@Kibona
Shukrani kwa kujitokeza lakini umewasili na hisia kali raund hii! Nakubali Wakenya wanafaa elimu ya kujua kuishi vyema na wengine. Lakini wacha niseme hivi, wanaodai kufunzwa ni wale wapumbavu/(ignorant bila masomo). Utakatu ni asilimia chache tu ya waKE wanafanya biashara au wenye mali hawana elimu. Lakini wale walio na elimu ni asilimia kubwa. Kimsimgi ugumu tunaoona zimechangiwa sana na yaliotokea katika historia sana sana punde tu Afrika mashariki na nchi zake zilipopata Uhuru wa kujitawala.
Elimu inafaa ipewe wakenya na hata Watz kwa sababu tayari tumeshuhudia kizazi kikipita, na hivi watz wa sasa pia wanahitaji hayo mafunzo ya kuwa na staha na baadhi ya wengine. Mara nyingi huwa nasema na ninarudia, hamutasafiri maili nyingi kutafuta soka ya bidhaa zenu, na nchi za East Africa ndio tegemeo la kwanza mutafikiria kuuza na kununua bidhaa. Unaposema munajifahamu nyie watanzania kwamba muna rushwa na uongozi mbovu, si ni nyie munaowapigia kura hawa viongozi. Tayari unakiri pamoja na uhuru munao, hamuwezi jinusuru kutokana na kuwaingiza viongozi wafisadi na kulingana na post yako una matumaini kwamba munajielewa na mutaipiku kenya kiuchumi.
Kuna ripoti za utenda kazi mbaya katika bandari zenu na kawaida pia KE kuna hizi ripoti. Wakati huu sio wakati wakukaza shingo, bali ni wakati wa kila mmoja aangalie njia za kupunguza rushwa, na vizingiti, na siasa mbaya kwake. Usishangae Rwanda hapa jirani Uganda na Burundi wakipiga hatua katika EAC. Kwa sasa kuna ripoti hata baada ya kuondolewa kwa vizingiti baada ya mkutano wa waakilishi wa EAC, bado serikali inazuia watu na malori yao kuwatoleza dola 200, la sivyo paspoti zinachukuliwa na maafisa wa polisi kwa madai ya kuwa nchini humo bila paspoti. A very bad system ya "ugavi wa mamlaka" ambao hauheshimu baadhi ya viongozi na mwito wao.
Mradi tu tungeendeleza kile Mkapa na M7 walianzisha mwaka 2001, tungekuwa tunafungua kurasa mpya katika kuboreshwa kwa sekta za uuzaji, ununuzi, na usafirishaji wa bidhaa ndani ya Jumuiya. Lakini ndio vituko tunavyo hapa Afrika siasa za ubinafsi zinazuia maendeleo bila kujua kilicho na mwanzo hakikiosi kuwa na mwisho.
Mzalendo452,
Hii ndiyo aina ya debate nilitarijia baina ya wadau wa nchi hizi mbili. Kwanza kujadili kwa kuheshimiana na pili kutambua historical nature ya mambo yaliyo mezani. Jambo moja ambalo mimi ninatofautiana na wewe ni pale unaposema kuwa wanohitaji elimu ya kutambua kuishi vizuri na jirani ni watu wapumbavu - watu ambao hawajapata 'formal education'. Kwa hakika huhitaji kupata PhD ya chemistry au electonics ili kujua namna ya kuishi na jirani.
Kwa mfano, week iliyopita hapa London, Saatchi na mke wake Nigella Lawson wameuza flat yao waliyokuwa wanaishi hapo zamani. Na sababu kubwa iliyowafanya wakahama toka kwenye hiyo flat ni mzozo na jirani zao. Saatchi sio mpumbavu, yeye na kaka yake ndio walianzisha Saatchi & Saatchi, pia mke wake (Nigella) sio mpumbavu, ameenda shule, na ni mtoto wa former chancellor of Exchequer Lord Lawson. Hivyo mgogoro kati ya majirani unaweza kutokea regardless watu hao wamesoma au la.
Tukirukudi hapa kwetu, nakubaliana kabisa na Kibona kwamba friction kati ya Kenya na Tanzania ni historical. Na hata leo hii ukifanya survey Kenya, statistically, watu wengi watasema watanzania ni 'wapumbavu' na nchi ni backward. Vivyo hivyo ukifanya survey Tanzania, statistically, watu wengi watakuambia wakenya ni manyang'au, wabinafsi na walafi wa pesa. Hizi ni feelings kati wa nchi hizi mbili, na zimedumu kwa muda mrefu. Na katika mazingira haya ni mwendawazimu tu ndiyo anaamini kuwa unaweza ku-fast track muungano (hata wa kuchota maji ya kunywesha mbuzi)!
Tanzania na Kenya ni nchi mbili tofauti kabisa na zimejengwa kwenye misingi tofauti. Tangu uhuru Kenya ime-emabrace capitalism, huku Tanzania wakiegemea african socialism. Hii ndiyo misingi inayofuma (suka) 'fabric' ya society kwa nchi hizi mbili. And unless kunakuwepo na juhudi za maksudi ili watu wa nchi hizi mbili wafahamiane EAC itakuwa zigzag. Tayari tuna skeleton in our cupboard, East Africa Community ya miaka ya 1970 ilikufa kwa sababu hizi hizi ambazo zinatuzonga sasa. Na watanzania dakika hii wangeulizwa wanataka nini EAC, I am almost certain wengi watasema tugawane mbao (kama zipo) kila mtu aende zake. People hate EAC with a passion. Na wanaposikia kelele mara za ardhi, free movement of labour, trade etc ndio wanazidi kupatwa na nyongo. tuachie hapo.
Hapo kwenye blue: Dawa ya kupambana na rushwa, ufisadi etc si kubalisha mtu mmoja mmoja tu. You need to do more than that. Ni lazime kuwepo na institutional framework strong enough ili kukabiliana na viongozi wabovu. Ndio maana tunaandaa katiba mpya. Na harakati za kudai katiba mpya zimedumu kwa miaka aprox 20 sasa (tangu 1992), better late than never. Hivyo tunajua tatizo la msingi ni lipi na kama jamii we are now doing something about it. Ninaamini tatizo la rushwa na ufisadi haliko tu Tanzania, Kenya nako kuna a catalogue iliyosheni kama x'mas tree. Na huko nyuma ilikuwa ni shida kupambana na ufisadi kwa sababu 'institutional framework' ililalia upande wa wakubwa, lakini baada ya kupata katiba mpya tunaona ile nguvu ya watawala kufunika mambo inapungua na wananchi wanakuwa na sauti stahiki kwenye ulingo wa utwala.
Ninachotaka kusema hapa, kama nchi, Tanzania tuna matatizo yetu and we are addressing them in our own way. Mahusiano mazuri kati nchi jirani kwenye nyanja mbalimbali i.e biashara, siasa ni jambo la kheri lakini kwa sasa EAC sio priority kwa watanzania wengi, EAC si mama wala baba wa watanzania. La msingi ni kusafisha nyumba na kuhakikisha msingi uko imara, and kama umesoma kwenye sub-forums hapa jamvini utaona kelele nyingi kati ya CHADEMA na CCM. EAC ni nyongeza.
Hivyo basi, kama nchi nyingine zinakwazwa na Tanzania kwa namna yoyote ile, basi ni vema wakajipanga upya na kuendelea bila Tanzania. But for nown, we are very busy sorting out our fundementals. Kelele hazitasaidia kitu zaidi ya kutibua nyongo za watu.