Mkuu, sababu ya mimi kuulizia hili ndo hiyo...nilipenda nijua..na possibly wengine wajue..je ni mkakati wa kuongeza mauzo? uhuru wa kupata habari huo....sidhani kama kuna ubaya walau tukajua kuwa sasa wamebadili mbinu..ili nijue kuwa nikitaka kusoma Tanzania Daima, nalipata muda gani kwenye mtandao!
Nimekupata, katika majibu yangu nilikuwa sijibu hoja yako ya awali moja kwa moja bali nilikuwa najibu kwa upana nikichukulia na mawazo ya Kasheshe na Pundit pia. Wewe kutaka kujua sababu ni jambo zuri na la kiungwana kulikuo kuassume kuwa ni "uzembe" kama alivyofanya Kasheshe.
Unazungumzia waliopo nchi zilizoendelea....well,, walioko huko hawana uwezo wa kupata hard copies otherwise sidhani kama ingekuwa tatizo kununua mkuu!
Believe me.. don't bet on that... Ni rahisi zaidi kudandia gazeti lililonunuliwa na mwingine kuliko mtu kununua lake mwenyewe. Kuna watu ambao sidhani kama watanunua hata kama gazeti linauzwa at minimum.
Mkuu mi nadhani hapa tukiingiza suala la 'udezo' tutafika siko....kama nilivosema....I just want to know if that is the case..na sio suala la dezo...
Nimekupata.. angalia jibu langu la kwanza hapo juu. Kuna watu ambao vya dezo vinavutia zaidi hata kama vina thamani sana. Lakini ukiweza fedha tu wanakimbia...
mfano hapa JF..watu wanakuja wanatoa mawazo maoni hoja etc...wanalipia? hawalipii..guess what? ni kwa namna gani JF imechangia kubadili hali ya mambo hususan ufisadi nyumbani? hata msomaji ambaye si mchangiaji, anabadilika kifikra kwa kusoma hapa JF...na nikikunukuu msemo wako mahiri wa 'mapambano ya kifikra....ndipo tunapotegemea ushindi zaidi..wa kifikra.
good you mentioned JF.. hivi unafikiri ikitokea kuwa JF ni by subscription unafikiri ni watu wangapi watakuwa tayari kulipia? Kati ya memba 5000 wangapi watakuwa tayari kufanya hivyo ambao tayari wamezoea kupata vya dezo (ingawa si dezo kweli kwani kuna watu wanalipia iende mbele).
Kwa mfano tufanye JF unaweza kuona ukurasa wa mbele tu lakini ukianza kuingia kwenye mada lazima uwe memba aliyelipia... utasikia malalamiko ya "sisi wanafunzi"... !
kwangu mimi gazeti kama Tanzania daima ni sehemu ya mapambano hayo! kama linasomwa na watu wengi, the better..manake ujumbe unakuwa unafika...sasa ukisema ni suala la kuzoea 'dezo' mkuu that sounds a bit offensive!
It is not my intention to offend you.. but the truth need to be told.. kuna watu ambao wamezoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi. Ni rahisi kulalamikia gazeti tunalolipata kwa bure kuliko kulalamika gazeti unaloligharimia. My worry is a sense of entitlement kwamba kwa vile sisi ndiyo wasomaji so we have to have what we want and now! Katika original posting umesema hivi:
Yote kwa yote, wanapaswa waelewa kuwa wana wasomaji wengi sana online na kuchelewa kutoka mtandaoni, wataanza kutupoteza taratibu
Hii kwangu ni kama katishio ka aina fulani kuwa wakichelewesha kutoka mtandaoni sisi wasomaji "wataanza kutupoteza taratibu" so bora waje na maelezo vinginevyo tutaenda kwenye vyombo vingine ambavyo vinatuletea habari wakati tunaotaka.
Na suluhisho sio 'kuanzisha vyombo vyetu' vya kujitolea...ukweli ni kuwa unapoingia kwenye biashara, iwe ya habari au nini. lazima uangalie hali ya soko kama je, unaweza kuhimili mikikimikiki ya ushindani? kwa sababu sasa hivi vyombo vya habari ni vingi na kila kimoja kinatafuta nafasi kwneye soko....so kwa sisi hatuwezi kuingia huko...lakini wapo wanaoweza kuingia huko na kutupa habari!
sasa wale wanaoingia kwenye biashara hiyo lazima pia waeleweke badala ya kubebeshwa lawama au kuonekana hawawajali "wateja" (of course wateja wasiolipia chochote).
Hilo halina tatizo waridi, lakini siamini kwua umeme unakatwa Tanzania Daima tu tena kila siku..kwa hiyo kuna zaidi ya umeme
Kuna watu kama Mwanakijiji wanasuggest kuwa hilo linatokana na mkakati wa kibiashara..kuwa kwa wao mauzo ya print ndo msingi wao mkubwa so inabidi 'waminye' kwanza kutoa online...sina tatizo na hilo na ndio maana nikaulizaa kuwa tatizo ni nini hasa....
mzee siyo kwamba na suspect; kwa vile siyo msemaji rasmi lakini nikiwa miongoni mwa waandishi wa gazeti hilo na mimi niliuliza swali hili hili over a week ago baada ya makala fulani kuchelewesha ndiyo jibu nililopatiwa. Ni uamuzi ambao umechukuliwa kati ya Raia Mwema na Tanzania Daima na hata MwanaHalisi. Vinginevyo kwa kadiri watu wanavyozidi kuongezeka wanaotumia intaneti nyumbani, basi magazeti yatakuwa yanayeza kupunguza mauzo.
Kimsingi hizi electronic editions za magazeti ni kwa ajili ya sisi hasa wa nje siyo wa ndani.