Tanzania Daima: Kama CHADEMA ni Wachagga, CCM ya Waislamu?

Ndugu zangu, nenda kushoto nenda kulia, ukweli unabaki ni ukweli. Miongoni mwa vyama vya siasa hapa nchini vina udini, ukanda na ukabila. Vyama vya aina hii watanzania tuvikatae kwa nguvu ya Umma maana vitatugawa na kutuletea matatizo makubwa.
 
Hakika umenikuna mwanakijiji. Naomba chadema wafanye yafuatayo;
1. Kumstaki nape na ccm mahakamani ili wathibishe kuwa chadema ni chama cha wachaga.
2. Naomba chadema wakomalie hiki kipengele cha uzushi ili kiingie kwenye katiba mpya
Again, Uishi milele mkuuu.
Naomba CHADEMA kwanza kuomba maelezo na msimamo wa chama CCM kuhusu kauli hiyo ya Nape na viongonzi wengine wa CCM kuhusu tamko hilo la uchagga,ukabila udini au kijinsia n.k.Baada ya hapo ichukue hatua za kisheria,Kufungua mashitaka kwa Chama cha CCM au vyama vingine vyovyote na mtu au kikundi chochote kinachotoa matamko hayo bila uthibitisho kwa kufungua mashitaka.Jambo hili likiendelea kuishia kutoa majibu ya majukwaani na malumbano linaendelea kupotosha umma na jamii mzima na jamii itashindwa kuzitofautisha kauli za CCM na CHADEMA kwa ujumla itatupeleka pabaya MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Ah dada/kaka mbopo huyooo!
Sijutii kutolisoma hilo gazeti leo. Hili gazeti sasa hivi ni sehemu ya Habari Corporation. Hivi leo kweli mtu unaweza kuzungumzia Tanzania Daima wakati Raia Mwema iko mtaani? labda kama unataka kusoma mawazo ya mafisadi, ndo utapata Tanzania Daima.
 
Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake. Wahenga bana,walikua na mambo ya ukweli sana. Hivi wahenga bado wapo sku hizi?
Ushauri: Gazeti likizidi sana upeo wa ufahamu wako si jambo la afya sana kulisoma. After all yapo magazeti mengi tuu ya kusoma. HAMIA UWAZI huku tuna hadithi za shigongo kali tuu!
Mkuu kwani ulikuwa ujui? si unawaona wanavyotoa maneno, mimi gazeti likishaanza kusifia mafisadi sitaki ata kuliona
 
M. M. Mwanakijiji​

Matokeo yake tunalazimishwa kuiangalia CHADEMA aidha ni kama chama cha Wakristu au chama cha Wachagga kwa sababu mantiki inayopendekezwa mbele zetu haitupi uchaguzi mwingine wowote. Na tukifuata mlolongo huo huo wa mantiki tunajikuta tunaangalia CCM vile vile kama chama cha Waislamu na ukishaliona hili utaelewa ni kwanini baadhi ya Waislamu ambao walikuwa na tatizo na CCM miaka kadhaa huko nyuma leo hawana tatizo nayo kwa sababu wanaona kuwa kinaongozwa na “Waislamu”. Na matokeo yake utaona kundi la Waislamu hawa hawawezi kuona kosa au tatizo lolote lile la serikali kwani kwa kufanya hivyo itabidi wakubali matatizo ya “Muislamu” mwenzao au “Waislamu wenzao”.

Hapo kwenye red kuna pointi ya msingi. Hili ni swali ambalo labda wakristo wanatakiwa walijibu, Kwa nini wao wamekuwa wakiisapoti na kwenda against na ccm kwa phases?Mfano wakati wa Mkapa Makanisa yote yalikuwa yakiisapoti CCM km ilivyokuwa wakati wa Nyerere hata kufikia kusema Waislam wameanzisha cha cha CUF?
Kwa nini hata mwanzoni Kikwete alipogombea urais Makanisa yalisema yeye ni CHAGUO LA MUNGU mpaka pale alipokataa kutekeleza baadhi ya matakwa ya KANISA akageuka kuwa chaguo la SHETANI? JE, ushawahi kujiuliza ni nani kati ya KANISA na MUNGU alietuongopea kuwa Kikwete alikuwa CHAGUO LA MUNGU? au MUNGU alimchagua kwa wakati fulani tu mpaka pale alipokataa kutekeleza matakwa ya KANISA?
Je, ni kutokana na kufeli kwa JK kutekeleza matakwa ya KANISA, ndio sababu MAKANISA yakakaa kikao cha pamoja kumpendekeza SLAA kugombea urais 2010 km suluhisho katika utekelezaji wa AJENDA ZA KANISA?
Umeelezea kwa umakini na uhodari wa hali ya juu HISTORIA YA NCHI HII TANGU UKOLONI. Nakupongeza sana kwa kuwaelimisha WanaJF waliowengi ambao hawaijui kwa usahihi historia yao kwani imepindishwa Makusudi tu kwa ajili ya kuwaonyesha baadhi ya watu kama ndio mashujaa wa kudai uhuru.
Hivi leo ukimuuliza mtoto pengine na WanaJF walio wengi kuwa ni nani waliodai UHURU atakuambia ni NYERERE.Hawezi kujua role ya akina Sykes wala Waislamu wa pwani, kwani hii haijaandikwa popote.Kutoandikwa huko, sio kwa bahati mbaya bali ni kwa makusudio maalum.
Lkn km ccm ni chama cha Waislam basi ni wema kweli pale waliposaini Memorandum of Understanding na KANISA tena wakiwakilishwa na Lowasa mwaka 1993 ili Serikali ilisaidie KANISA na taasisi zake katika kujiendesha huku wakiacha MISIKITI ijiendeshe kwa VIJICHENCHI vya SADAKA PEKEE.
Ni hawa hawa Waislaam na ccm yao walioifuta MAHAKAMA YA KADHI NCHINI ambayo ilikuwepo tangu enzi za mkoloni pamoja na kuikatalia nchi kujiunga na OIC wakati ikifungua UBALOZI WA VATICANI NCHINI uanaowakilisha KANISA KATOLIKI NCHINI achilia mbali ulea ITALY ambayo Vatican ni sehem ya.
KWELI WAISLAMU HAWA NA CCM YAO NI WATU WEMA SANA HASA WAKATI WA UONGOZI WAKE SHEKH JULIUS NYERERE.
 
mawakili wa chadema, mh. Lisu na marando tafadhali fungueni kesi mapema iwezekanavyo dhidi ya nape na washirika wake. Ni hatari nape wa ccm kuendelea kuligawa taifa kwa msingi ya ukabila na udini kinyume ne katiba ya nchi yetu tuliachiwa na mwalimu. Amani ya nchi ni muhimu kuliko ccm
 
Mzee MM, wengi tunamtazamo kama wako tatizo hatuna uwezo kwa kuandika kwa namna wewe ulivyofafanua - hongera hoja nzuri kazi nzuri na ni ukweli mtupu.

Wanaobishia hoja hii ni wale wanaonufaika na hizi propaganda za udini na ukabila kwa manufaa yao binafsi na chama chao.
 
mawakili wa chadema, mh. Lisu na marando tafadhali fungueni kesi mapema iwezekanavyo dhidi ya nape na washirika wake. Ni hatari nape wa ccm kuendelea kuligawa taifa kwa msingi ya ukabila na udini kinyume ne katiba ya nchi yetu tuliachiwa na mwalimu. Amani ya nchi ni muhimu kuliko ccm

mahakimu na majaji wanariporti kwa nani?
 
CCM ni chama cha Kitaifa na kimataifa..kisera na hata kiuongozi (mpangilio nk)

Chadema ni chama cha kidini (ukristo) na kichagga kisera na hata kiuongozi (mpangilio nk)

Utaratibu wa kupata viongozi wa juu unaratibiwa na kanisa..kwahiyo waislamu watawekwawekwa tena wachumia tumbo e.g. Prof. Safari, Yule makamu wa darasa saba (kama vile wamekosa educated muslims) wanafanya kiini macho....

Chadema ki-utaratibu kinahakikisha maslahi ya kifedha yanafaidisha wachaga..tafuta watunza fedha na watumiaji fedha wengi wanatokea huko..wengine mtachujwa na kuzushiwa kashfa mpaka muondoke...

Waislamu wenye uwezo wamebinywa kwa maelekezo ya kanisa katoliki (hidden) mfano Zitto will go no where??, jambo hili linaratibiwa katika jumuia za kanisa katoliki mitaani....

Wanaweza kujivua gamba wakidhamiria kweli..lakini wanakoelekea wataimba sana kupata nchi kwakuwa ni wabaguzi wengi wa washabiki wao ni "christian fundamentlist"

Nembo ya chama ni msalaba (mistari meusi) wakipata nchi wanakamisha...

wamejificha lakini wanaonekana wazi kwa tabia, nyendo zao...

Eeeh, Feedback, HEBU VUA HUO UDINI TUONE KAMA UNAWEZA KUJIBU HOJA ZA MSINGI BASI.
 
Topical,
Kinachonishangaza unapotoa hoja zako mara nyingi naona kama uko pekee
yako na siku zote hoja hujadiliwa na watu wakachangia na kuonekana upande
mmoja umeshinda,Lakini wewe mara zote nikiangalia hoja unazopinga naona
wazi umeegemea upande mmoja kama vile unafaidi zaidi matunda ya uhuru wa
Tanzania bila kuona huruma ya watanzania walio wengi.
Labda nikufahamishe kuwa CCM ni chama cha mapinduzi ya amani kati ya
vyama vya TANU(TAA) na ASP
CCM ni sehemu ya maisha ya watanzania,
ccm ni msingi wa siasa za Tanzania,kila mtanzania unayemuona leo ktk Siasa
ukiondoa wachache sana wametokea CCM,
Mimi ni mwanachama wa ccm kwa miaka 25 (Believe it NOT)
Tofauti iliyopo kati ya CHADEMA na CCM ni kuwa CHADEMA kwa miaka michache
sana tangu kuanza siasa za vyama vingi imeweza kuwa mshindani wa karibu sana
na CCM.Hizi ni jitihada za hali ya juu sana kwenye ulingo wa siasa za ushindani.
Kwa mantiki hii utaona wazi kuwa CCM imeshazeeka na inahitaji damu changa ili kiende na wakati
Sasa bahati hiyo tayari imeshapotea na badala yake imeshikwa na CHADEMA na kwa taarifa yako
CCM inaelekea UPINZANI.Huu ndio ukweli na wenyewe wameshakiri wamepoteza umaarufu na mvuto.
sasa ccm wameshaanza siasa za majitaka...oh chadema ni wachaga,mara ...oh chadema ni wakristo..
.oh chadema wanapoka demokrasia
Watanzania wameshajua nani mtetezi wa kweli hapa...ccm au chadema....niambie mwenyewe Topical.
Naomba uniambie sababu mbili (2) tu za kushindwa kwa ccm.
Sbabu (2) za CHADEMA kupanda chati.

Hapa JF of course hoja kama zangu lazima nitakuwa tofauti kwakuwa nina akili niko huru sifuati bendera fuata upepo

Pili Mwanakijiji ni katika mtandao huo huo wa kanisa katoliki (jumuia za kanisa zimejaa mitaani kupandikiza ubaguzi)

Proof namba moja kama mwandishi siku zote atamsifu mkristo mtawala, na chama ambacho ni kinaratibiwa na kanisa kikristo kama chadema na si vinginevyo umeshawahi kuona akiandika kuhusu CUF pamoja na kwamba ni chama kikubwa sana cha upinzani kwanini (hidden agenda), atafanyeje hayo wakati chama hicho hakifuati matakwa kutoka kwa jumuia?

Chadema haipendwi na watu, vyombo vya habari vinatuhadaa..what is 26% mkuu? pamoja na support kubwa ya fedha haramu za kanisa na mtandao mkubwa wa jumuia mitaani kuwashawashi watu wakipigie lakini wameambulia nini?

Wabadilike au watazimika kwa dhambi ya ubaguzi na kufanya usanii kuchagua waislam weak kwa maslahi fulani fulani?
 
Mnapojibu moto huu ni muhimu mkakumbuka kuwa mnachochea moto uliowashwa na mtu ambaye yeye na familia yake hawapo Tanzania.......

Ni hayo tu
 
duh jamii forum is the best place to be.......................................................viva MMJ:A S-rose:
 
Hapa JF of course hoja kama zangu lazima nitakuwa tofauti kwakuwa nina akili niko huru sifuati bendera fuata upepo

Pili Mwanakijiji ni katika mtandao huo huo wa kanisa katoliki (jumuia za kanisa zimejaa mitaani kupandikiza ubaguzi)

Proof namba moja kama mwandishi siku zote atamsifu mkristo mtawala, na chama ambacho ni kinaratibiwa na kanisa kikristo kama chadema na si vinginevyo umeshawahi kuona akiandika kuhusu CUF pamoja na kwamba ni chama kikubwa sana cha upinzani kwanini (hidden agenda), atafanyeje hayo wakati chama hicho hakifuati matakwa kutoka kwa jumuia?

Chadema haipendwi na watu, vyombo vya habari vinatuhadaa..what is 26% mkuu? pamoja na support kubwa ya fedha haramu za kanisa na mtandao mkubwa wa jumuia mitaani kuwashawashi watu wakipigie lakini wameambulia nini?

Wabadilike au watazimika kwa dhambi ya ubaguzi na kufanya usanii kuchagua waislam weak kwa maslahi fulani fulani?

Mkuu hapo kwenye red............. unaota ndoto za mchana au?? Ni chama cha upinzani wapi? CUF ni chama tawala siku nyiiiingiii, au unaishi nchi gani wewe?
 
Principles of valid inferences bado ni tatizo kubwa.Sizani kama Mwanakijiji anataka kutete udini wala ukabila.
Kimsingi amejaribu kuchambua SYLLOGISM iliyotumika kufikia hitimisho kwamba CHADEMA ni wachaga na ameonesha kwamba kama tukitumia hiyohiyo SYLLOGISM lazima tufikie hitimisho kwamba CCM ni cha WAISLAMU.
Hata hivyo ameonesha pia kwamba SYLLOGISM iliyotumika inapelekea kwenye FALLACY.
 
Mnapojibu moto huu ni muhimu mkakumbuka kuwa mnachochea moto uliowashwa na mtu ambaye yeye na familia yake hawapo Tanzania.......

Ni hayo tu

Moto uwashwe na wenzako unishakizie mimi? Hamtaki hata kuambiwa mmeuwasha moto, mnauchochea na mtu akiwaambia mnatuangamiza anakuwa ndiye "aliyeuwasha". Familia yangu huko Tanzania uliiondoa wewe au ndio mpango wa kutaka kuiondoa? Nilishawakatalia wengine kuwa hamuwezi kuwatenga Watanzania walioko nje ya nchi wasitolee maoni taifa lao kana kwamba wenye haki ni nyinyi ni uzao wenu. Its not going to happen.
 
Principles of valid inferences bado ni tatizo kubwa.Sizani kama Mwanakijiji anataka kutete udini wala ukabila.
Kimsingi amejaribu kuchambua SYLLOGISM iliyotumika kufikia hitimisho kwamba CHADEMA ni wachaga na ameonesha kwamba kama tukitumia hiyohiyo SYLLOGISM lazima tufikie hitimisho kwamba CCM ni cha WAISLAMU.
Hata hivyo ameonesha pia kwamba SYLLOGISM iliyotumika inapelekea kwenye FALLACY.

Tatizo ni kuwa wako tayari kukubali mwelekeo wa mantiki kwenda upande mmoja lakini kwa kutumia vigezo vile vile hawataki mwelekeo uende upande ule mwingine.

Mtu anasema "Binadamu wote ni sawa (kwa utu na hadhi yao)" vigezo kavitumia ni utu na hadhi
Halafu anasema "Hawa ni binadamu"
Kwa hiyo anataka tuamini kuwa "hawa" binadamu wote wako sawa kwa vigezo hivyo hivyo.

Tatizo ni kuwa atakuja na kusema "Huyu ni binadamu mndengereko"
na kusema "siyo sawa kwa utu na hadhi na binadamu mmakua yule".

Lakini ukimuonesha kujipinga kutokana na kanuni aliyoiweka mwenyewe anaanza kutafuta maelezo kwanini Mndengereko na Mmakua si sawa in light of "binadamu wote ni sawa kwa hadhi na utu". Wanasema Chadema ni chama cha Kichagga kwa uanzilishi wake, uongozi wake, na eneo lake la jiografia kilipokubaliwa awali. Hawajali kama kuna watu wa makabila mengine humo au Waislamu na wasioamini - hilo wakilikubali linavunja hoja yao kuwa CHadem ni chama cha Wakristu na Wachagga. Sasa tukitumia mtiindo huo huo - kwamba tusijali kama kuna Wakristu au Wachagga ndani ya CCM nasi tukafuata mtiririko huo huo wa mawazo tunaweza kusema tu bila shaka CCM ni chama cha Waislamu. Wao watakataa hilo na watajaribu kueleza kwanini CCM SIYO ya Waislamu lakini CHADEMA ni cha Wakristu! It baffles my mind. Na hawa ndio wanaitwa WASOMI.
 
Mwanakijiji nimekuwa nikisoma makala zako na thread zako zote ndani ya jf, sasa nakiri tanzania tutatoka shimoni ambako watawala uchwala wametupeleka. Jinsi ulivyopangilia hoja na kuiwakilisha nakuunga mkono kwa asilimia zote. Ni wendawazimu na ukosaji wa sera kwa kiongozi yeote wa kijamiii awe mwanasiasa, maalimu, askofu, mchungaji, katibu tarafa, economist na wengineo kuzungumuzia udini na ukabila karne hiiiii, watanzania tunashida nyingi saana zinazotaka majibu utashangaaaaa mtu anaongelea ukabila na udini -kiongozi wa nchi?????? Tena bila kuchukua hatua! Mimi nakubaliana na wewe ikitokea kiongozi anaendeleza majitaka hii wanachi tumvue madaraka.
 
Tatizo ni kuwa wako tayari kukubali mwelekeo wa mantiki kwenda upande mmoja lakini kwa kutumia vigezo vile vile hawataki mwelekeo uende upande ule mwingine.

Mtu anasema "Binadamu wote ni sawa (kwa utu na hadhi yao)" vigezo kavitumia ni utu na hadhi
Halafu anasema "Hawa ni binadamu"
Kwa hiyo anataka tuamini kuwa "hawa" binadamu wote wako sawa kwa vigezo hivyo hivyo.

Tatizo ni kuwa atakuja na kusema "Huyu ni binadamu mndengereko"
na kusema "siyo sawa kwa utu na hadhi na binadamu mmakua yule".

Lakini ukimuonesha kujipinga kutokana na kanuni aliyoiweka mwenyewe anaanza kutafuta maelezo kwanini Mndengereko na Mmakua si sawa in light of "binadamu wote ni sawa kwa hadhi na utu". Wanasema Chadema ni chama cha Kichagga kwa uanzilishi wake, uongozi wake, na eneo lake la jiografia kilipokubaliwa awali. Hawajali kama kuna watu wa makabila mengine humo au Waislamu na wasioamini - hilo wakilikubali linavunja hoja yao kuwa CHadem ni chama cha Wakristu na Wachagga. Sasa tukitumia mtiindo huo huo - kwamba tusijali kama kuna Wakristu au Wachagga ndani ya CCM nasi tukafuata mtiririko huo huo wa mawazo tunaweza kusema tu bila shaka CCM ni chama cha Waislamu. Wao watakataa hilo na watajaribu kueleza kwanini CCM SIYO ya Waislamu lakini CHADEMA ni cha Wakristu! It baffles my mind. Na hawa ndio wanaitwa WASOMI.
Mmmh!......mkuu mwanakijiji unatisha! Big up kaka
 
Back
Top Bottom