PICHA SI TATIZO: TATIZO SIASA ZA ZITTO za 'opportunism and facemongerism' - siasa za uuza sura ambazo CDM si mahali pake. CDM ni hoja kwa hoja, hoja kwa hoja ...
SIASA za 'gizani' ambazo zimefanywa na wanamtandao tangu miaka ya 1970 ndizo zimeifikisha nchi hii hapa ilipo: PABAYA, MBELE HAIENDI NYUMA HAIRUDI. MTANDAO ulianzisha siasa za gizani kwa sababu moja kuu, nayo ni kwamba NDANI YA CCM kwa kufuata utaratibu wa chama mafisadi hawa hawakuwa na nafasi ya kupata uongozi wa juu. WAO WANAMTANDAO wakaliona hilo, wakabuni mbinu (1) siasa za pesa tena chafu, na (2)
publicity, vyombo vya habari kuwatangaza kwamba wao ndio wakombozi,
messiah, wetu. KUMBE PUUUUUUUUUUU. WATANZANIA walipokuja kuwagundua mambo yakawa yameisha, wako IKULU.
SASA KWA BAHATI NZURI AU MBAYA MH. ZITTO nae anakabiliwa na mazingira yaleyale yaliyokuwa yakiwakabili WANAMTANDAO, nae ameamua kutumia mbinu zilezile zilizotumiwa na WANAMTANDAO, na yeye ZITTO ameongeza mbinu nyingine CHAFU ZAIDI (kwani ni bidhaa inayogombaniwa na wajinga wengi) ya kwamba ANAONEWA ndani ya CDM, na silaha yake ni eti kwa kuwa ni 'muislamu' na ni 'maarufu'. Gazeti LISIPOMTANGAZA anavyotaka yeye KWAKE LIMETANGAZA vita. KWA TARATIBU ndani ya CDM ZITTO 'si mzito' kama yeye anavyofikiri, siyo kwamba anabaniwa ila kuna 'VICHWA' zaidi yake. KWA MFANO alipokuwa MBUNGE 2005 - 2010 ALIKUWA maarufu kama
pop star MICHAEL JACKSON, na sababu ni kwamba, alikuwa peke yake kijana (akisaidiwa na vijana wengine kwa kweli kama MDEE) upande wa CDM na alikuwa na hiyo
platform BUNGE. SASA vijana ni wengi BUNGENI na wengi wao kwa uwezo wako mbali sana, wanamzidi. KUPAMBANA NA HILO ZITTO ameanzisha siasa mpya tofauti na alizozifanya 2005 - 2010, kwamba anachukua MSIMAMO wake binafsi tofauti na ule wa chama CDM. KWA MFANO CDM inakuwa na hoja na wabunge wao wanajipanga kwa pamoja kwamba, nani kati yao je, ni MH. MNYIKA au TUNDU au MDEE au MSIKA au ZITTO nk atayesimama kupambana na CCM na SERIKALI YAO. Sasa hapa ndipo tatizo kwa ZITTO anapochaguliwa MH mwingine, yeye atasimama na msimamo wake, na hapa sasa ndipo matatizo yanapoanzia KWA CDM kwani lazima MBUNGE wa namna hiyo ashughulikiwe (lakini kwa silaha ya ZITTO ya uislamu CDM wanajikuta mikono yao imefungwa kwa kiasi fulani).
MIMI napenda kushauri (1) KUWA WANANCHI WATAMBUE KUWA watu wa namna hii wapo wengi kwenye siasa (angalia siasa za KENYA); (2) CDM iongeze juhudi za kutambua 'true characters' za watu wao na 'watu WALIO NYUMA YAO'; (3) hizo characters zioneshwe wazi kwa wananchi ili watu hao WATAKAPOCHUKULIWA HATUA madhara kwa chama yawe madogo; na (4) lazima chama kiendelee kuwalea na kuwaonya vijana kama akina ZITTO kwani wanaamini kuwa wao ni maarufu sana, kitu ambacho siyo kweli, ili waweze KUZINGATIA MSIMAMO wa CHAMA: kama kila mtu atafanya kile anachoona yeye kinafaa, basi chama hakitakuwepo. CHAMA ni msimamo wa pamoja, kama imeamuliwa na CHAMA kwa vikao halali ambamo mhusika alishiriki na kujenga hoja zake ambazo hazikuungwa mkono, basi hana namna bali ni kuunga mkono msimamo wa CHAMA la siyo njia nyeupeeeeeeeeeeeeeeee.
No, kuna kitu hapa hakipo sawa. Si zambi kukutana na na Rais lakini kuna mipaka yake. Hasa ukiwa ni mwanasiasa. David na Ed (both Milband and Balls ) huwa wanakutana kila mara ila sijawahi ona wamepiga picha pamoja (labda washamba na sio wastaarabu). Kuna mpipaka yake kwenye siasa.
Picha ya Zitto na kikwete ina ujumbe ufuatao nao ni kwamba Zitto anamkubari sana Raisi ila watendaji wake ndiyo anaona wana matatizo. Swali kama unaona hivyo na wewe unaipenda nchi kwa nini usiende kumumsaidia?
Najua CDM wanajua kuwa tatizo la nchi hii chanzo ni kikwete na zitto anasema hapana kwa mawazo, maneno na matendo.
Zitto kwa ufupi tu akaokoe jahazi la Raisi ampendaye!