Tanzania: Crisis kubwa inakuja

Tanzania: Crisis kubwa inakuja

NAMPINGA TUNTU.

Wapo wasomi wa chuo kikuu wanataka kuwekeza ila wanaminywa, wananyimwa fursa na wale Miungu (walio serikalini). Wenzetu walio serikalini wanapenda sana 10%.

Hatuna uzalendo, tunapenda sana 10%.

Kwa mfano nataka kuwekeza kwenye kilimo, nataka hata angalau heka 10 nitapata wapi???

CHC wamekabidhiwa mashamba ya NAFCO na RANCH ila wamekalia hayo mashamba, wanasubiri dili za wageni wapate 10%

Au mwananchi wa kawaida hawezi pewa shamba ila vigogo wa CCM wanapewa heka 2000, 1000, 500. Refer Raisi Mwinyi, Mkapa, Sumaye, R One, Benno Ndulu, Charles Kimei na wengine.
 
Kwakweli hali mbaya, hii mada imenigusa sana..wasomi wengi wanakuwa hopeless...hata hiyo elimu inakuwa haina maana kama mtu anavyeti kibao halafiu vinakuwa kama mapambo, inasikitisha sana, hebu tusaidiane kukabiliana na hili jambo maana hali mbaya sana..
 
Hakika kuna ujio wa mpasuko wa kada ya wasomi ambao kuzuia hakutakuwa na madoido ya maujanja dotcom bali ni genuine kwa kuwa wasomi wanajua kinachoendelea.Mapinduzi ya Nchi za Kiarabu yamesababishwa na wasomi waliokosa kazi.
 
Mtazamaji said:
Sijawai kusikia wabunge wanaojiita vijana kama kina ziito, Makamba . H mdee na wnegine Wakiomba free time eg dar city center hata pale chuo cha IFM kwa dk japo 30 ili kupokea maoni na ushauri wa watu wa fani mbali mbali kotoa ofisi mbali mbali juu ya mambo kama
  • ICT
  • Uhandisi
  • walimu na elimu
  • Madereva
Nje ya kamati zao za bunge wabunge wanapata wapi taarifa na ushauri mbali mbali za kitaalam ambazo zinawza kusaidia kuhoji kama si kusuluisha matatizo mbali mbali?

comment Hii niliandika katika thread moja yenye tittle SIASA KIINI CHA MATATIZO MENGI LAKINI SIO SULUISHO LA HATA 15% YA MATATIZO YETU

Sasa ni kweli bwana kigwala alitambua hilo lakini je anajua kuwa yeye ni sehemu ya tatizo. Sijawai usikia wabunge wakiomba Maaafisa KILIMO, MIFUGO, BIASHARA, MISTU wa Mikoa na walaya wapewe mishahara minono.

  • Sijawai Kusikia mbunge akisema Kuwa kazi ya AFISA ELIMU, AFYA, KILIMO WA WILAYA NA MKOA Ni muhimu na majuumu mazito kulio kazi ua mbunge
  • Sijawai uona lecturer anaacha kazi CHUO kwenda kuwa AFISA KILIMO , AFISA MAJI, AU AFISA ELIMU.
Mwisho wa siku wasomi wanaongezeaka NEC yenyewe inaongeza majimbo ya uchaguzi,Serikali inaongeza wilaya Lakini mambo ya msingi ya ELIMU, AFYA, KILIMO watendaji wake huko wanakuwa hoi. hawapati ma VX. Haiwavutii vijana na wasomi.

So kifupi Tunajenga taifa la Wanasiasa na KISIASA . Hata hao wabunge wasomi wakishakuwa wabunge wanakuwa wanasiasa. tatizo wabunge wote wa upizani na CCM wanadhani wanajua suluisho la matatizo yote.
 
Nionavyo mimi pia ni kweli kwamba hili ni janga jipya,...ni zuri kwa wapinzani
kwani litachangia kuiondoa ccm madarakani,lakini halita wasaidia wapinzani sana baada ya hapo
maana tatizo hilo hilo laweza kuwaondoa madarakani pia.

Ni vyema sasa serikali ikaangalia jinsi ya kuwawezesha wasomi ili wajiajiri wao wenyewe.
Kwa mfano:-

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa
na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.
Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,
kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu

Tatizo lingine tumejengewa akili ya White colar jobs. Kazi za kalamu, kazi za suti. NDio maana wanasiasa wanakimbilia kuidhinishasha vyuo vikuu.
Wenzetu kenya Michezo ni kiini cha ajira. Wanaridha wa kenya form fr wanajuliakan kuliko wavaa suti na wasomi wakubwa.

  • Medali na mshiko inavunwa na watu amabo inawezekana wameshia form four kenya ilitawia iwe fundisho kwetu tunatakwiatufanye jambo. JKT na JWTZ wangeweza uongeza ajira binafis kwa kuibunua na kedeleza vipaji vya vijana.
  • Kuna wakenya wanakimbia kwa majina ya nchi nyingineka Qatar, UK, USA Norway. Kama hatuna fedha kwa nini tusiwatambue mapema wenye vipaji tuwaombe waendelezwe na norwaya au sweeden ikiwezekana wapeperiushe hata bendera zao lakini tanzania itakuwa imefaidika
  • Yule msukuma aliyeendesha baiskeli utokageita mpaka dar Jk angefanya kazi nzuri angemptaia jap traing akashiriki na kuwakilisha nchi kwenye cycling . Hata kama ngeshindwa lakini Hizo ndio investment watu wanasiasa wanatakiwa kutambua.
 
Nionavyo mimi pia ni kweli kwamba hili ni janga jipya,...ni zuri kwa wapinzani
kwani litachangia kuiondoa ccm madarakani,lakini halita wasaidia wapinzani sana baada ya hapo
maana tatizo hilo hilo laweza kuwaondoa madarakani pia.

Ni vyema sasa serikali ikaangalia jinsi ya kuwawezesha wasomi ili wajiajiri wao wenyewe.
Kwa mfano:-

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa
na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.
Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,
kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu

usitegemee lolote kwa serikali hii inayoendesha mambo yake kwa kugawa tisheti na khanga.

dawa ni kuwang'oa tu.
 
Taaluma haizingatiwi tena siku hizi. Engineers na Doctors wanakuwa politicians, bankers etc
na wamejaa kweli kwenye siasa... ukiwasikiliza sometimes huwezi hata kujua kama walifika hata form four. but there are a few good politicians
 
The first useful thread to real national interests in a veeeery long time....reminds me of the old JF.
 
Miaka 26 baada ya ujamaa kuzikwa hapa nchini bado kuna tuna fikra tegemezi sana, bado wananchi ata wale waliobahati kupata elimu nzuri wanategemea eti serikali iwalishe chakula mdomoni, fikra potofu sana hizi.

Serikali imefanya wajibu wake kwa kuhakikisha hao "unaowaita wasomi" wamepata elimu yao, . Tunatarajia kuwa mtu mwenye elimu ya "chuo kikuu" awe na uwezo wa kuyasoma vizuri mazingira yake, kuangalia matatizo yaliyopo, na kuyatafutia ufumbuzi kwa faida yake binafsi na taifa kwa ujumla. hivyo ni wajibu wa hao wasomi wenyewe, kupitia elimu zao ambazo zinapaswa ziambatane na ujuzi, maarifa na fikra sahihi kuweza kuanzisha shughuli za uzalishaji mali na kuwaajiri wengine ambao hawakupata fursa za "elimu".

Naamini kama wameelimika vizuri, kama elimu imewawezesha kuyajua mazingira yaliyopo vizuri, basi watakuwa na uwezo wa kuzitumia fursa zilizopo kujikomboa kiuchumi, la kama hawawezi basi tatizo lao kubwa "lipo kwenye fikra zao" wenyewe na hivyo ata kama serikali ingewapa mitaji, mitaji hiyo haitawasidia lolote na mwisho wa siku itakuwa ni matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi wengine.

Naamini msaada wa serikali katika hili unaweza ukawa tu kwenye kuwaunga mkono wale "walioweza kufikiri na kuanzisha "shughuli zao" kwa kutoa upendeleo maalumu kwa kampuni za ndani kwenye baadhi ya kazi/huduma full-stop.

Jamani muda wa kuisubiri serikali ikuletee chakula mezani umepita, ebu tutambue kuwa "Ujamaa Umekufa Na Hautarudi Tena", ebu tubadilike kifikra na tuitumie elimu tuliyoipata kujikomboa wenyewe, nchii hii bado ni "bikira" kwa kiwango kikubwa na hii ni fursa kwa "msomi aliyeelimika", unachopaswa kufanya ni kufungua tu macho yako na kufikiri kwa bidii sana.
Siyo fikra tegemezi kuitaka serikali yako iwezeshe kupatikana kazi. Marekani Obama hivi sasa anaendeshwa puta kwa sababu ya ajira, ajira, ajira.
Ni kazi ya serikali kuunda sera zitakazowezesha kupatikana kwa ajira.
 
Tatizo la Tanzania si kukosekana ajira tu bali elimu duni. Unakuta watu wanafika chuoni hawajua kuongea Kiingereza vizuri (hapa msiseme lugha ya taifa kwa maana tunajua fika kwenye soko la ajira siku hizi lugha hii ni muhimu) na wala hajui kujenga hoja. Elimu yetu ni theoretical na siyo practical kwa hiyo mtu akitoka chuoni hajui afanye nini bila kusoma sehemu. Tuna tegemea ajira ya serikali na wakati muajiri mkuu kwenye nchi yoyote ina takiwa iwe sekta binafsi. Wataalamu wengi tulio nao siyo free thinkers bali nao wanaleta siasa. Matatizo ni mengi sana.

Suluhisho:
Tuifanye overhaul sekta nzima ya elimu Tanzania. Elimu yetu lazima ikidhi mahitaji yetu. Elimu yetu ina kazania sayansi na hisabati wakati nchi nzima hatuwezi kuwa wanasayansi au madokta.

Shule za serikali ziwe bure kwanzia la kwanza mpaka kidato cha sita.

Tuwa wezeshe wale ambao hawata weza kufika chuo kikuu. Tume kazania wasomi na wakati tuna idadi kubwa ya wananchi ambao hata hawafiki chuo kikuu. Je hawa tuwa tumiaje wanufaishe jamii zao na taifa kiujumla?

Tuondoe siasa kwenye elimu na tukazanie taaluma.

Tuwe na mpango wa kuwa wezesha wananchi kujitengenezea ajira na kutengeneza ajira kwa wengine. Serikali haiwezi kuwa muajiri mkuu wa nchi.

Tuwe na kima cha chini kinacho endana na uhalisia wa maisha ya Tanzania.

Serikali itengeneze mipango endelevu ya muda mfupi na muda mrefu.

Tu encourage watu watumie taaluma zao. Kuna wasomi wengi wanasomea kitu fulani lakini kwenye ajira wanafanya kitu tofauti kabisa.

Tuondoe rushwa. Ajira zipo nyingi tu siyo kwamba hazipo. Tatizo mtu kupata ajira ni mpaka ujuane na mtu.
 
NAMPINGA TUNTU.

Wapo wasomi wa chuo kikuu wanataka kuwekeza ila wanaminywa, wananyimwa fursa na wale Miungu (walio serikalini). Wenzetu walio serikalini wanapenda sana 10%.

Hatuna uzalendo, tunapenda sana 10%.

Kwa mfano nataka kuwekeza kwenye kilimo, nataka hata angalau heka 10 nitapata wapi???

CHC wamekabidhiwa mashamba ya NAFCO na RANCH ila wamekalia hayo mashamba, wanasubiri dili za wageni wapate 10%

Au mwananchi wa kawaida hawezi pewa shamba ila vigogo wa CCM wanapewa heka 2000, 1000, 500. Refer Raisi Mwinyi, Mkapa, Sumaye, R One, Benno Ndulu, Charles Kimei na wengine.

Hizo haziwezi kuwa sababu za msomi kushindwa kujiajiri, bali ni dalili za ukosefu wa maarifa, taarifa, na udhubutu wa kijasiriamali, hasa kutokana na wasomi wetu kujawa na mawazo tegemezi.

Sijui kama umeshazunguka vijijini, ndugu yangu wala hauna haja ya kushindania hizo zilizokuwa ranchi za taifa, kuna ardhi kubwa na ya kutosha katika nchi hii, tatizo la wasomi wetu halipo kwenye urasimu serikali wala halipo katika pesa, ni ukosefu tu wa maarifa tu.

Ebu kisome kijitabu hiki kidogo,http://www.changeagent101.com/lib/richdad.pdf
 
Miaka 26 baada ya ujamaa kuzikwa hapa nchini bado kuna tuna fikra tegemezi sana, bado wananchi ata wale waliobahati kupata elimu nzuri wanategemea eti serikali iwalishe chakula mdomoni, fikra potofu sana hizi.

Serikali imefanya wajibu wake kwa kuhakikisha hao "unaowaita wasomi" wamepata elimu yao, . Tunatarajia kuwa mtu mwenye elimu ya "chuo kikuu" awe na uwezo wa kuyasoma vizuri mazingira yake, kuangalia matatizo yaliyopo, na kuyatafutia ufumbuzi kwa faida yake binafsi na taifa kwa ujumla. hivyo ni wajibu wa hao wasomi wenyewe, kupitia elimu zao ambazo zinapaswa ziambatane na ujuzi, maarifa na fikra sahihi kuweza kuanzisha shughuli za uzalishaji mali na kuwaajiri wengine ambao hawakupata fursa za "elimu".

Naamini kama wameelimika vizuri, kama elimu imewawezesha kuyajua mazingira yaliyopo vizuri, basi watakuwa na uwezo wa kuzitumia fursa zilizopo kujikomboa kiuchumi, la kama hawawezi basi tatizo lao kubwa "lipo kwenye fikra zao" wenyewe na hivyo ata kama serikali ingewapa mitaji, mitaji hiyo haitawasidia lolote na mwisho wa siku itakuwa ni matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi wengine.

Naamini msaada wa serikali katika hili unaweza ukawa tu kwenye kuwaunga mkono wale "walioweza kufikiri na kuanzisha "shughuli zao" kwa kutoa upendeleo maalumu kwa kampuni za ndani kwenye baadhi ya kazi/huduma full-stop.

Jamani muda wa kuisubiri serikali ikuletee chakula mezani umepita, ebu tutambue kuwa "Ujamaa Umekufa Na Hautarudi Tena", ebu tubadilike kifikra na tuitumie elimu tuliyoipata kujikomboa wenyewe, nchii hii bado ni "bikira" kwa kiwango kikubwa na hii ni fursa kwa "msomi aliyeelimika", unachopaswa kufanya ni kufungua tu macho yako na kufikiri kwa bidii sana.

Sawa mkuu,hatuongelei ujamaa lakini tunaongelea sera mbovu za elimu
ambazo zinatengeneza watu ambao wanasiasa wana waita "wasomi" lakini kiukweli
ni bomu ambalo litakuja kuwasumbua au kuisumbua serikali kwa mda mrefu.

Bajeti nyingi za serikali ni za kisiasa,kila kitu wanacho fanya ni siasa tu.
Hakuna mipango ya mda mrefu zaidi ya miaka mitano (5) wakimaanisha wana focus
uchaguzi hadi uchaguzi.

Nimemaliza form6 mwaka 2009 na kujiunga chuo mwaka huo.
Tuliokua tunasoma sayansi tuliahidiwa "mkopo 100%" na tukapewa kweli.
Kwa nini? kwa sababu walikua wana focus kwenye uchaguzi wa 2010.

Unajua mwaka huu (2011) wametoa vipi mkopo baada ya uchaguzi kuisha?
Hakuna cha 100% tena,wanao soma course kama yangu wapo waliopata 80% wengine 70%,..
kwanini?
Ni ubabaishaji mwanzo mwisho.

Hakuna anae taka kulishwa siku zote,kwanza ni kujidhalilisha kulishwa milele kwa hiyo hatulilii kulishwa.
Tunataka kuwezeshwa kwa sababu hatuna msingi financially kwa kujiinua na kufanya kile tunacho weza.

Hebu nambie,nimemaliza civil engineering kwa mfano,...unategemea nipate wapi mtaji wa kufanya kazi
zinazo husiana na taaluma yangu ili hata baadae niajiri wengine?

Nadhani umetoa mfano ukidhani kila anae soma chuo ni mtoto wa fisadi,wengine hata mkopo
kidogo tunaopata tunasomesha wadogo zetu shule za kata,...
 
NAMPINGA TUNTU.

Wapo wasomi wa chuo kikuu wanataka kuwekeza ila wanaminywa, wananyimwa fursa na wale Miungu (walio serikalini). Wenzetu walio serikalini wanapenda sana 10%.

Hatuna uzalendo, tunapenda sana 10%.

Kwa mfano nataka kuwekeza kwenye kilimo, nataka hata angalau heka 10 nitapata wapi???

CHC wamekabidhiwa mashamba ya NAFCO na RANCH ila wamekalia hayo mashamba, wanasubiri dili za wageni wapate 10%

Au mwananchi wa kawaida hawezi pewa shamba ila vigogo wa CCM wanapewa heka 2000, 1000, 500. Refer Raisi Mwinyi, Mkapa, Sumaye, R One, Benno Ndulu, Charles Kimei na wengine.

Nahisi kuna haja ya ile hoja ya kuanzisha baraza la vijana
la kitaifa kuanzishwa mapema.

Hili lita saidia ku-air out maoni ya vijana maana so far hakuna anae ongelea
swala la sera za ajira na uwezeshaji wa graduates.
 
Kwa jinsi mfumo wetu ulivyo,mtu akiwa anafaulu vizuri mitahani yake tuu... HUANZA KUFIKIRIA KUAJIRIWA/kutumika. Badala ya kutumia hiyo akili kubuni kitu kipya kitacho mfanya ajiajiri.

Huwa nasikitika sana kuona mtu analalamika eti hana ajira, na mda huo huo ukimpa hata laki tano hujui aanzie wapi kuitumia/kuizungusha. Hii ni kwasababu tukiwa mashuleni badala ya kuelimishwa... tunaimbishwa/mezeshwa. Hasara ya hii ni kuwa na akiri tegemezi(baba anaziita "AKILI ZA CHANJO"). MFANO MZURI NI WEWE MWENYEWE HAPO ULIPO UNAITUMIAJE HIYO INTERNETR CONNECTION TO MAKE MAXIMUM AMOUNT OF MONEY?.

Watanzania wangapi wanajitahidi kujineemesha na huu "u-bikra" wa taifa letu legaly?...

Asilimia kubwa ya watanzania tunaamini kuwa "UKITAKA UENDELEE, LAZIMA UWE NA MTAJI/PESA". Sasa hapa ndio mwanzo wa anguko letu. wengi tunafikia conlussion kwamba... "ILI UPATE MTAJI, SHARTI UAJILIWE KWAZNZA" ...Tunasahau kwamba mishara mingi tunayo ripwa, huishia kutulisha tuu.. na sii vinginevyo. BWT Nyerere aliliona hili(SOMA AZIMIO LA ARUSHA)

SWALI.. Hivi tangu SUA ianze, kuna mtu yeyote aliyesoma pale, na leo anafahamika kama mkulima mkubwa hapa tanzania?. LAILA ODINGA ALISHA WAHI KUSEMA KUWA HUWA ANASHANGAA SANA KUONA MTU ANA DEGREE YAKE,HARAFU ANATEMBEZA VYETI MAOFINI. elimu hapa inakua useless....

"USHINDANI NI KIWANDA CHA UBINUFU"= G NAKO. kwa hili taifa letu ushindani kwenye mambo ya maendeleo haupo,na badala yake tuaendeleza upinzani kwenye maendeleo. JANGA LA KITAIFA HILI.. Hivi tanzania mpaka sasa inashindana na nchi gani kimaendeleo?. mimi mpaka sasa sijui, zaidi ya kusikia viongozi wetu wakijilinganisha ubora na nchi kama somalia.

SERIKALI kwa sasa inahitaji kutu kimoja "propaganda" zitazo saidia kutubadilisha mawazo ya kusoma ili kuajiriwa,hadi kusoma ili kujiajiri. the people must be able to think out of the box!!. NOTE: "PROPAGANDA BILA SERA ZINAZOTEKEREZEKA=KUWAHADAA/KUWATUKANA WANANCHI"

Serikari ijayo itabidi ijitahidi sana KU-EMPOWER VETA ili vijana wanaotoka hapo, wawe working machine wa taifa letu(hawa wa veta wengi wao wataajiriwa na wale wenye degree waliofanikiwa kujiajiri).

SWALI: ni watu wangapi hapa dunia walio AJIRIWA leo hii tunawafamu kama matajiri wakubwa???.

You have written well mkuu.
Thanks,nimepata kitu toka kwako
 
Siyo fikra tegemezi kuitaka serikali yako iwezeshe kupatikana kazi. Marekani Obama hivi sasa anaendeshwa puta kwa sababu ya ajira, ajira, ajira.
Ni kazi ya serikali kuunda sera zitakazowezesha kupatikana kwa ajira.

Na ndicho kitu ambacho hakipo tanzania.
Unapo piga kelele kuwakumbusha wanakuja wengine kusema "hamfikirii"
sijui kufikiria gani wanakotaka tufikirie,....tushafikiria hadi madonda ya tumbo tunayo
 
pamoja na yote hayo kuna kitu hakijadiliwi hapa....

nacho ni vyuo vingi kutoa wanataaluma wa fani zinazofanana na ambazo ajira zake ni chache...ndani na nje...

tungekuwa na graduates wengi wa sekta ya afya kwa mfano....tatizo lisingekuwa kubwa hivi...
 
lakini halita wasaidia wapinzani sana baada ya hapo
maana tatizo hilo hilo laweza kuwaondoa madarakani pia.

Mkuu mimi kwa sasa napenda upinzani, nauunga mkono na napenda uingie madarakani. Lakini wakiingia madarakani wasidhani nitaingia nao. Nitabaki kuwa mpinzani na nitasapoti wapinzani wa wakati huo ili uchaguzi unaofuata waingie madarakani, kisha niwatose, nianze kusapoti wapinzani wengine. Kwa ufupi mimi ni mpinzani damu...
 
Hahaha,ume nifurahisha sana aisee.
Asante sana
 
Nahisi kuna haja ya ile hoja ya kuanzisha baraza la vijana
la kitaifa kuanzishwa mapema.

Hili lita saidia ku-air out maoni ya vijana maana so far hakuna anae ongelea
swala la sera za ajira na uwezeshaji wa graduates.

Mkuu naomba nikukosoe na na na wewe unalta siasa. Za kuwasahau vijana na unasisistiza graduates. baraza la vijana litakaiwa kuongela vijana. Bomu la jaira si la gradutaes tu bomu la ajiralipo hata wa walioishia darasa la saba, form four ,na form six. Ni haki yao kupata ajira na ipato kama wako kijijini.

Kijana kama yu tabora vijijini anatakiwa japo akimaliza la saba au foru four awe anajua jisni ya kijiari wa asali kisasa.
Vijana wa arusha Arusha mwenye vipaji vya kukimbia wanataikiwa wajuliane mapema na JKT iwatarishe mapema ili hata wasipoendela a elimu ya mbele wawe na kipaji kinachweza kuwaingia kipato

Sasa mbunge ana ofisi. Samani za ofisi ya mbuge zinagizwa kutoka dar na dar zinaagizwa kutoka China. Hakuna ubunifu wa mbunge kujua hata yeye anaweza kuajiri kuwa Samani za ofisi yake zitengenzwe na fundi kwenye wilaya yake. NI sababu ya Siasa wanasema taratibu za Manunuzi zilifuatwa.

Hao wanasisasa wanavaa suti za Italy. Sidhani kama kuna mbunge ana uzalendo wa kushonesha hata suti moja kutoka kwa fundi jimboni kwake. Sidhani kama kuna mbunge anaweza kujivunia i uuwa na pair moja ya kiatu atu cha kuchonga. Wanaona aibu.

Kwa hiyo mkuu unazumguzi bomu la vijana sio Graduates tu. La sivyo roba za mbao hazitaisha. TUtasikia hata bibi zetu vijijini wanaanza kupigwa roba za mbao na vijana sababu baraza la vijana wa mjini lilifikira graduates tu.
 
Back
Top Bottom