Tanzania Daima lamshambulia Zitto?

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
leo uk wa mbele kuna Picha ya Mh Jk akifurahi na Zitto.
Katika picha hiyo tzdaima lajidai "Marafiki wa kufa na kufaana"

Kwanini tzdaima haichapishi picha ya Mh mbowe na JK wakicheka pamoja?
Jee kwa zitto kuchapisha na kuandika maneno hayo , Viongozi wa CDM hawatazidi kumuona ZItto ni msaliti?
 
kuna kipindi alisema anaenda kulalamika gazet hilo kwa mmiliki. alienda?
 
Mi nafikiri siasa sio uadui. Tulimwona Nassar akiwa na W. J. Malecela, tulimwona mganga Maji marefu akiwa na viongozi wa cdm. Sidhani kama cdm wanataka kuona Zitto akipigana na jk! Hatujafika huko!
 
Mkuu ni picha tu na maneno hayo hakuna content zaidi?
 
leo uk wa mbele kuna Picha ya Mh Jk akifurahi na Zitto.
Katika picha hiyo tzdaima lajidai "Marafiki wa kufa na kufaana"

Kwanini tzdaima haichapishi picha ya Mh mbowe na JK wakicheka pamoja?
Jee kwa zitto kuchapisha na kuandika maneno hayo , Viongozi wa CDM hawatazidi kumuona ZItto ni msaliti?

Mkuu hoja yako nadhani haina mashiko kwani kucheka na mtu ndo kwamba unakubaliana nae ktk matendo yake 100%?
 
kuna kipindi alisema anaenda kulalamika gazet hilo kwa mmiliki. alienda?
Alisema anamshitaki mmiliki wa gazeti (Mbowe) kwa katibu mkuu wa chama (Dr Slaa). Sijui walimalizana vipi. Kama sijasahau, ni wakati wa sakata la Kafulila kutaka kumpindua Mbatia na mbunge mmoja wa NCCR kunukuliwa na gazeti hilo akisema alishawishiwa kuunga mkono mapinduzi hayo na kuhakikishiwa kuwa Zitto alikuwa na fungu la kutosha kufadhili mpango huo.
 
Mi nafikiri siasa sio uadui. Tulimwona Nassar akiwa na W. J. Malecela, tulimwona mganga Maji marefu akiwa na viongozi wa cdm. Sidhani kama cdm wanataka kuona Zitto akipigana na jk! Hatujafika huko!

Kweli mkuu siasa siyo vita
 
haina aja ya picha mwanzisha mada anataka kuchochea na kuweka vitu visivyokuwepo na visivyo na maana kwa kuitafsiri atakavyo hii picha!

maandishi yanasomeka. "marafiki wa kweli wa kufa na kufaana" jee jk na zitto ni marafiki kiasi hicho? Au tzdaima wanatka wananchi wafahamu kwamba zitto ni kibaraka?
 
leo uk wa mbele kuna Picha ya Mh Jk akifurahi na Zitto.
Katika picha hiyo tzdaima lajidai "Marafiki wa kufa na kufaana"

Kwanini tzdaima haichapishi picha ya Mh mbowe na JK wakicheka pamoja?
Jee kwa zitto kuchapisha na kuandika maneno hayo , Viongozi wa CDM hawatazidi kumuona ZItto ni msaliti?
Kwenye siasa za Chuki wataona hivyo, Kwa wanaojua siasa, hizo ndizo siasa za kistaarabu.
 
maandishi yanasomeka. "marafiki wa kweli wa kufa na kufaana" jee jk na zitto ni marafiki kiasi hicho? Au tzdaima wanatka wananchi wafahamu kwamba zitto ni kibaraka?

Tanzania daima hawana tofauti na baadhi ya mitandao ya kijamii inayoamini kuwa rafiki wa Chadema ni yule anayekisifia chama hicho na kukashfu Serikali. Huo ni ufinyu wa mawazo. Zitto bwana amekomaa kisiasa mwacheni tu.
 
Binafsi sioni tatizo la picha wala caption yake. Haya ni mambo ya uandishi wa habari. tatizo ni fikra tofauti miongoni mwa jamii yetu. Wengine wanaona kama Zitto atamfunika Mbowe kitu ambcho sio kweli kwa sababu kila mtu ana persnality yake na role yake ya kuplay kwenye Chama, Bunge na jamii kwa ujumla. Tuwaombee wote wenye nia njema na taifa hili walete umoja na kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi wa kipato cha chini.
Haina aja ya picha mwanzisha mada anataka kuchochea na kuweka vitu visivyokuwepo na visivyo na maana kwa kuitafsiri atakavyo hii picha!
 
Hapa vipi napo????

Zitto ni kijana "wetu"

269398_218120438224649_116393691730658_547970_3290987_n.jpg
 
leo uk wa mbele kuna Picha ya Mh Jk akifurahi na Zitto.
Katika picha hiyo tzdaima lajidai "Marafiki wa kufa na kufaana"

Kwanini tzdaima haichapishi picha ya Mh mbowe na JK wakicheka pamoja?
Jee kwa zitto kuchapisha na kuandika maneno hayo , Viongozi wa CDM hawatazidi kumuona ZItto ni msaliti?
Hueleweki mkuu. Kinachofanya aonekane msaliti ni kuchapishwa kwa picha hiyo au ni yeye kucheka na MH Rais? Maana picha au gazeti linareport event tu!

Lakini kubwa ni kwa nini unaamini si sawa kwa Zitto kuongea na kucheka na Rais. Tuliona karibu viongozi wote wa CDM walipoenda pale magogoni na kupewa chai wote walionesha tabasabu/kufurahi tu. Sasa hili la Zitto ni kwa nini lionekane kuwa ni tatizo? Na kwa gazeti kuchapisha picha hiyo ni kwa nini unaona vibaya...mimi naona kama vile inamjenga Zitto kisiasa kwa sababu inaonesha anavyokubalika hata na wapinzani wake (CCM).

Kama utakumbuka hili la kukubalika na wapinzani liliwapa taabu sana washabiki wa JK pale ilipokuwa inaonekana kama vile Dr Slaa hamkubali, anamkwepa etc. Ilivyotokea mwanya wa Dr Slaa na JK kukutana sote tunajua picha hizo zilivyopewa umuhimu hata na magazeti ya CCM au Pro CCM. Well hili la Zitto pengine lipo tofauti kidogo lakini kimsingi sioni tatizo kwa picha hizo kuchapishwa gazeting kama kweli hiyo event ilitokea.

Kama unadhani kuna hoja/agenda nyingine labda utuambie.
 
Hiyo picha haina shida yoyote.Mbona gazeti ninalo na imeandikwa MARAFIKI WA KWELI.Kuna ubaya gani? Mbona sisi huku mtaani CCM na CDM tunaazimana chumvi? Mleta mada analeta uchochezi wa kipumbavu usiyo na maana yoyote.
 
Back
Top Bottom