Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly.
Mkuu wangu,Hawa-appreciate the fact kwamba serikali, kwa kuona uwezo wake mdogo wa kugharamia elimu, imeamua kuwaangalia waanafunzi wasio na uwezo kupitia sera hiyo, ili wale wenye uwezo watoe nafasi kwa wasio na uwezo kulipiwa na serikali. Huu ni ubaguzi wa aina gani? Je, kutaka matajiri na masikini wote walipiwe 100% huko si kuwanyanyasa wasio na uwezo?
Kwa tathmini yangu ni kwamba hawa vijana wanatumiwa na watu fulani, ambao wameweza kuwamanipulate kutokana na kutokukomaa kwa wanafunzi hawa kifikra. Ndio maana migomo ya UD siku zote ni ya undergraduate students. Ingekuwa ni migomo genuine mature postgraduate students nao wangekuwa wanagoma.
Mkuu usilinganishe Kenya na Tz...!2. Ni jukumu la jamii kuwa na mikakati kuwasomesha watu wake..mbona pesa ya arusi tunaweza kuchanga mamilioni?
Yes, serikali uwezo wake mdogo sana.
Mashangingi ya bei mbaya 700 kwa mwaka mmoja. Kukodisha ndege mbovu za ATCL, zilizopelekwa Kiwira kimya kimya, za safari, za vikao, washa, seminar, kongamano................ Kweli serikali uwezo wake mdogo, AMEN!!
... hili la kwamba mbona postgraduate hawagomi inanidhihirishia hufahamu tofauti ya UG's na PG' pale mlimani.
Who feels it knows it!!!!!!
Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly
Naamini panapofuka moshi pana moto...tatizo la msingi lipo kwenye namna mikopo inavyotolewa elimu ya juu. Serikali ina sera za kutoa mikopo, lakini implementaion inaleta matatizo kwasababu so far imekuwa ngumu kujua nani ni maskini wa kweli mwenye kuhitaji 100% na nanani siye. Cha msingi ni kuazima busara na kutafuta njia muafaka ya kulitatua. Kitu kibaya sana badala ya wahusika kuendesha suala zima kama ni ishu of national interest linageuzwa ni suala la kisiasa zaidi. Kauli za machibya siyo sahihi...ila condemning the claim about problems related to how loans are being given for higher learning students is also not realistic.
We should all seek to understand before being understood. Otherwise migomo itakuwa inaendelea kila kukicha kwasababu ya ku handle everything with arrogance
Tafadhali nifafanulie hiyo tofauti iliyopo kati ya UGs na PGs wa UDSM.
Our understanding huku kijijini
Hatukatai hii sera ila wakati wake bado, watu hawajawa tayari. Nchi hii haina kuaminiana hata chembe. Haiwezekani utumie computer kuangalia nani apewe asilimia gani. Watu wamedanganya i have a evidence on this na sitanii. Hiki ndicho kinachonifanya nione kuwa hapa pana kamchezo. DARUSO hapa ndo mahala pa ku komaa napo mana hawa hawa mafisadi ukishafika chuo kwa private sponsor wanakusaidiia kupata mkopo.
Maandalizi ya hapa lazima tuanze kupanga uzazi kuliko kuamini kuwa kila mtoto atakuja na riziki yake mwisho ni WIZI MTUPU. Nyumbani mpaka ughaibuni.
Jiweke kwenye position ya mtanzania mwanafunzi wa UDSM asiyeweza kutimiza masharti hayo ya readmission kabla ya kulaumu hizo lugha 'zisizo na busara' aliyotumia.
Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine
UGs = Undergraduate students na PGs = Post graduate students nadhani niko sahihi...