Tanzania Daima: Kama CHADEMA ni Wachagga, CCM ya Waislamu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Daima: Kama CHADEMA ni Wachagga, CCM ya Waislamu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, May 18, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,935
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180


  M. M. Mwanakijiji​


  NIVUNJE mwiko, nisivunje? Nimeamua kujitolea kuvunja mwiko hata kama hamtaki nivunje.

  CHADEMA ni chama cha Wachagga na CCM ni chama cha Waislamu. Huwezi kukubali moja ya hilo na ukakataa jingine. Vigezo vinavyotumiwa na baadhi ya watu kuitaja CHADEMA kuwa ni chama cha Wachagga tukivikubali bila kutumia uwezo tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu kuvihoji basi vinatusukuma kama mkokoteni ulioachiliwa kwenye mteremko na shehena ya madafu kufikia hitimisho kuwa CCM nayo yaweza kabisa kutajwa kuwa ni chama cha Waislamu.

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilipoanzishwa viongozi wake wengi wa awali walikuwa ni Wachagga. Na hata leo baadhi ya viongozi wake wengi ni Wachagga hata wale waliostaafu.

  Kutokana na historia hii baadhi ya watu (hasa wana Chama Cha Mapinduzi na wapinzani wengine) wamekitaja CHADEMA kuwa ni Chama “Cha Wachagga”. Na ni kutokana na hilo wamehitimisha pasipo kuonyesha uwezo wa kutumia mantiki kuwa CHADEMA ni chama cha kikabila. Kama kuna Wachagga wengi – wanasema, basi kuna ukabila.

  Baadhi ya viongozi wa kwanza wa Chama hicho ni pamoja na mzee Edwin Mtei, Freeman Mbowe, na Philemon Ndesamburo. Hawa watatu licha ya kuwa ni viongozi maarufu vile vile ni wafanyabiashara wakubwa nchini. Kwa vile uanzishwaji wa CHADEMA unahusishwa moja kwa moja na Edwin Mtei mtu wa Kilimanjaro na chama hicho kikavutia watu wengi wakiwemo baadhi ya hao wafanyabiashara basi kimekuwa kikitajwa tangu mwanzo kuwa ni chama cha Wachagga.

  Hivyo tunaweza kuona kwa urahisi kabisa kuwa tuhuma za Uchagga wa CHADEMA zinatokana na mambo makubwa matatu: uasisi wake, uongozi wake na nafasi za wanachama wake maarufu wanatoka maeneo gani ya nchi. Tukumbuke kuwa kinachoangaliwa katika “ukabila” huu ni kile kinachoonekana ni “wingi” au idadi ya Wachagga ndani ya CHADEMA na nafasi zao kubwa za kisiasa.

  Chama Cha Mapinduzi kilipoasisiwa (wakati huo kikiitwa TANU na ASP) viongozi wake wengi walikuwa ni Waislamu. Hili siyo siri. Kwa upande wa TANU viongozi waanzilishi wake kabla hata Mwalimu Nyerere hajahamia Jijini Dar na kuanza shughuli za kisiasa rasmi walikuwa ni Waislamu maarufu wa Jiji la Dar ambao majina yao yalikuwa yakijulikana wakati huo.

  Miongoni mwao tunaowakumbuka leo hii ni familia ya Sykes (maarufu kati yao akiwa ni Abdulwahid Sykes na kaka zake Ali na Abbas), masheikh maarufu wa Jiji la Dar es Salaam kama kina Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Chaurembo na mzungumzaji maarufu, Sheikh Suleiman Takadir.

  Kwa madhumuni ya hoja yangu siwahesabu Wakristu kama John Rupia, Vedasto Kyaruzi au Stephen Mhando ambao nao ni waasisi wa TANU kama vile ambavyo sitawahesabu watu wengine ambao hawakuwa Wachagga lakini walishiriki katika uasisi wa CHADEMA kama kina mzee Brown Ngwilulupi, Jacob Nkomola na Bob Makani. Tukiwaingiza hao wengine hoja yetu haitanoga.

  Ni Waislamu hata hivyo waliokuwa na nguvu zaidi ndani ya TANU kutokana na nafasi zao na uwezo wao wa kifedha katika Jiji la Dar. Walitumia mali na nafasi zao kuweza kukijenga chama na wengine walitoa hata nyumba zao kwa ajili ya matumizi ya TANU.

  Kitabu cha Mohammed Said cha Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968): Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati Za Waislam Dhidi Ya Ukoloni Wa Waingereza Katika Tanganyika kinaelezea kwa kina jinsi Waislamu walivyokuwa na nafasi ya pekee katika kuanzishwa kwa TANU kiasi kwamba sehemu mojawapo Said anatangaza pasipo shaka wala kujiuma meno kuwa “Kimsingi Chama cha TANU kilikuwa ni chama cha Waislamu”.

  Lakini siyo kutokana na uasisi wake tu ndio maana TANU ilikuwa ni chama cha Waislamu bali pia eneo lake ambapo kilikuwa na nguvu sana. Kama CHADEMA kuwa na nguvu kwa muda mrefu mikoa ya Kaskazini kutokana na kukubalika zaidi maeneo hayo TANU nayo ilikuwa na nguvu sana katika maeneo ya Pwani na maeneo ambayo yalikuwa na Waislamu wengi kama Tabora, Tanga na Dar yenyewe.

  Hivyo, kilikuwa ni chama cha Waislamu siyo kutokana na uasisi wake tu bali pia kutokana na maeneo yake ambayo kilikuwa kimekubalika zaidi kwani hata katika maeneo hayo mengine ni viongozi wengi wa Kiislamu waliokuwa wakijitokeza kukiunga mkono.

  Vile vile CCM baada ya kuundwa kufuatia kuunganishwa kwa ASP na TANU kilijikuta kimepokea viongozi wengi ambao ni Waislamu kutoka Zanzibar na matokeo yake hadi leo hii ni rahisi kuona kuwa Kamati Kuu inachukua wajumbe wengi kutoka Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya CCM kitu ambacho kinasababisha chama hicho kuwa na Waislamu wengi kwenye Kamati Kuu kutoka na wingi wa Waislamu wanaotoka Zanzibar.

  Hivyo basi tunalazimika kufikia mahitimisho yafuatayo tunapoviangalia vyama hivi viwili:


  CHADEMA ni chama cha Wachagga kwa sababu:
  • Kiliasisiwa na Wachagga wakiwa na nafasi za pekee.
  • Kilikubalika zaidi katika maeneo ya Kilimanjaro na Kaskazini (Moshi mjini na maeneo mengine).
  • Viongozi wake wameendelea kuwepo kuwa ni Wachagga.
  Kama Uchagga ni haya mambo matatu na watu wenye akili timamu wanakubali kuwa ni haya yanayofanya chama hicho kuwa cha “Kichagga” au cha “kikabila” basi ni kweli CHADEMA ni chama cha Wachagga na ni chama cha kikabila.


  CCM ni chama cha Waislamu kwa sababu:
  • Kiliasisiwa na Waislamu wakiwa na nafasi za pekee (Baraza la Wazee la TANU ilipoundwa liliundwa na Waislamu watupu).
  • Kilikubalika kwenye maeneo yenye Waislamu wengi
  • Viongozi wake wengi wameendelea kuwa ni Waislamu.
  Hivyo basi tunaweza kuona kitu kingine cha pekee ambacho kimefichika na huwa tunadokezwa nacho katika hizi tuhuma. Wachagga wengi ni Wakristu! Hivyo, kwa namna moja au nyingine tunaona kuwa tuhuma za “CHADEMA ni chama cha Wakristu” zinatokana na hilo vile vile na hivyo wale ambao wanakishambulia kuwa ni Chama cha Wakristu hufanya hivyo kwa sababu ile ile kwamba ni chama cha Wachagga.

  Matokeo yake tunalazimishwa kuiangalia CHADEMA aidha ni kama chama cha Wakristu au chama cha Wachagga kwa sababu mantiki inayopendekezwa mbele zetu haitupi uchaguzi mwingine wowote. Na tukifuata mlolongo huo huo wa mantiki tunajikuta tunaangalia CCM vile vile kama chama cha Waislamu na ukishaliona hili utaelewa ni kwanini baadhi ya Waislamu ambao walikuwa na tatizo na CCM miaka kadhaa huko nyuma leo hawana tatizo nayo kwa sababu wanaona kuwa kinaongozwa na “Waislamu”. Na matokeo yake utaona kundi la Waislamu hawa hawawezi kuona kosa au tatizo lolote lile la serikali kwani kwa kufanya hivyo itabidi wakubali matatizo ya “Muislamu” mwenzao au “Waislamu wenzao”.

  Ndugu zangu, hapa ndipo tulipofikishwa na watawala wetu walioshindwa; hapa ndipo tulipopigishwa magoti na kuambiwa tuabudu; naam, hapa ndipo tunalazimishwa kuangalia na kuangaliana kwa misingi ya dini na kabila. Na wapo baadhi ya watu kati yetu ambao wanaangalia Tanzania kwa misingi hiyo. Viongozi wengine, wakuu wa taasisi za umma ambao wakiona jina la Kichagga wanafikiria ni jinsi gani hawatompa mtu huyo nafasi.

  Kuna mifano ambayo siku moja ikiitwa wazi tutaona haya kwani baadhi ya watu wanaotukuzwa kwa “uongozi bora wa mashirika ya umma” ni wabaguzi wa kikabila waliokubuhu ambao wanastahili tuzo mbovu ya ufisadi wa kidini! Naam, wapo na wengine wanaochukulia hali iliyopo sasa na kuamini kabisa kuwa tatizo ni kikundi cha Waislamu na hivyo nao wanapoona jina la Muislamu wanaanza kufikiria wafanye nini naye au watumie mbinu gani kutokumtendea haki kwa sababu tu ni Mwislamu.

  Ndugu zangu, chuki ya kidini na kikabila ambayo inaenezwa na watawala walioko madarakani ni lazima ikataliwe na kila Mtanzania ambaye anakumbuka tunu za taifa letu. Chuki hizi zinapandikizwa kiujanja na wanasiasa walioshindwa hoja na hupepewa kama cherezi cha ubani na harufu yake mbovu hukumbatiwa na watu ambao hawataki kufikiri kwa kutumia chembe za ubongo walizojaliwa na Muumbaji wao.

  Leo hii tunawasikia wanasiasa wakubwa wa CCM wakizungumza bila haya wala kupepesa macho kuwa “CHADEMA ni cha Wachagga” na chama chao hata kuwakemewa hakithubutu na wanasiasa wapo ambao hueneza sumu hii ili kuwatisha Watanzania wengine. Kinachoniudhi mimi zaidi ni kuwa serikali ya CCM ndio imeshika madaraka na ndiyo inatakiwa kusimamia sheria zetu.

  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo Rais Kikwete, Rashid Othman, Waziri Mkuu Pinda, IGP, DPP, Mwanasheria Mkuu, majaji na viongozi wote wa kisiasa nchini wameapa kuilinda inasema hivi katika Ibara ya 20:2(a) kuwa hakuna chama chochote cha kisiasa (au kikundi) nchini ambacho kitaandikishwa chenye misingi au malengo ya “kukuza na kupigania” i. (i) imani au kundi lolote la dini; (ii) kundi lolote la kikabila pahala watu watokeapo, rangi au jinsia.

  Kama kweli watawala wetu ambao wanapigiwa saluti na kuhutubia kwa mbwembwe kuwa “Tanzania ni nchi ya utawala wa sheria” wanaamini kuwa walikula kiapo hatuna budi kuwauliza imekuwaje kuwe na Chama cha Wachagga ambacho kimeruhusiwa kushiriki uchaguzi na kushinda vizuri na kupata wabunge na madiwani wengi na kumsimamisha mgombea wa Urais ambaye alilindwa na vyombo vya dola wakati chama hicho ni cha kidini na cha kikabila?

  Swali hili wanahitaji kuulizwa watetezi wa CCM na wapiga panda wake ambao hukesha kutuambia kuwa CHADEMA ni chama cha kikabila na kidini wamechukua hatua gani kukifuta chama hicho?
  Nakumbuka Tendwa alitishia kuifuta CHADEMA si kwa sababu ya ukabila au udini wake bali kwa sababu ilikuwa imeing’ang’ania CCM kwa kuhoji matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  Tunajiuliza huyu Tendwa kwanini hajawahi kusimama na kuliambia taifa kuwa CHADEMA ni kweli chama cha Wachagga na kinavunja sheria na Katiba na hivyo kinafutwa? Kwanini hatujawaona wale wenye kuamini kuwa CHADEMA ni chama cha Wakristu na Wachagga hajawasimama na kuandamana kutaka sheria ifuate mkondo ili chama hicho kifutwe mara moja na mimi nitawaunga mkono! Jibu pekee ambalo tutapatiwa ni kuwa “kauli hizo zinatolewa na wanasiasa”. Kwamba maneno ya kada mmoja wa CCM kuwa asingeweza kujiunga na CHADEMA kama ilivyodaiwa kwa sababu ni “Chama cha Wachagga” ni ya kisiasa na hayana uzito wowote.

  Kwamba sumu inayoenezwa kwenye vyombo vya habari na radio maarufu nchini na kwenye hotuba mbalimbali za viongozi kadhaa kidini na kisiasa ni “uhuru wa maoni” basi tunalazimika kuhoji uwezo wa watawala wetu kuongoza. Katika suala la uhuru wa maoni kuna kanuni moja ambayo pale Marekani huwa wanaitumia sana kuzuia maoni yenye kuhatarisha usalama wa watu. Kwamba “huwezi kupiga kelele za ‘Moto Moto’ kwenye ukumbi uliojaa watu” wakati hakuna moto wowote na ukiulizwa useme ati “nilikuwa natumia haki yangu ya maoni”. Wale wanaotuambia “ukabila ukabila, udini na udini” kama hawamaanishi hicho na kama hakuna ushahidi wanachezea mchezo wa “moto moto”.

  Kuwaendekeza hawa ni kuliandaa taifa kwa majanga kwani chuki dhidi ya Wachagga ambayo imepandikizwa kwa muda mrefu katika jamii fulani ya watu inazidi kukua na sasa kuna ushahidi imepitishwa kwenda kizazi cha pili. Tunakumbuka sisi wengine kuwa chuki hii ilikuwepo wakati wa Mwalimu hadi tume ya Mang’enya ikaundwa kufuatilia na sasa hivi wameibuka watu wengine ambao wanalindwa na watawala walioko madarakani kwa ajili ya kujipatia manufaa ya kisiasa wakiendeleza chuki dhidi ya Wachagga.

  Watanzania ni lazima waanze kuwakataa viongozi hawa na wakati umefika kiongozi wa kisiasa yeyote atakayetoa kauli hizi na kushindwa kuthibitisha au kuchukua hatua kushughulikia wale wenye “ukabila” na “udini” ni lazima awajibishwe mara moja na hata ikibidi kuandamana kuwapinga. Ninaamini sasa CHADEMA wasivumilie tena tuhuma hizi ambazo wamezitolea ufafanuzi miaka nenda rudi lakini zinaendelea.

  Akijitokeza tena kiongozi yeyote wa serikali ambaye atadai CHADEMA ni cha Wachagga, CHADEMA iitishe maandamano ya kumuondoa mtu huyo madarakani kwani hatuwezi kuendelea tena kuchezea tunu zetu za taifa ambazo nilizigusia katika toleo lililopita. Wakati umefika kuwakataa viongozi wa aina hiyo.
  Na nina uhakika ukitaka kujua ni jinsi gani wana chuki dhidi ya Wachagga waulizeni mnataka CHADEMA iwafanye nini hao Wachagga walioko ndani yake? Mtashangaa watakavyojiuma meno kutafuta majibu. Hili nalo waulizwe wale wenye kudai kuwa CCM ni chama cha Waislamu.
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,467
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Nimeikosa Tanzania Daima ya leo ambayo inakuwa na makala nzito. Hadi saa mbili na nusu leo haikuwa vibandani.
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu na mimi nimekosa nimezunguka vibanda vyote hakuna
   
 4. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,172
  Likes Received: 4,505
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona huku kariakoo yapo mengi vibandani yamejaa watu wanayapita tu sijui kwa nini, labda mitaa ya Rombo ndio hamna
   
 5. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbona umekaa uchi? Unahitaji nini?
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,467
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Akina Kibanda wangetutangazia hata kupitia redio pendwa za asubuhi kama CloudsFM, RadioOne, .....Tanzania Daima ya Jumatano ni chakula cha ubongo kwa baadhi yetu.
   
 7. Josephine

  Josephine Verified User

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii picha yako inatishia amani,yaani mmechoka mpaka kusahau kuvaa nguo.Please be back to yourself.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,467
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Mwenge hayakuwepo, PostaMpya pia hayakuwepo. Ngoja nikalitafute huko Kariakoo.
   
 9. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Yap mi ndio nimelipata muda si mrefu naona mwanakijiji kapiga vibaya mno anasema "KAMA CHADEMA NI WACHAGA,CCM CHAMA CHA WAISLAMU?"
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,700
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  mkuu ndo maana hata cuf hawasemi eeeh!
   
 11. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Muchas gracias!, bravo! Mwanakijiji kwa "nguvu ya hoja"
   
 12. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 980
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ritz mbona picha yako ya avatar inatisha, utadhani ni yule binadamu wa kwanza aliyegundulika Olduvai. hayo mavidole hatari duh!! au upo tayari tayri kuchakaza mafisadi wa magamba
   
 13. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Henge tafuta hilo gazeti usome,namnukuu mwanakijiji paragrafu ya pili kutoka mwisho.anasema


  "Akijitokeza tena kiongozi yeyote wa serikali ambaye atadai chadema ni chama cha wachaga,Chadema iitishe maandamano ya kumuondoa mtu huyo madarakani kwani atuwezi kuendelea tena kuchezea tunu zetu za taifa ambazo nilizigusia toleo lililopita .Wakati umefika wa kuwakataa viongozi wa aina hiyo.Na nina uhakika ukitaka kujua ni jinsi gani wanachuki dhidi ya wachagga waulizeni mnataka chadema iwafanyie hao wachagga walioko ndani yake?Mtashangaa watakavyo jiuma meno kutafuta majibu.Hili nalo waulizwe wale wenye kudai kuwa CCM ni chama cha waislamu."Hayo ni maneno ya mwanakijiji kwenye tanzania daima la leo tarehe 18,mei,2011
   
 14. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sijutii kutolisoma hilo gazeti leo. Hili gazeti sasa hivi ni sehemu ya Habari Corporation. Hivi leo kweli mtu unaweza kuzungumzia Tanzania Daima wakati Raia Mwema iko mtaani? labda kama unataka kusoma mawazo ya mafisadi, ndo utapata Tanzania Daima.
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,134
  Likes Received: 836
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikalitafute.........
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,134
  Likes Received: 836
  Trophy Points: 280
  tafadhari fafanua sjakusoma siku hivi Tanzania Daima ni gazeti la mawazo ya mafisadi....!?
   
 17. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Precisely. It has of late become a mouthpiece of the Triplets!
   
 18. markach

  markach Senior Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tembelea www.freemedia.co.tz/daima. Utakutana na Gazeti la Leo
   
 19. m

  mob JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 1,788
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  hivi hili gazeti liko mtaani leo kweli
   
 20. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hakika umenikuna mwanakijiji. Naomba chadema wafanye yafuatayo;
  1. Kumstaki nape na ccm mahakamani ili wathibishe kuwa chadema ni chama cha wachaga.
  2. Naomba chadema wakomalie hiki kipengele cha uzushi ili kiingie kwenye katiba mpya
  Again, Uishi milele mkuuu.
   
Loading...