Huwa napata shida sana na wana JF humu ndani ukizungumza udhaifu wa CDM utashambuliw alkini ukiweka post ya mazuri kila mtu atakusifu safi kamanda hakika wewe ni mapambanaji, ktk siasa za sasa ni lazima wana CDM wakubali kuw Zitto, ni tishio ndani ya CDM na nje ya CDM, na hata Picha yake kutumiw aktk ukurasa wa mbele kwenye Gazeti la Tanzania Daima tunajua klichojificha nyuma yake.
Ni nani asijua Zitto, alipokwenda katika sherehe za kutangazwa uhuru wa Sudani Kusini, Gazeti hili hili lilitoka na picha kubwa ya Zitto na JK sambamba na habari kubwa iliyosema 'JK ambeba Zitto', amuandaa kugombe urais hali ya kuwa siku zote Zitto anajijenga mwenyewe kutokana na hoja zake mahili kwa Taifa letu.
Hakika huu ni mkakati wa baadi ya viongozi wa CDM katika kufifisha nyota yake lakini daima haiwezekani kwa Tanzania ya sasa.