Tanzania Daima hamuitendei haki JamiiForums | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Daima hamuitendei haki JamiiForums

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JoJiPoJi, Oct 17, 2011.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,460
  Likes Received: 1,334
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikitegemea kupata habari kutoka hapa JF na kwa lugha nyingine wamekuwa wakifanya biashara ya kuuza habari ambayo tunazileta hapa bila idhini ya wamiliki wa habari husika.
  Kwenye gazeti la Tanzania Daima la leo ukurasa wa mbele kuna habari “viongozi chadema kuhujumiwa” hii habari bila shaka ilijadiliwa hapa kwa kirefu sana, ila leo inatumika kuuza gazeti, inasikitisha, basi wahariri hata wangetumia busara kusema chanzo cha habari yao ni JamiiForums ili angalau hata kijijini ambako hawajui jamii forums waanze kutafuta na kujua ni nini, habari zetu mchukue bure basi mtusaidie kututangaza
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Hakuna tatizo. Wamesaidia ujumbe uwafikie Watanzania wengi. Natamani kama magezeti na redio station zote wangechukua habari hapa jf ili ziwafikie Wananchi wengi.
   
 3. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sioni shida maana wana grounds za kujitetea bado, kwamba wamesoma hiyo habari hapa then wakaanza uchunguzi wao wa kina kujua kinachoendelea..then ndo waka publish.
  Pili, hili suala la kutumia majina anonymously .....linaweza kukufanya uhisi kwamba Tanzania daima wame copy and paste...kumbe muanzisha thread ni mwandishi wa Tanzania Daima.
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Wanazidi kuipandisha chati! mimi niliifahami jamiiforum kupitia gazeti la Raia mwema. uzuri waliuwa wanasema jf ndio chanzo cha habari yao!
   
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Je wewe unajuaje aliyeileta ndokaandika kwenye hilo gazeti???Think twice before provoke some one or something!!
   
 6. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,460
  Likes Received: 1,334
  Trophy Points: 280
  Naona hauelewi, hata kama aliyeileta hiyo habari hapa hata kama ni mwandishi wa gazeti hilo, bado jf inaendelea kuwa chanzo cha habari yake na alitakiwa awaambie wasomaji kuwa chanzo cha habari yake ni JAMIIFORUMS, au haujui kuwa kila unachoandika hapa kinabaki kuwa mali ya JF
   
 7. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,460
  Likes Received: 1,334
  Trophy Points: 280
  Na hilo ndilo linatakiwa, licha yakuwa jamiiforums hawazuhii kutumika kwa habari zake ila ni busara pia kuwajulisha wananchi kuwa habari kwa hisani ya JamiiForums
   
 8. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,460
  Likes Received: 1,334
  Trophy Points: 280
  Ndugu ninachoelewa kuwa kila kilichomo au kinachoanzishwa hapa JF kinabaki kuwa mali halali ya JamiiForums kisheria, sasa kama unahisi ukianzisha thread na baadae uiamishe unakuwa umetenda kosa kisheria
   
 9. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Umesoma disclaimer notice ya JF? Wanasema wao wala third parties hawatawajibika kwa info zozote zitakazoandikwa humu. Sasa iweje kuwe na contradiction na sheria unayoisema?

   
 10. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Unaweza kuita ukurasa wa maoni ya wasomaji katika gazeti "chanzo cha habari?". Jamii Forumns ni shirika la habari? Hiyo ni mosi. Pili ni kwamba huyo mtu aliyeleta "habari" hapa na kisha habari hiyo ikatoka gazetini amelalamilka? Kama hajalalamika kinakuudhi kitu gani?

  Tuaaandika hapa kwa dhumuni la kuwafikishia wananchi wenzetu wengi maoni yetu, na hata wakati mwingine kuwapa kile tunachoona ni "habari". Kama kuna magazeti yanasaidia kusambaza kwa wengi zaidi basi hilo halina noma. Si lazima watutaje. Kwani tuko hapa kutafuta sifa?

  Hongera Tanzania Daima. Tafadhali mtusaidie kusambaza zaidi mada zetu, ili tuiendeleze nchi yetu.
   
 11. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Yani habari yake mwenyewe aombe rukusa??
   
 12. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Unamwambia mwenzio 'think twice' wakati wewe mwenyewe huja-think twice! Kwa utaratibu wa haki miliki, hata kama ni wewe umeleta humu, basi sema imetoka JF ambako uliipeleka wewe kama sio kwamba chochote kinachoingia JF basi copyright ni ya JF.
   
 13. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  In the academic world, every fact must be cited and that is why you have authors referencing their old works in new ones (by mentioning name of the author-their name and year of publication). Tz daima were supposed to acknowledge the source of information regardless of whether the author is the same in all works.
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa vyovyo vile, Tz daima au mtu yeyote anayechukua habari kutoka JF anatakiwa kusema kuwa chanzo ni JF kama ambavyo wana-JF wamekuwa wakitaja vyanzo vyao!

  Najua wanasaidia kutangaza habari hizo na kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi, ila kama wangekuwa wametaja JF, kuna watu wengi zaidi wangevutiwa kuona original news na hata kuchangia!
   
 15. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri ni jambo jema kwa vyombo vingine vya habari kuiga Tanzania Daima sababu si Watanzania wote wanaoweza ku-access jamiiforum na ukjihabarisha,na ni vyema tukatambua kuwa wanajamiiforum ujitolea kwa kutafuta habari mbalimbali kwa vyanzo vyao na kuzileta jammiiforum ili umma wa Watanzania uhabarike,hata habari ya January Makamba na Barrick ingewafikia watanzania wengi kama ingetolewa kwenye magazeti ingawa hata hapa kwenye forum hatuioni tena.
   
 16. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  JF ni zaidi ya HABARI...tutake tusitake watakuja na kuchukua habari tunazopost..
  Ila kiungwana kama wamachukua humu ndani inabidi waseme..
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Unajuaje kama aliyeleta hii habari hapa anauhisiano na Tanzania Daima?
   
 18. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #18
  Oct 17, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,228
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Kibiashara ni haki jf ilipwe huo ndo ukweli na wawe wanataja kuwa chanzo ni jf
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hilo ndili suala la muhimu ambalo binafsi naliona. Hata kama JF ni free access, si sawa mtu kukomba kitu hapa JF na kusambaza kana kwamba yeye ndiye source!

  Inawezekana sana, ila kama hii habari ilitoka kwanza hapa JF kabla ya TZ daima, basi walitakiwa kusema hivyo ili waache kujichukulia ownership ya kitu ambacho tayari kiko kwenye public domain! Ndiiyo maana hata sisi (wana JF) tukichukua habari kutoka kwingine tunawajibika (sana sana morally and for credibility purposes) kuweka source ya habari tunazobandika hapa!

  Hili nadhani ni jambo jingine tena jipya.....Sina hakika kama JF imeweka vifungu vya kisheria ambavyo vinaiwezesha kudai malipo. Hata hivyo kuna sheria za free online documents ambazo inabidi sasa JF ianze kuziangalia kwa makini!

  Hivi nikiweka hapa copywrite materials nani anawajibika?
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu bahati mbaya humu hatujuani nani ni nani lakini kuna waandishi au kuna watu wenye uhusiano na waandhi wa habari si Tanzania daima tu hutusaidia kupata news na sisi kuzileta hapa sasa ukisema eti wasizitumie utakuwa unakosema......
   
Loading...