits not on feeelings za mtu mmoja mmoja. There are also issues to do with stereotyping! Hili ni tatizo. Watu wengi na hata wale wanajiita researchers, wakati mwingine waki-sample vibaya study unit yao huangukia kwenye research results ambazo zina-stereotype kuhusu kabila na taifa. I do not agree with Moyo's findings not because I am a Tanzanian but because I know that has been major issue among watu wa nje kuhusu Tanzania. what does that mean to our economy? Ina maana mining companies, tourists companies and hoteliers wanaleta wapishi wakuu, wasaidizi, walinzi na hata madrivers kutoka nchini kwao. Tatizo sio reliability shida ni kwamba hata pale wanapofanya makosa process ya litigation hadi mtu apate haki yake ni miaka. Mfano kuna kesi za ardhi zinakwama kwa miaka hadi 25! Nani atakuwa anahangaika mahakamani muda wote huo unaanza kesi ukiwa kijana unamaliza mzee hata ukishinda you will not have energy to work on the land
Hapa ndo kinacholeta shida! Hii tuiache kwanza
While we commend China for the achievement, tunasahau kuwa mambo makubwa manne ndo yamechangia China kunyanyuka (pamoja na kwamba ndani ya China umasikini unazidi) na kujitangaza nje. Mambo hayo ni pamoja na kujua what they want (get their priorities right), kuwekeza walipo masikini zaidi, kuboresha miundo mbinu na kisha kuwa na focus. Not changing policies and strategies after every 3years! Huu ni uhuni. Sasa kwa kuwa kila mmoja anaimba wimbo ule ule (politicians, technocrats and moderate people) ina maana hata law enforcers find it easy to execute/implement! Mimi nadhani Kenya haiwezi kuwa mfano mzuri....it might be too early to do that! Kwa kipindi ambacho nimewahi kufanya kazi Kenya (mwaka mmoja) na hata leo hufika Kenya kila baada ya miezi 2, nina mashaka kuwa hata wao wanaweza kujidai nje ya karatasi. Mifano miwili ambayo nadhani wamefanikiwa na mmoja sijaona kama watafanikiwa. Unapoongelea muida wa kufungua bar na kufunga na mtu kuonekana amelewa nyakati za kazi (nguvukazi) hii kwa sehemu wamefanikiwa,but should this be the respinsibilit of each one of us/Kenyans. Kutoa taarifa kuhus bar zilizowazi wakati wa kazi? Hapa nadhani ipo safari. Pili ni kuhusu upandaji wa matatu! Kwa mstari mtu wangu -first in first serve. It works but si kwa matatu zinazokatisha njia! But you see, nimejariwa kwenda nchi za wengine ambazo kila raia anaona ni wajibu na LAZIMA alipe kodi---they are proud about that, na pia ukikutwa unampiga/mnyanyasa mkeo simu inapigwa polisi na jirani na polisi wanakuja muda ule ule kutoa msaada! what about us?
Sasa hilo linanileta kwenye mfano mwingine ambao sioni kama Kenya inafanikiwa. Unajua baada ya uchaguzi na mauaji yaliyofuata ya watu zaidi ya 1400, nilidhani wakenya wengi wangechukia kitendo kile kwa kuwa kinaleta picha mbaya kinakiuka haki za binadamu. Recently nikasikia mjadala kwenye bbc nilikuwa shocked kusikia vijana wengi Kenya na hata wanasiasa wakubwa wanachukulia suala la ICC na wale washtakiwa kuwa ni la kisiasa zaidi kuliko vile limebebwa.
Mimi nadhani viongozi ndo wametuangusha na sisi kwa kutokuwa macho na wasimamizi wa rasilimali zetu tumechangia uozo huu. Do not understimate the effect of rent seekers pale wanapojidai wanawekeza kwenye madini, but take everything, wanapodai wamenunua parastatals ambazo zimekuwa privatised and end up vitually killing them! Kwa Tanzania nijuavyo hao rent seekers pamoja na viongozi wabofu wamechangia kuleta umasikini kuliko unavyoweza kufikiria. Swali hapa ni je, the so called donors are they not aware about this? Pengine wanajua but what are they doing about it? May be they are letting everything inthe hands of wananchi...very unfortunately that the wananchi are not well informed. Hata wale wawakilishi wao (wabunge) nao hawana taarifa za kina!