Tanzania: Crisis kubwa inakuja

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,326
2,228
Miaka mitatu mijayo tutakuwa na crisis ya upungufu mkubwa wa ajira na
ongezeko kubwa la graduates mitaani kuliko kipindi chochote kile katika historia ya nchi yetu!

Ni changamoto nzuri kiuchumi lakini itatumaliza kisiasa.
Serikali iweke mkakati wa kuwajengea uwezo wa kujiajiri hii critical mass mapema kabla bomu hili halijailipua CCM 2015!

" says kigwangala."

Nionavyo mimi pia ni kweli kwamba hili ni janga jipya,...ni zuri kwa wapinzani
kwani litachangia kuiondoa ccm madarakani,lakini halita wasaidia wapinzani sana baada ya hapo
maana tatizo hilo hilo laweza kuwaondoa madarakani pia.

Ni vyema sasa serikali ikaangalia jinsi ya kuwawezesha wasomi ili wajiajiri wao wenyewe.
Kwa mfano:-

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa
na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.
Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,
kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu
 
WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
2,919
1,228
Mkuu Clemmy, serikali yetu bado inahitaji watendaji wasomi kuanzia ngazi ya chini mfano kata, tarafa, wilaya na mikoani hadi taifa. Achilia mbali na taasisi zilizojaa wastaafu wenye kuunga unga mikataba kwa kisingizio cha uzoefu bila kujenga capacity kwa waajiriwa wapya.

Wakiingia watu walio serious, watacreate job opportunities nyingi na watu wataona mapinduzi makubwa mno ya kiuchumi. Watendaji wengi wa serikali hawana elimu ya kutosha, hivyo ni sera tu ndo zinahitajika kumaliza tatizo la ajira kwa graduate.

Angalia kwa mfano: Mashule ya kata yasivyokuwa na walimu, serikali ikirekebisha mishahara kwa waalimu naimani wengi watagruate sehemu na kupiga course ya ualimu harafu wanafundisha watoto wetu.
 
sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
20
Ni kweli hilo janga si kwamba tu linakuja tayari tunalo, na cha kusikitisha ajira inategemea na mipango mizuri ya mda mrefu ya uchumi hivyo sio rahisi kukabiliana nalo kirahisi hivyo tena ukizingatia upeo wa viongozi wetu tulionao wanaojua kusema na sio kutenda.

Pia mimi na wewe tuanze kwa kuwa wazalendo tukawa tunatumia bidhaa za hapa kwetu itapelekea kuongeza ajira kwani viwanda vitalazimika kuzalisha zaidi hivyo nguvu kazi itahitajika kwa wingi, hivyo hivyo kwa shughuli zinazohusiana na usambazaji zitakuwa na kuweza kuajiri watu wengi zaidi.Kwa njia hiyo hata kodi itaongezeka kwa maana itokanayo na wafanyakazi na ya mapato ambayo makampuni yatalipa.
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,826
8,642
Clemmy, hilo si janga jipya... lina miaka minne au mitano sasa

Yote ni matokeo ya siasa uchwara na focus ya serikali iliyo madarakani kubaki madarakani badala ya kuendeleza watu wake

to be honest, ni ile myopia ya wanasiasa wa leo wa CCM (as opposed to enzi za mwalimu) kuangalia zaidi 5 years, if i were a CCM leader i would easily focus on 20 years to come... lose one term and trust me wapinzani bado hawako tayari kuchukua nchi 10 continuously coz upinzani wetu upo disadvantaged na mfumo mzima wanchi

then recoup and have sustainable plans.... being outside the game at least for one term would benefit CCM kuliko upuuzi tunaouona sasa wa mabilioni tukumika kwa jimbo lenye literacy score ndogo, and poor on almost everything

anyway ni mawazo yangu.... this is not a new problem, kama hamis anavyotaka tuamini
 
Tuntu

JF-Expert Member
Jan 28, 2009
211
23
Ni vyema sasa serikali ikaangalia jinsi ya kuwawezesha wasomi ili wajiajiri wao wenyewe.
Kwa mfano:-

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa
na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.
Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,
kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu

Miaka 26 baada ya ujamaa kuzikwa hapa nchini bado kuna tuna fikra tegemezi sana, bado wananchi ata wale waliobahati kupata elimu nzuri wanategemea eti serikali iwalishe chakula mdomoni, fikra potofu sana hizi.

Serikali imefanya wajibu wake kwa kuhakikisha hao "unaowaita wasomi" wamepata elimu yao, . Tunatarajia kuwa mtu mwenye elimu ya "chuo kikuu" awe na uwezo wa kuyasoma vizuri mazingira yake, kuangalia matatizo yaliyopo, na kuyatafutia ufumbuzi kwa faida yake binafsi na taifa kwa ujumla. hivyo ni wajibu wa hao wasomi wenyewe, kupitia elimu zao ambazo zinapaswa ziambatane na ujuzi, maarifa na fikra sahihi kuweza kuanzisha shughuli za uzalishaji mali na kuwaajiri wengine ambao hawakupata fursa za "elimu".

Naamini kama wameelimika vizuri, kama elimu imewawezesha kuyajua mazingira yaliyopo vizuri, basi watakuwa na uwezo wa kuzitumia fursa zilizopo kujikomboa kiuchumi, la kama hawawezi basi tatizo lao kubwa "lipo kwenye fikra zao" wenyewe na hivyo ata kama serikali ingewapa mitaji, mitaji hiyo haitawasidia lolote na mwisho wa siku itakuwa ni matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi wengine.

Naamini msaada wa serikali katika hili unaweza ukawa tu kwenye kuwaunga mkono wale "walioweza kufikiri na kuanzisha "shughuli zao" kwa kutoa upendeleo maalumu kwa kampuni za ndani kwenye baadhi ya kazi/huduma full-stop.

Jamani muda wa kuisubiri serikali ikuletee chakula mezani umepita, ebu tutambue kuwa "Ujamaa Umekufa Na Hautarudi Tena", ebu tubadilike kifikra na tuitumie elimu tuliyoipata kujikomboa wenyewe, nchii hii bado ni "bikira" kwa kiwango kikubwa na hii ni fursa kwa "msomi aliyeelimika", unachopaswa kufanya ni kufungua tu macho yako na kufikiri kwa bidii sana.
 
mpuuzi

Member
May 29, 2010
99
17
say kigwangala.

Nionavyo mimi pia ni kweli kwamba hili ni janga jipya,...ni zuri kwa wapinzani
kwani litachangia kuiondoa ccm madarakani,lakini halita wasaidia wapinzani sana baada ya hapo
maana tatizo hilo hilo laweza kuwaondoa madarakani pia.

Ni vyema sasa serikali ikaangalia jinsi ya kuwawezesha wasomi ili wajiajiri wao wenyewe.
Kwa mfano:-

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa
na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.
Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,
kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu

kweli mkuu, nilikuwa na demu mmoja alimaliza SUA sijui ndo Agricultural Engineering, sasa hivi ni afisa mikopo PRIDE
 
Maganga Mkweli

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
2,090
826
say kigwangala.

Nionavyo mimi pia ni kweli kwamba hili ni janga jipya,...ni zuri kwa wapinzani
kwani litachangia kuiondoa ccm madarakani,lakini halita wasaidia wapinzani sana baada ya hapo
maana tatizo hilo hilo laweza kuwaondoa madarakani pia.

Ni vyema sasa serikali ikaangalia jinsi ya kuwawezesha wasomi ili wajiajiri wao wenyewe.
Kwa mfano:-

UDSM,DIT,ARIDHI etc wana hitimu ma-injinia kila mwaka,lakini wote huenda kutafuta ajira kwenye makampuni makubwa
na huko huwa watumishi wa kawaida tu,na possibly wengi husahau hata profession zao.
Serikali ingetoa fungu kwa Mainjinia kama hawa,then waka kabidhiwa bara bara kwa mfano ili waisimamie,
kwanza wangepata experience na tungetengeneza wataalamu kweli kweli sio wataalamu wa nadharia tu
mkuu hii TIME BOMB honestly inaniuma sana nikiona nchi hii isivyo thamini wasomi hasa WAHANDISI where i belong ,hivi kweli mnataka kuendelea bila wahandisi jamani inaumiza sana wanatusisitiza tusome masomo ya sayansi halafu unaingia pale UHANDISI /FOE/COET unakaa miaka minne unatoka unaanza kuhaha mtaan,i the same time serikali inasema inaupungufu wa watalaamu kweli hii ni akili ?
hivi nchi yenye watu 40M+ wenye degree wanaweza wakafika laki moja kweli ? kama hawafiki kuna utaratibu gani wakuwatumia hawa wasomi wachache waliopo
nina ushuhuda miaka ya karibuni ambayo na mimi ni moja ya magraduate yaani ukimaliza tu hata uwe nani labda daktari tu, vinginevyo lazima upige bench mtaani unless mzazi wako ana kampuni au unafahamiana na fulani ndio ukitoka chuo tu unapata kazi . tunakubali elimu yetu ina mapunguzu sana hasa kwenye kumuundaa mtu kujiajiri lakini hivi kila mtu akijiari kutakuwa na public servant kweli?
 
Tuntu

JF-Expert Member
Jan 28, 2009
211
23
Pia mimi na wewe tuanze kwa kuwa wazalendo tukawa tunatumia bidhaa za hapa kwetu itapelekea kuongeza ajira kwani viwanda vitalazimika kuzalisha zaidi hivyo nguvu kazi itahitajika kwa wingi,hivyo hivyo kwa shughuli zinazohusiana na usambazaji zitakuwa na kuweza kuajiri watu wengi zaidi.Kwa njia hiyo hata kodi itaongezeka kwa maana itokanayo na wafanyakazi na ya mapato ambayo makampuni yatalipa.

Nakubaliana sana na wewe katika hili.
 
kikahe

JF-Expert Member
May 23, 2009
1,350
280
Taaluma haizingatiwi tena siku hizi. Engineers na Doctors wanakuwa politicians, bankers etc
 
Tuntu

JF-Expert Member
Jan 28, 2009
211
23
mkuu hii TIME BOMB honestly inaniuma sana nikiona nchi hii isivyo thamini wasomi hasa WAHANDISI where i belong ,hivi kweli mnataka kuendelea bila wahandisi jamani inaumiza sana wanatusisitiza tusome masomo ya sayansi halafu unaingia pale UHANDISI /FOE/COET unakaa miaka minne unatoka unaanza kuhaha mtaan,i the same time serikali inasema inaupungufu wa watalaamu kweli hii ni akili ?
hivi nchi yenye watu 40M+ wenye degree wanaweza wakafika laki moja kweli ? kama hawafiki kuna utaratibu gani wakuwatumia hawa wasomi wachache waliopo
nina ushuhuda miaka ya karibuni ambayo na mimi ni moja ya magraduate yaani ukimaliza tu hata uwe nani labda daktari tu, vinginevyo lazima upige bench mtaani unless mzazi wako ana kampuni au unafahamiana na fulani ndio ukitoka chuo tu unapata kazi . tunakubali elimu yetu ina mapunguzu sana hasa kwenye kumuundaa mtu kujiajiri lakini hivi kila mtu akijiari kutakuwa na public servant kweli?

Ndugu yangu, katika hili tatizo lipo kwako mwenyewe na wala sio serikali.

Kuna vijaa kadhaa waliotoka hapo hapo FOE, na tena wametoka kwenye familia duni sana, kwa mfano hawa (http://www.sihebs.co.tz/solutions.html), lakini wamejitahidi kutumia fursa ya elimu, ujuzi na maarifa walioupata kujitafutia shughuli zao, mie binafsi nimewahi kutumia huduma zao na zilinifurahisha sanaa, na bado kuna matatizo chungu nzima katika nchi hii yanayohitaji "engineering solutions", msaada wa serikali na umma kwa ujumla unaweza ukawa tu kwenye kuwaunga mkono "vijana wanaojiajili" kwa kuacha kasumba tu ya kupenda vya nje na kuanza kutumia huduma na bidhaa za ndani.

Nakushauri tu usikate tamaa,na usijlimit tu kwenye kuajiriwa, anza sasa kutafuta solutions utakazotoa wewe kwenye matatizo yanayoikabili nchi yako, na mwisho wa shimo solution zako hizo zitakuwa ajira yako na za Watanzania wenzako.
 
Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,326
2,228
Ni kweli hilo janga si kwamba tu linakuja tayari tunalo, na cha kusikitisha ajira inategemea na mipango mizuri ya mda mrefu ya uchumi hivyo sio rahisi kukabiliana nalo kirahisi hivyo tena ukizingatia upeo wa viongozi wetu tulionao wanaojua kusema na sio kutenda.Pia mimi na wewe tuanze kwa kuwa wazalendo tukawa tunatumia bidhaa za hapa kwetu itapelekea kuongeza ajira kwani viwanda vitalazimika kuzalisha zaidi hivyo nguvu kazi itahitajika kwa wingi,hivyo hivyo kwa shughuli zinazohusiana na usambazaji zitakuwa na kuweza kuajiri watu wengi zaidi.Kwa njia hiyo hata kodi itaongezeka kwa maana itokanayo na wafanyakazi na ya mapato ambayo makampuni yatalipa.

Mkuu ulivosema kuhusu kununua bidhaa za Tanzania duh,yataka moyo kweli.
Juzi hapa nilisikia Bakhresa (sijui spelling zake) katoa malta yake,basi nikasema ngoja
niionje nione malta za kitanzania zilivo,...mh,nilikunywa funda moja nikaimwaga.

Ina sukari balaa,na ndizo bidhaa za kitanzania zilivo,hazi thibitishwi ubora wake na madhara yake pia
ila wanacho angalia ni kutoa vitu sokoni tu.
Nani anataka kufa kwa kisukari mapema au magonjwa ya moyo?
Watoto wana fakamia kweli hayo ma malta,ni wangapi watapona?

Ni kweli lazima tuwe wazalendo na kununua bidhaa za tanzania,lakini
katika uzalendo huo tuna haki ya kulinda afya zetu.
Hadi sasa sina imani na bidhaa za kitanzania,honestly.
 
Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,326
2,228
Clemmy, hilo si janga jipya... lina miaka minne au mitano sasa

Yote ni matokeo ya siasa uchwara na focus ya serikali iliyo madarakani kubaki madarakani badala ya kuendeleza watu wake

to be honest, ni ile myopia ya wanasiasa wa leo wa CCM (as opposed to enzi za mwalimu) kuangalia zaidi 5 years, if i were a CCM leader i would easily focus on 20 years to come... lose one term and trust me wapinzani bado hawako tayari kuchukua nchi 10 continuously coz upinzani wetu upo disadvantaged na mfumo mzima wanchi

then recoup and have sustainable plans.... being outside the game at least for one term would benefit CCM kuliko upuuzi tunaouona sasa wa mabilioni tukumika kwa jimbo lenye literacy score ndogo, and poor on almost everything

anyway ni mawazo yangu.... this is not a new problem, kama hamis anavyotaka tuamini

Ni kweli mkuu,
sio janga jipya,lakini ni kama kansa,inakua kwa kasi sana.
Kila mwaka vijana wanajaa vyuoni,na ukiangalia idadi ya walio ingia toka
mwaka 2009 hadi sasa,then hesabu miaka mitatu toka 2011,...ikifika 2014 au 2015 lazima
tuta shuhudia maandamano makubwa na labda vurugu za watu kukosa ajira.

Kuna mtu namfahamu kamaliza mwaka jana,mpaka leo hana kazi na kachoka kweli kama
hana degree vile.Hawa wakijaa wakawa 5,000 au zaidi,wata isumbua nchi kweli.

Kama ulivo sema,viongozi wetu wana focus chaguzi tu (miaka mitano watasema nini kimefanyika).
Hawa focus katika miaka 20 au zaidi,...na hata kinacho kuwa focused 20years later kinakuja fanywa
miaka mi5 kabla ya deadline kufika (tunaita wanazima moto).

Sioni tofauti kwa wapinzani,ndo maana nikasema janga hili linaweza iondoa ccm madarakani.
Lakini litaondoa chama chochote kitakacho ingia madarakani mapema kuliko inavo tarajiwa.
 
mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,569
185
Hakuna wa kulizuia maana haliko huko tu anza na vijana wanaomaliza shule za Msingi halafu wanakosa pa kwenda, Shule za Kata sory za Sekondari hakuna pa kwenda, Sekondari za juu Hakuna pakwenda halafu graduates, Maana yake wote wanao anza drasa la kwanza mwisho wao ni kufika chuo kikuu lakini labda 2% ndio wanapata cha kufanya hilo bomb limesha washa yellow light
 
Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,326
2,228
Taaluma haizingatiwi tena siku hizi. Engineers na Doctors wanakuwa politicians, bankers etc

Mimi nilikua naamini kwamba madaktari na mainjinia wanao
kimbilia kwenye siasa ni wale "walio shindwa kutumia taaluma yao,au hawajui chochote kuhusu taaluma zao
ndo maana wanaficha udhaifu wao katika siasa".
 
Maganga Mkweli

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
2,090
826
Ndugu yangu, katika hili tatizo lipo kwako mwenyewe na wala sio serikali.

Kuna vijaa kadhaa waliotoka hapo hapo FOE, na tena wametoka kwenye familia duni sana, kwa mfano hawa (Sihebs Technologies :: Our Solutions), lakini wamejitahidi kutumia fursa ya elimu, ujuzi na maarifa walioupata kujitafutia shughuli zao, mie binafsi nimewahi kutumia huduma zao na zilinifurahisha sanaa, na bado kuna matatizo chungu nzima katika nchi hii yanayohitaji "engineering solutions", msaada wa serikali na umma kwa ujumla unaweza ukawa tu kwenye kuwaunga mkono "vijana wanaojiajili" kwa kuacha kasumba tu ya kupenda vya nje na kuanza kutumia huduma na bidhaa za ndani.

Nakushauri tu usikate tamaa,na usijlimit tu kwenye kuajiriwa, anza sasa kutafuta solutions utakazotoa wewe kwenye matatizo yanayoikabili nchi yako, na mwisho wa shimo solution zako hizo zitakuwa ajira yako na za Watanzania wenzako.

nakubaliana na wewe mkuu tena sana binafsi baada yakukaa na wajiri nimeshaona hakuna muajiri yeyote hapa tanzania anaweza akathamini professional yangu nimesha hamisha mawazo ya kutegemea hawa wajiri na kufikiri kufanya kazi za kwangu.

Ni kweli usemavyo fursa zipo nyingi sana hapa tanzania hasa za uhandisi nakukuabalia lakini kwa mfano ili upractise engineering tanzania lazima uwe registered na ili uwe register lazima uwe chini ya professional engineer atakaye kusimamia.

Huwezi kukurupa tu ukaanzisha engineering company ya civil/electrical ukitokea shule.
jingine ni kweli nchi yetu ina wasomi kiasi hicho cha kuwa waacha waanze kujiajiri wote? yaani wote mna graduate halafu mnajiajiri does it make sense hivi ata marekani ndio iko hivyo
 
String Theorist

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
203
176
Kwa jinsi mfumo wetu ulivyo,mtu akiwa anafaulu vizuri mitahani yake tuu... HUANZA KUFIKIRIA KUAJIRIWA/kutumika. Badala ya kutumia hiyo akili kubuni kitu kipya kitacho mfanya ajiajiri.

Huwa nasikitika sana kuona mtu analalamika eti hana ajira, na mda huo huo ukimpa hata laki tano hujui aanzie wapi kuitumia/kuizungusha. Hii ni kwasababu tukiwa mashuleni badala ya kuelimishwa... tunaimbishwa/mezeshwa. Hasara ya hii ni kuwa na akiri tegemezi(baba anaziita "AKILI ZA CHANJO"). MFANO MZURI NI WEWE MWENYEWE HAPO ULIPO UNAITUMIAJE HIYO INTERNETR CONNECTION TO MAKE MAXIMUM AMOUNT OF MONEY?.

BY Tuntu
nchii hii bado ni "bikira" kwa kiwango kikubwa na hii ni fursa kwa "msomi aliyeelimika",
Watanzania wangapi wanajitahidi kujineemesha na huu "u-bikra" wa taifa letu legaly?...

Asilimia kubwa ya watanzania tunaamini kuwa "UKITAKA UENDELEE, LAZIMA UWE NA MTAJI/PESA". Sasa hapa ndio mwanzo wa anguko letu. wengi tunafikia conlussion kwamba... "ILI UPATE MTAJI, SHARTI UAJILIWE KWAZNZA" ...Tunasahau kwamba mishara mingi tunayo ripwa, huishia kutulisha tuu.. na sii vinginevyo. BWT Nyerere aliliona hili(SOMA AZIMIO LA ARUSHA)

SWALI.. Hivi tangu SUA ianze, kuna mtu yeyote aliyesoma pale, na leo anafahamika kama mkulima mkubwa hapa tanzania?. LAILA ODINGA ALISHA WAHI KUSEMA KUWA HUWA ANASHANGAA SANA KUONA MTU ANA DEGREE YAKE,HARAFU ANATEMBEZA VYETI MAOFINI. elimu hapa inakua useless....

"USHINDANI NI KIWANDA CHA UBINUFU"= G NAKO. kwa hili taifa letu ushindani kwenye mambo ya maendeleo haupo,na badala yake tuaendeleza upinzani kwenye maendeleo(sio wa kisiasa). JANGA LA KITAIFA HILI.. Hivi tanzania mpaka sasa inashindana na nchi gani kimaendeleo?. mimi mpaka sasa sijui, zaidi ya kusikia viongozi wetu wakijilinganisha ubora na nchi kama somalia.

SERIKALI kwa sasa inahitaji kutu kimoja "propaganda" zitazo saidia kutubadilisha mawazo ya kusoma ili kuajiriwa,hadi kusoma ili kujiajiri. the people must be able to think out of the box!!. NOTE: "PROPAGANDA BILA SERA ZINAZOTEKEREZEKA=KUWAHADAA/KUWATUKANA WANANCHI"

Serikari ijayo itabidi ijitahidi sana KU-EMPOWER VETA ili vijana wanaotoka hapo, wawe working machine wa taifa letu(hawa wa veta wengi wao wataajiriwa na wale wenye degree waliofanikiwa kujiajiri).

SWALI: ni watu wangapi hapa dunia walio AJIRIWA leo hii tunawafamu kama matajiri wakubwa???.
 
Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,066
173
Bado darasa la saba - shule za kata - wako km 2million. Come 2015 watakua wanauliza CCM, nilikua naongoza darasa la kwanza hadi la saba / form one - form four ila mtihani wa mwisho nimepata Div Four au zero..... Ni janga, sioni kama CCM wanaliona, japo ndio ticket ya kuwaondoa 2015.
 
dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,725
252
Dumping area ni shule za kata. Hawa hawatakuwa wakata bali watukutu huko tuendako. Mfano ni Igunga.
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,974
1,640
Miaka 26 baada ya ujamaa kuzikwa hapa nchini bado kuna tuna fikra tegemezi sana, bado wananchi ata wale waliobahati kupata elimu nzuri wanategemea eti serikali iwalishe chakula mdomoni, fikra potofu sana hizi.

Serikali imefanya wajibu wake kwa kuhakikisha hao "unaowaita wasomi" wamepata elimu yao, . Tunatarajia kuwa mtu mwenye elimu ya "chuo kikuu" awe na uwezo wa kuyasoma vizuri mazingira yake, kuangalia matatizo yaliyopo, na kuyatafutia ufumbuzi kwa faida yake binafsi na taifa kwa ujumla. hivyo ni wajibu wa hao wasomi wenyewe, kupitia elimu zao ambazo zinapaswa ziambatane na ujuzi, maarifa na fikra sahihi kuweza kuanzisha shughuli za uzalishaji mali na kuwaajiri wengine ambao hawakupata fursa za "elimu".

Naamini kama wameelimika vizuri, kama elimu imewawezesha kuyajua mazingira yaliyopo vizuri, basi watakuwa na uwezo wa kuzitumia fursa zilizopo kujikomboa kiuchumi, la kama hawawezi basi tatizo lao kubwa "lipo kwenye fikra zao" wenyewe na hivyo ata kama serikali ingewapa mitaji, mitaji hiyo haitawasidia lolote na mwisho wa siku itakuwa ni matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi wengine.

Naamini msaada wa serikali katika hili unaweza ukawa tu kwenye kuwaunga mkono wale "walioweza kufikiri na kuanzisha "shughuli zao" kwa kutoa upendeleo maalumu kwa kampuni za ndani kwenye baadhi ya kazi/huduma full-stop.

Jamani muda wa kuisubiri serikali ikuletee chakula mezani umepita, ebu tutambue kuwa "Ujamaa Umekufa Na Hautarudi Tena", ebu tubadilike kifikra na tuitumie elimu tuliyoipata kujikomboa wenyewe, nchii hii bado ni "bikira" kwa kiwango kikubwa na hii ni fursa kwa "msomi aliyeelimika", unachopaswa kufanya ni kufungua tu macho yako na kufikiri kwa bidii sana.

Hapo kwenye bold and red: Tungekuwa tunalazimishwa kufikiri ningesema sawa, ila mhhhhhhhhhhhh!
 
12 Reactions
Reply
Top Bottom