Tanzania: Crisis kubwa inakuja

Mkuu naomba nikukosoe na na na wewe unalta siasa. Za kuwasahau vijana na unasisistiza graduates. baraza la vijana litakaiwa kuongela vijana. Bomu la jaira si la gradutaes tu bomu la ajiralipo hata wa walioishia darasa la saba, form four ,na form six. Ni haki yao kupata ajira na ipato kama wako kijijini.

Kijana kama yu tabora vijijini anatakiwa japo akimaliza la saba au foru four awe anajua jisni ya kijiari wa asali kisasa.
Vijana wa arusha Arusha mwenye vipaji vya kukimbia wanataikiwa wajuliane mapema na JKT iwatarishe mapema ili hata wasipoendela a elimu ya mbele wawe na kipaji kinachweza kuwaingia kipato

Sasa mbunge ana ofisi. Samani za ofisi ya mbuge zinagizwa kutoka dar na dar zinaagizwa kutoka China. Hakuna ubunifu wa mbunge kujua hata yeye anaweza kuajiri kuwa Samani za ofisi yake zitengenzwe na fundi kwenye wilaya yake. NI sababu ya Siasa wanasema taratibu za Manunuzi zilifuatwa.

Hao wanasisasa wanavaa suti za Italy. Sidhani kama kuna mbunge ana uzalendo wa kushonesha hata suti moja kutoka kwa fundi jimboni kwake. Sidhani kama kuna mbunge anaweza kujivunia i uuwa na pair moja ya kiatu atu cha kuchonga. Wanaona aibu.

Kwa hiyo mkuu unazumguzi bomu la vijana sio Graduates tu. La sivyo roba za mbao hazitaisha. TUtasikia hata bibi zetu vijijini wanaanza kupigwa roba za mbao na vijana sababu baraza la vijana wa mjini lilifikira graduates tu.

Kweli kabisa mkuu nimekusoma.
You're right

Hili tatizo ni kubwa zaidi ya tunavyodhani ,vijana wengi wanalalamika hawana kianzio au mtaji
Je ,wakiwezeshwa kifedha kama wengi wanavyotaka watafanikiwa ?
Binafsi bado ni mwanachuo ila kwa niliyoyashuhudia , sayansi imekua chaka la kutoa la kutoa vyeti tu
ila graduates wengi hatujitoshelezi ki maarifa
Hata tukiweka sera gani , ila kwa elimu hii hatutafika mbali

kweli mkuu, nilikuwa na demu mmoja alimaliza SUA sijui ndo Agricultural Engineering, sasa hivi ni afisa mikopo PRIDE
Kuna mdada amemaliza SUA, akaombwa awe meneja wa kijiji,akaikataa kazi..yupo NMB sasa hivi.
Hapo tutaendelea?

Haijalishi nenda shule yako,utakuwa na profesheni yako,na unasaidia jamii kila kukicha,
Lakini katibu kata au diwani ambao hawana upeo kama wewe wata kunyanyasa nakukutharau na kukutapeli kila siku
wakikiambia kama we hutoi mchango ccm,umeumia.
wakati ni darasa la saba.Je tutafika wapi

Nionavyo mimi pia ni kweli kwamba hili ni janga jipya,...ni zuri kwa wapinzani
kwani litachangia kuiondoa ccm madarakani,lakini halita wasaidia wapinzani sana baada ya hapo
maana tatizo hilo hilo laweza kuwaondoa madarakani pia.

Ni vyema sasa serikali ikaangalia jinsi ya kuwawezesha wasomi ili wajiajiri wao wenyewe.
Kwa mfano:-

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa
na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.
Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,
kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu

Kuhusu swala la wimbi la wasomi wanaokaa vijiweni na kuchomwa na jua kutwa nzima kama solar pannel litaifikisha Tanzania pabaya coz wasomi wanaokosa ajira na kukaa vijiweni wanaushawishi mkubwa kwa umma ivyo huanza kutumia elimu yao kuanzisha movement zenye hisia ya kupambania haki ya wanyonge wanonyonywa na wanasiasa. Tanzania ina wasomi wengi wasio na ajira na wanazidi kuongezeka ila ipo siku huu mzaa mzaa ukiendelea wasomi hawa wasio na ajira wataanzisha mambo makubwa kwa kutumia kalamu na ushawishi walio nao kwa umma dhidi ya serikali. Kenya limeibuka kundi la MUNGIKI ambapo serikali ya Kenya kwa uoga inajaribu kulichafua kundi hili kua ni kundi la wauwaji ila kiukweli MUNGIKI ni community inayosimamiwa na wasomi kadhaa wa Kenya wasio na ajira. Tazama documentary hii hapa chini ujionee ukweli wa wasomi wa Kenya maarufu kama MUNGIKI wanavyopambana na serikali yao yenye dhuluma.[video]www.youtube.com/watch?v=1EMFUxA0zS0[/video]

Nionavyo mimi pia ni kweli kwamba hili ni janga jipya,...ni zuri kwa wapinzani

kwani litachangia kuiondoa ccm madarakani,lakini halita wasaidia wapinzani sana baada ya hapo

maana tatizo hilo hilo laweza kuwaondoa madarakani pia.

Ni vyema sasa serikali ikaangalia jinsi ya kuwawezesha wasomi ili wajiajiri wao wenyewe.

Kwa mfano:-

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa

na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.

Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,

kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu

Hapo kwenye red kama CDM itakamata dola na mm nikiwa mwanachama hai this is a biggest opportunity kwao na wala siyo tatizo kwani kitu watakacho kifanya kitaipa legacy na a big difference kati yake na CCM....Acha kwa sasa tuwatumie kupata dola maana CCM hawakawii ku copy na ku paste, then baada ya hapo wanageuka kuwa mtaji wa kuendelea kuwaongoza kwa muda mrefu....

Wasomi hawajawahi kuwa burden hata siku moja katika historia ya dunia zaidi ya kuwa resource kama watatumiwa effectively na efficiently! Tatizo ni kuwa muhimili mkuu wa CCM ni ufisadi na kwakuwa wasomi wako objective basi lazima kwao wawe bomu litakalo walipukia.

NAMPINGA TUNTU.

Wapo wasomi wa chuo kikuu wanataka kuwekeza ila wanaminywa, wananyimwa fursa na wale Miungu (walio serikalini). Wenzetu walio serikalini wanapenda sana 10%.

Hatuna uzalendo, tunapenda sana 10%.

Kwa mfano nataka kuwekeza kwenye kilimo, nataka hata angalau heka 10 nitapata wapi???

CHC wamekabidhiwa mashamba ya NAFCO na RANCH ila wamekalia hayo mashamba, wanasubiri dili za wageni wapate 10%

Au mwananchi wa kawaida hawezi pewa shamba ila vigogo wa CCM wanapewa heka 2000, 1000, 500. Refer Raisi Mwinyi, Mkapa, Sumaye, R One, Benno Ndulu, Charles Kimei na wengine.

Wakiwaacha maisha yao ya ufisadi yako hatarini....Na yakujipa madaraka wasiyo stahili; hivi vyote ndiyo sababu kuu ya hofu ya hawa mabwana otherwise kuwa na resource pool kubwa haiwezi kuwa tatizo kwa taifa lolote lile objective.

Nionavyo mimi pia ni kweli kwamba hili ni janga jipya,...ni zuri kwa wapinzani
kwani litachangia kuiondoa ccm madarakani,lakini halita wasaidia wapinzani sana baada ya hapo
maana tatizo hilo hilo laweza kuwaondoa madarakani pia.

Ni vyema sasa serikali ikaangalia jinsi ya kuwawezesha wasomi ili wajiajiri wao wenyewe.
Kwa mfano:-

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa
na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.
Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,
kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu

Wakuu kujiajiri proffesionally siyo kitu rahisi for a fresh from school candidate but is possible. Ndiyo maana mnasikia wamarekani wakilalamika jobs jobs kila siku. Personally I have a very good experience towards kujiajiri, I am a living proof kuhusu success and difficulties kuelekea kujiajiri proffesionally. It is not as simple kama watu wengi wanavyofikiri au ku-portray. Anyways kuna mambo yafuatayo yanatakiwa yazingatiwe.

1. Ufahamu wa hiyo shughuli unayotaka kujiajiri nayo. Hakuna chuo kikuu duniani kinakufundisha say kuwa injinia wa kwenye cement, au karatasi, au chuma. Vinanvyofundishwa shule ni fundamentals na principles. Ukienda kwenye industry ndiyo unakutana na specific trainings.

2. Uzoefu wa shughuli unayotaka kufanya. Kumbuka unapojiajiri moja kwa moja unaingia kwenye competetion. Consumers wa products zako hawajui wala hawahitaji kujua kwamba wewe ni fresh from school. All they need is better stuffs. Lakini pia kuna kitu kinaitwa corporate culture, unatakiwa uwe na uelewa na uzoefu wa namna gani makampuni yanaoperate. Hili ndiyo tatizo kubwa walilonalo wafanyakazi karibu wote wa serikali duniani.

3. Mtaji - Hii inaweza kuwa ndiyo centre ya tatizo, Unahitaji kuwa na reliable equipment, magari, wasaidizi etc. Wewe mwenyewe unahitaji kuwa mentally and physically fit. Kumbuka unapotoka shule huna pa kulala, nauli, kula kwenyewe sometimes ni ishu. Kwa mazingira yale ya kibongo ni graduates wangapi wanweza ku-afford just to buy a $500 laptop? Sasa basi kwa shuhuli mfano za kihandisi ambazo nna uzoefu nazo, the amount of money needed is ernomous, na on top of that kuna regulations zinazokulazimisha to spend even more.

4. Networking - You need to know people and them need to know you kishughuli, kwa Tanzania hii iko even worse kwa sababu you may sometimes be required to be networked with politicians. The idea of networking kwenye mazingira ya kifisadi na kukosekana maadili is always ill-mannered.

Anywayz kifupi ni kwamba, the idea of self employment is the best lakini is much easier ukiajiriwa kwanza say for some five years. Utapapata almost yote niliyoyaelezea hapo juu tena bure. You will build understanding and confidence in your carrier. Attend paid for by the company trainings, workshops, seminars etc. You will easily learn simple stuff such as how to deal with your subordinates, boss, secretary. How to present issues, ideas for implentation etc. In fact you will be doing things that sometimes would have been a disaster to give a try if the $$ were from your pocket.

Hivyo basi kwa nchi yetu bado serikali ina wajibu wa kutengeneza sera nzuri kama vile kuwekeza kwenye nishati, maji, utalii etc. Serikali inahitaji kuondoa ukiritimba, rushwa But the idea kwamba say graduates laki tano wamwagike mtaani of which 90% will be in Dar wajiajiri profesionally is just a pie in the sky.

Nakubaliana kabisa na unayoyasema. Kipindi cha miaka mitano ijayo hadi 10 kama hakutakuwa na mabadiliko ya kweli nchini kwtu ili kupambana na hii hali ya kutisha kuhusu ukosefu wa ajira basi kutakuwa na mlipuko wa kutisha ambao unaweza kusababisha maafa makubwa sana.

Hawa wanaojiita Viongozi tangu wagundue neno "kujiajiri" basi wanalitumia kirahisi rahisi mno kila pale kunapokuwa na malalamiko ya ukosefu wa ajira kwa wasomi wanaomaliza katika vyuo mbali mbali nchini. Utawasikia wakiwaambia wasomi hao, "Msitegeme kuajiriwa sasa hivi Serikali haina kazi ni lazima mjiajiri." Kujiajiri kunataka capital kubwa sana ambayo asilimia kubwa ya wasomi hawa hawana kwa kuwa wametoka katika familia za kimaskini ambazo haziwezi kuwasaidia watoto/ndugu zao pamoja na kuwa wangependa kufanya hivyo kama wangekuwa na uwezo.

Nchi yetu ina utajiri wa kutisha ambao tumerithishwa na Mungu lakini kutokana na kuwa mabazazi wanaoongoza nchi basi utajiri huo huwanufaisha wachache na wageni huku asilimia kubwa ya Watanzania wakiendelea kuishi katika maisha yenye dhiki iliyokithiri. Tanzanet yetu ambayo haipatikani nchi nyingine yeyote ile duniani ianingiza mabilioni ya dollars kule RSA, USA, Kenya na hata India lakini Watanzania tunaambulia kiduchu. Dhahabu yetu inachimbwa kwa mwaka wa 10 sasa na kama sikosei Tanzania ni nchi ya tatu au nne katika uzalishaji wa dhahabu duniani lakini tunaambulia 3% na 97% inapelekwa nje ya nchi. Fikiria kama tungekuwa tunapata 50% ya mapato ya dhahabu yetu na asilimia kubwa ya mapato ya Tanzanet katika nchi za US, RSA, Kenya na India yangekuwa yanaingia nchini na hivyo kuongeza pato la Taifa kwa kiwango cha juu sana na hivyo kuweza kupambana na hili tatizo la ukosefu wa ajira kwa wasomi wetu.

Tunaambiwa nchi yetu ina Wananchi 40 millioni lakini wanaolipa kodi kila mwaka hawafiki hata laki 7, lakini husikii mikakati yoyote toka kwa hao walioshika madaraka ili kuongeza idadi ya walipa kodi. Kuhusu Tanzanet na dhahabu yetu kuzinufaisha nchi nyingine pamoja na vilio vya Watanzania ili kubadilisha hali hii lakini hakuna mikakati yoyote ile ya kuhakikisha rasilimali zetu zinatumika katika kuinua viwango vya maisha ya Watanzania ikiwemo upatikanaji kirahisi wa ajira kwa wasomi wetu katika nyanja mbali mbali walizosomea.

Na bado hawa wanaojiita Viongozi wanaweza kupanda majukwaani bila hata aibu wakatoa hotuba zao kwamba nchi yetu ni maskini, kauli ambayo haina ukweli wowote, na kupita huku na kule na vibakuli vyao vya omba omba. Watanzania wengi wamekata tamaa ya maisha, na kwa maoni yangu halii hii inachangiwa sana na watu wazembe ambao hawakustahili kabisa kupewa madaraka ya aina yoyote ile. Huwa tayari kushika vitabu vya dini wanapoapishwa na kudai kwamba watalinda na kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania lakini wakishaapishwa basi ahadi zao zote huzisahau na kuwa na kiburi cha hali ya juu huku Watanzania wengi wakiendelea kutaabika miaka nenda miaka rudi.

Kama ulivyosema mkuu nchi yetu inahitaji mabadiliko makubwa sana tena katika kipindi kifupi kijacho, vinginevyo mlipuko hauko mbali sana na hakuna wa kulaumiwa ila hao mabazazi ambao wameng'ang'ania madaraka pamoja na kuwa wameshindwa kufanya lolote lile la kuinua uchumi wa nchi na hivyo kuongeza ajira na vipato kwa Watanzania ili waweze kukidhi gharama za maisha yao ya kila siku.

Siyo fikra tegemezi kuitaka serikali yako iwezeshe kupatikana kazi. Marekani Obama hivi sasa anaendeshwa puta kwa sababu ya ajira, ajira, ajira.
Ni kazi ya serikali kuunda sera zitakazowezesha kupatikana kwa ajira.

Ni fikra tegemezi kuililia serikali ikupatie mtaji.

Kinachopendekezwa hapa ni idea ya serikali ku-spend eti kwa ajili ya ku-creat jobs, hili sio jambo sahihi na ndipo Obama pia alipochemka, na matokeo yake badala ya kupunguza tatizo la ajira ameliongeza, na hii itam-cost sana come 2012, na anastahili kupewa hukumu kwa hili. Sasa kwa Tanzania itakuwa ndio even worse, unaweza uka-imagine ile stimulas plan iliyotolewa na serikali i guess 2009 imeleta hasara kiasi gani kwa mlipa kodi wa Tanzania, unaweza uka-imagine zile Billion 21 za Kikwete kila mkoa zimeingiza hasara kiasi gani kwa mlipa kodi, hii sio njia sahihi ya kutengeneza ajira, ajira zinapaswa ziletwe na uongezo la production na sio vinginevyo.

Ajira zinategemea sana utengamaa wa sekta binafsi, na ili sekta hii iwe stable tunahitaji "Wazawa/Watanzania wenye elimu/maarifa/taarifa sahihi na udhubutu wa kuanzisha shughuli za kutengeneza pesa, na hapa ndipo tatizo letu kubwa lilipo, opportunity zipo za kutosha.

Serikali uwanja wake wa kusaidia utakuwa sio kuspend bali kuondoa urasimu usio wa lazima, kuondoa/kupunguza kodi zisizo support growth, na kwa serikali na umma kwa ujumla ku-support kampuni/huduma/bidhaa za ndani, na pia kwa serikali kutoingilia mipango ya wafanyabiashara/wakulima kwenye strategy zao za kutengeneza pesa unless kama wamevunja sheria, wapi atauza bidhaa/mazao yake ni suala lake binafsi kibiashara, halilihusu serikali, thats the way to go.

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa
na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.

Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,
kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu

Wakati wa chama chashika hatamu ndipo hali mbaya ya elimu, ajira na kuzolora kwa uchumi uliikumba nchi hii. Wakati huo , mkazo haukuwa kujenga uchumi, ila kujenga taifa lenye watu wenye siasa kali sana chama chenye nguvu za mungu. Hali ya Igunga na masiaha ya wanaigunga ni ushahidi wa kutosha .

wasomi kutoka, kivukoni na hombolo ndio wamemwagwa nchi nzima kuanzia wilayani mapa ngazi za mikoa. Wao wanachojua ni kuahamasisha maendeleo na sio nini cha kufanya ili kuleta maendeleo. Hawajui nini maana ya kutatua swala la ukosefu wa kazi wala kujenga miji bora.

sera zetu za siasa za nchi za nje nazo huchangia sana kutopata wawekelezaji wengi wa kutuletea ajira. Hili zana la kujifanya kuwa tunauwezo wa kuandika matusi katika nakala za magazetini kwa mataifa kama Marekani, Israel na Ulaya magharibi, hazitupeki kokote ila kuzidi kujikandamiza.

Hivi jiulize, kwa nini tuna ofisi ya ubalozi katika taifa masikini la misri na tusiwe na ofisi ya ubalozi katika taifa tajiri kama Israel? Misri anauwezo gani wa kuleta viwanda hapa nchini kutatua tatizo letu la ajira kuliko Israel? Ukosefu wa ajira ni swala la kuweka urafiki zaidi na tajiri kuliko masikini.

Ukiangalia dunia ilipofikishwa sasa chini ya NEW WORD ORDER conspiracy(kwa taarifa yenu kwenye 15[SUP]th[/SUP] meeting of COPENHAGEN kila nchi ili-sign kukubali kuundwa kwa WORLD GOVERNMENT). sasa ili ku-solve unemployment problem, raisi ajaye anatakiwa.......
1. VIONGOZI NDANI YA SERIKALI YAKE WAMUONE DICTATOR(hapa ndio sera nzuri zitaundwa na kusimamiwa kwa nidhamu/uadilifu wa hali ya juu).
2. WANANCHI WAWE WANAMUONA RAISI KAMA MKOMBOZI WAO.

You guyz in this forum have been crying for democracy but you don't know what it cost to achieve a democracy!!

Wakuu kujiajiri proffesionally siyo kitu rahisi for a fresh from school candidate but is possible. Ndiyo maana mnasikia wamarekani wakilalamika jobs jobs kila siku. Personally I have a very good experience towards kujiajiri, I am a living proof kuhusu success and difficulties kuelekea kujiajiri proffesionally. It is not as simple kama watu wengi wanavyofikiri au ku-portray. Anyways kuna mambo yafuatayo yanatakiwa yazingatiwe.

1. Ufahamu wa hiyo shughuli unayotaka kujiajiri nayo. Hakuna chuo kikuu duniani kinakufundisha say kuwa injinia wa kwenye cement, au karatasi, au chuma. Vinanvyofundishwa shule ni fundamentals na principles. Ukienda kwenye industry ndiyo unakutana na specific trainings.

2. Uzoefu wa shughuli unayotaka kufanya. Kumbuka unapojiajiri moja kwa moja unaingia kwenye competetion. Consumers wa products zako hawajui wala hawahitaji kujua kwamba wewe ni fresh from school. All they need is better stuffs. Lakini pia kuna kitu kinaitwa corporate culture, unatakiwa uwe na uelewa na uzoefu wa namna gani makampuni yanaoperate. Hili ndiyo tatizo kubwa walilonalo wafanyakazi karibu wote wa serikali duniani.

3. Mtaji - Hii inaweza kuwa ndiyo centre ya tatizo, Unahitaji kuwa na reliable equipment, magari, wasaidizi etc. Wewe mwenyewe unahitaji kuwa mentally and physically fit. Kumbuka unapotoka shule huna pa kulala, nauli, kula kwenyewe sometimes ni ishu. Kwa mazingira yale ya kibongo ni graduates wangapi wanweza ku-afford just to buy a $500 laptop? Sasa basi kwa shuhuli mfano za kihandisi ambazo nna uzoefu nazo, the amount of money needed is ernomous, na on top of that kuna regulations zinazokulazimisha to spend even more.

4. Networking - You need to know people and them need to know you kishughuli, kwa Tanzania hii iko even worse kwa sababu you may sometimes be required to be networked with politicians. The idea of networking kwenye mazingira ya kifisadi na kukosekana maadili is always ill-mannered.

Anywayz kifupi ni kwamba, the idea of self employment is the best lakini is much easier ukiajiriwa kwanza say for some five years. Utapapata almost yote niliyoyaelezea hapo juu tena bure. You will build understanding and confidence in your carrier. Attend paid for by the company trainings, workshops, seminars etc. You will easily learn simple stuff such as how to deal with your subordinates, boss, secretary. How to present issues, ideas for implentation etc. In fact you will be doing things that sometimes would have been a disaster to give a try if the $$ were from your pocket.

Hivyo basi kwa nchi yetu bado serikali ina wajibu wa kutengeneza sera nzuri kama vile kuwekeza kwenye nishati, maji, utalii etc. Serikali inahitaji kuondoa ukiritimba, rushwa But the idea kwamba say graduates laki tano wamwagike mtaani of which 90% will be in Dar wajiajiri profesionally is just a pie in the sky.

Nyambala you said all...Lakini tukumbuke kazi ya kuajiri ni ya serikali kokote kule na ajira ni moja ya haki za raia iwe private au government. Tatizo letu kubwa ni la kisera zaidi kuliko uhalisia wa neno kukosa ajira. Inawezekana vipi watu kukosa ajira kwenye nchi ambayo robo tau ya watu wake hawana makazi; Zaidi ya nusu hawana good clothing; zaidi ya nusu hawapati milo mitatu na asilimia 90 ya miji yote ni michafu alafu uje na nyimbo za kusema hakuna ajira?

Tatizo letu kubwa tunapoangalia suala la ajira tunaongea luga zinazofanana na nchi zilioendelea kwao kudai kuwa hakuna ajira linaweza ku hold water maana hizo shuguli zote hapo zinawatu na ambapo hakuna sehemu unaweza kupata sehemu ambayo unaweza kuipeleka population yao. Sisi tatizo letu ni la kisera zaidi kuliko la kukosa sehemu ya kuwaajiri watu wetu. Pia ufisadi umesababisha wanasiasa kutopenda ku create ajira kwani wakifanya hivyo tayari wana create competition kwenye bussiness zao ambazo wanazi protect kwa udi na uvumba ziendelee kuwa na monopoly ili wao waendelee kupata super profit. Tanzania hatujafika bado sehemu tukasema ajira ni challenge no I totally disagree!

Ni fikra tegemezi kuililia serikali ikupatie mtaji.

Kinachopendekezwa hapa ni idea ya serikali ku-spend eti kwa ajili ya ku-creat jobs, hili sio jambo sahihi na ndipo Obama pia alipochemka, na matokeo yake badala ya kupunguza tatizo la ajira ameliongeza, na hii itam-cost sana come 2012, na anastahili kupewa hukumu kwa hili. Sasa kwa Tanzania itakuwa ndio even worse, unaweza uka-imagine ile stimulas plan iliyotolewa na serikali i guess 2009 imeleta hasara kiasi gani kwa mlipa kodi wa Tanzania, unaweza uka-imagine zile Billion 21 za Kikwete kila mkoa zimeingiza hasara kiasi gani kwa mlipa kodi, hii sio njia sahihi ya kutengeneza ajira, ajira zinapaswa ziletwe na uongezo la production na sio vinginevyo.

Ajira zinategemea sana utengamaa wa sekta binafsi, na ili sekta hii iwe stable tunahitaji "Wazawa/Watanzania wenye elimu/maarifa/taarifa sahihi na udhubutu wa kuanzisha shughuli za kutengeneza pesa, na hapa ndipo tatizo letu kubwa lilipo, opportunity zipo za kutosha.

Serikali uwanja wake wa kusaidia utakuwa sio kuspend bali kuondoa urasimu usio wa lazima, kuondoa/kupunguza kodi zisizo support growth, na kwa serikali na umma kwa ujumla ku-support kampuni/huduma/bidhaa za ndani, na pia kwa serikali kutoingilia mipango ya wafanyabiashara/wakulima kwenye strategy zao za kutengeneza pesa unless kama wamevunja sheria, wapi atauza bidhaa/mazao yake ni suala lake binafsi kibiashara, halilihusu serikali, thats the way to go.

Kutengeneza ajira ni kazi ya serikali through sera na kazi ya raia ni kufanya kazi/ajira iliyotengenezwa kwa ujuzi wake wote...Mfano huwezi kusema M-famasia ajiajiri iwapo serikali haijatengeneza ajira yake hiyo kupitia sera ya kuwa kazi za kifamasia zote zifanywe na profesionals wa hiyo tasnia na kuwe na sheria zinazolinda hizo ajira so hapo utaona jinsi hao watakavyo respond kuzifanya hizo kazi through either public or government sectors na mifano mingine kibao...

Tusichanganye issues hakuna kokote duniani ajira inaweza kutengenezwa pasipo serikali kuweka sera sahihi zilizo tafitiwa kwamba zinaweza tengeneza ajira tena mpaka kiwango cha waajiriwa kinajulikana. Raia anaingia katika stage ya mwisho kabisa ya demand na suply lakini stages za mwanzo za Invention-inovation na hata practice ya hizo innovation ni ya serikali maana hapo price theory hai apply kabisa kwani resources zinazohitajika ni kubwa na ambazo haiwezekani kwa private/individuals ku-realize profit- Nyambala ameainisha hizo constraint zote naye ame learn through experience lakini zipo theory ambazo ziko tested zinazo ainisha ni jinsi gani private/individuals wasivyo weza ku-create ajira bila public/government support. Na ndiyo maana kukawepo serikali inayokusanya kodi na moja ya kazi za kodi ni ku-create ajira through policies na strategy zake.

Hizo ndo chagizo za maendeleo. Wewe unashangaa wakati USA leo unemployment imefika 9.1%

Naungana na wengine wengi kuwa ingawa serikali inawajibu wa kujenga mazingira na kuwezesha vijana kupata ajira ni fikra potofu kuidai serikali ikupe ajira. Na ndiyo maana Kikwete aliposema atzalisha ajira 1000 kila mwaka wengi tulimponda kwa maana tulifikiri ajira nikuandikwa kazi. Hatuona kuwa mapesa ya Kikwete yangetumiwa ilivyoopaswa kweli yangeweza kuzalisha ajira hata 2000 kwa mwaka. Fikiria vijana 1000 wangefaidika na kuanzisha bishara endelevu zikakakua na kuajiri mtu mmoja mmoja au kusaidia wazazi wao kwenye kilimo tungekuwa wapi? Kwa mawazo yangu finyo tungekuwa mbali sana kama nchi.

Tanzania imetoka kwenye mfumo wa uchumi ambao serikali ndiyo mzalishaji, msambazaji na mnunuzi na hivyo basi mtoa ajira mkuu. Mfumo wa uchumi tulioingia tangia miaka ya 95 ni ule ambao serikali inajitoa katika uzalishaji na inweka mazingira na uwezeshaji wa sekta binafsi ikijumlisha makampuni na watu binafsi kuzalisha, kusambaza na mengineyo. Serikali ina jiingiza tuu kwenye uzalishaji kwenye maeneo ambayo mitaji inayohitajika ni mikubwa sana kwa sekta binafsi ama mtu binafsi kuweza kuwa nayo ama risk ni kubwa mno. Na hii ingefanywa vizuri ni mfumo endelevu wa maendeleo. Kwa bahati mbaya mabadiliko haya hayakufanywa vizuri hivyo tunamfumo dumavu wa maendeleo ambapo serikali inafikiri sekta binafsi itafanya majukumu yake bila uwezeshaji wa serikali na hivyo kupanua uwigo wa ajira. Haitaweza kamwe! Kenya ni mfano mzuri wa mfumo mchanganyiko (mixed) ambako sekta binafsi (kwa mapana ya maana yake na siyo kwa maana ya kampuni binafsi) imeshika hatamu lakini serikali haijajitoa katika uwezeshaji na usimamiaji (regulatory role) kuhakikisha kila mmoja (ofscourse matabaka, ukabila bado ni changamoto kwao) anapata fursa sawa kushiriki . Pia serikali bado inawekeza kwenye maeneo fulani fulani. Kuanzia ngazi ya kijiji serikali ya Kenya imeweka mifuko/mifumo mbali mbali, na uwezeshaji mwingine elimu, extension services kwa mtu binafsi kuthubutu kujiajiri na kujituma. Elimu ya msingi, sekondari na ya vyuo vya Kenya imetengenezwa kumtayarisha mtu binafsi kujiajiri mashindano ya ubunifu na ujasiriamali hayaanzii chuo kikuuu au baada ya kumaliza chuo kikuu bali tangu shule ya msingi. Ushindani endelevu unazawadiwa tangu shule ya msingi. Vijana 7 was sekondari moja kenya walipata zawadi kwa kubuni mradi wa huduma za dhobi baada ya kuona eneo wanaloishi kuna mahitaji. Mtaji wao ulikuwa mikono yao, vipande vya sabuni vyao na kutumia elimu ya takwimu waliyoipata kujua watu wanahitaji huduma gani. Leo hii wamekuwa wameanzisha dry cleaning services na mpaka miaka miwili pato lao lilikuwa kubwa sana hadi kupata tuzo. Hawa ni vijana mabinti wa miaka 15 na 17 tuu! tuache kufanya shule zetu magodown ya kuksanya vipaji na hatuvipi changamoto kuwa wabunifu.

Mfumo wa kijamii usioruhusu utegemezi ni muhimu kuwawajibisha watu kutokuchagua kazi- Tanzania ni rahisi mtu kumaliza chuo kikuu na kukaa na kula bure kwa ndugu hadi kupata kazi ya kuandikwa na mtu mwingine hata kama ni miaka miwili. Mfumo wa kijamii wa Kenya hautoi nafasi hiyo. Kula yako ni kazi ya mikono yako hakuna ndugu hata awe tajiri atakupa nafasi ya kumtegemea hadi upate kuandikwa kazi yeye mwenyewe ataanza kwa kukutaka uoshe gari, vyombo na kukulipa au kama mchango kwa kupata malazi na chakula bure. Huwezi kufanya hivi Tanzania ni kinyume cha maadili, upendo na mshikamano! Hivi misingi ya kujitegemea tuliyojengewa na Mwalimu Nyerere imegeukaje kutufanya wategemezi wakubwa!

Dhamira ya Mkenya hata housegirl au houseboy ni kujiendeleza kielimu ili asiwe hapo ndiyo maana Marehemu mzee Kimani Ng'ang'a Maruge, 88, alikuwa mwanafunzi Mzee aliyejiandikisha kusoma shule ya msingi akiwa na miaka 88.

Utamaduni wa kujitolea kama njia endelevu ya kupata ujuzi na ajira-tofauti kubwa sana kati ya Kenya na Tanzania ni utayari wa graduates wa kenya kufanya kazi kwa kujitolea kama njia ya kupata ujuzi. Hapa kijana akimaliza chuo kikuu akikuomba ajishikize kupata ujuzi anataka mjadiliane mshahara! Kenya mara nyingine vijana wanalipa kupata nafasi ya kujifunza na kupata ujuzi kwako! Hapa kwetu tunabeba vyeti badala ya ujuzi tulionao. Tunataka tufanye kazi kidogo lakini tulipwe sana! Sasa utakuta mnakwenda kwenye interview na kijana wa kenya mwenye first degree lakini amefanya internship miaka miwili na wewe una masters hujawahi fanya kazi ila unakusanya vyteti yeye anakushinda kwababau anajua content ya kazi kwa vile ameifanya na wewe una vyeti ila hutaki kuchafuka mikono maana unavyeti vya masters na PhD! na kwa maan ahiyo ulipwe tuu hata kama uzalishaji wako ni duni!

Tubadili uelewa wetu wa ajira - ajira siyo kuandikwa kazi bali ni zaidi ya hiyo inayojumlisha kujiajiri, kuajiriwa na mazingira endelevu yanayowezesha watu warika zote kuthubutu kujiandika kazi. Pili tuisukume serikali iwezeshe na iwajibishe sekta binafsi kwa maana kampuni na watu binafsi iwe na misingi bora ya uajiri (mikataba, uwazi katika kuajiri kupunguza upendeleo kwa njia yeyote ukabila, jinsia, rangi etc).

Hivi ni maengineer wangapi wamewahi jitolea kijijini kwao kuhamasisha wanavijiji wajenge madaraja ya muda, nyumba za kutumia malighafi zinazopatikana vijijini kwao, au mbinu za kutatua matatizo yao? Miaka 7 iliyopita nilienda kijiji kimoja Kigoma nikamkuta kijana wa darasa la saba amebuni incubator ya kutotoa vifaranga vya kuku wa kienyeji kutumia mafuta ya taa. Pia alibuni njia ya kuvuna maji ya mvua. Miaka miwili iliyopita alinitafuta akaniambia alishauriwa na wataalamu wa Tanzania haitamsaidia sana maana ni vizuri ingekuwa ya umeme. Nikamuuliza ni waTanzania wangapi wanaumeme vijijini? mjanja mmoja Dar amechukua ubunifu wa huyu kijana bila kumacknowledge na sasa anatengeneza hizi mashine na kuuza nusu million or laki saba na sifa anapata yeye! kwa njia hii ndiyo maana hatufiki popote! Tuwe wabunivu na tutumie elimu yetu kuvumbua fursa zilizopo kwenye jamii zetu na kutatua matatizo ya jamii.

nakubaliana na wewe mkuu tena sana binafsi baada yakukaa na wajiri nimeshaona hakuna muajiri yeyote hapa tanzania anaweza akathamini professional yangu nimesha hamisha mawazo ya kutegemea hawa wajiri na kufikiri kufanya kazi za kwangu.

Ni kweli usemavyo fursa zipo nyingi sana hapa tanzania hasa za uhandisi nakukuabalia lakini kwa mfano ili upractise engineering tanzania lazima uwe registered na ili uwe register lazima uwe chini ya professional engineer atakaye kusimamia.

Huwezi kukurupa tu ukaanzisha engineering company ya civil/electrical ukitokea shule.
jingine ni kweli nchi yetu ina wasomi kiasi hicho cha kuwa waacha waanze kujiajiri wote? yaani wote mna graduate halafu mnajiajiri does it make sense hivi ata marekani ndio iko hivyo

Unaweza kukuta wizara husika hata haijui graduates wangapi wanaingia kwa soko la ajira na wangapi hawana kazi todate

Back
Top Bottom