Yaani tuondokane na mawazo mgando kuwa ili reli zetu zifanye kazi lazima ziunganishwe na nchi jirani!!! nchi yetu ni kubwa sana tunaweza kuendesha wenyewe..kwa faida zetu za kiuchumi..watu bado mnalalamika tu wakati hatua za kurekebisha kasoro zinachukuliwa kama hiyo ya ku-split tzr kama ni kweli badala ya kuongelea the best way ya kuitumia hiyo reli mijitu inalalamikia nchi za jirani au mnalipwa!!!usafiri wa kusini nyanda za juu unaweza ukaimarika sana pengine ukachukua muda mfupi zaidi kufika mbeya na mikoa mingine kama tzr itawekezwa ndani ya TZ nakubakiza kipande cha zambia kwa matumizi yao kama watahitaji!!!Nilikuwa ninajaribu kuwaza kwa sauti tu mkuu. Maana hats migodi hatuna share an jirani lakini haitusaidii. Tuna teli ya Kati nayo haitusaidii, nayo ndiyo tena. Hatuna mfano was kuonyesha kuwa tuki stand Aline Luna tuwezacho.
What if Zambia nao wakiamua kujenga reli kuelekea Mozambique?
Ninasema kuwa ninawaza kwa sauti kwa kuwa ninaamini sina uelewa mzuri juu ya saga hii, lakini kadili mjadala unavyoendelea nina hakika kuna vitu Nita catch up, pia kauli ya waziri no muhimu.
Yaani tuondokane na mawazo mgando kuwa ili reli zetu zifanye kazi lazima ziunganishwe na nchi jirani!!! nchi yetu ni kubwa sana tunaweza kuendesha wenyewe..kwa faida zetu za kiuchumi..watu bado mnalalamika tu wakati hatua za kurekebisha kasoro zinachukuliwa kama hiyo ya ku-split tzr kama ni kweli badala ya kuongelea the best way ya kuitumia hiyo reli mijitu inalalamikia nchi za jirani au mnalipwa!!!usafiri wa kusini nyanda za juu unaweza ukaimarika sana pengine ukachukua muda mfupi zaidi kufika mbeya na mikoa mingine kama tzr itawekezwa ndani ya TZ nakubakiza kipande cha zambia kwa matumizi yao kama watahitaji!!!
Usichanganye mambo!!! kama huelewi kitu ni bora kukifuatilia au kuomba mwenye taarifa rasmi ya huo mpango mzima amwage data hapa ili tujue, pengine ni kwa manufaa ya TZ.Tazara kama ilivyo kwa sasa haina faida yeyote na wawekezaji hawawezi kuingia kitu ambacho kimeganda kama barafu...yaani Dar to Kapirimposhi only..Tanzania inaweza kunufaika kama TZR itakuwa diversified. Pengine wenzetu bado hawako tayari kwa mfano kuweka express train from Dar to Mbeya ambayo itaongeza uzalishaji kwenye mikoa ya kusini..sasa kama Zambia hawataki kuwekeza zaidi tufanyeje..???
Mi naunga mkono hoja and is the step towards the right direction..Nyie watu wa kaskazini kazi yenu kupinga kila kitu..mpaka mkataba afanye Mtei na Mbowe ndo mnaona wa akili...
Mkuu......inawezekana sisi tukawa wajinga sana lakini.....tufike mahali hawa majirani zetu.... should not take us for a ride...! to hell na huo ujirani ambao hauna mutual benefit......yaani tusifanye mambo yetu kisa lazima tum-consult jirani.....yaani tusifanye safri za ndani mpaka tuwa-consult Zambia!!.....
Mkuu Ogah kwanza nianze kuunga mkono bandiko lako hakika wengi wetu humu hatujui kwanini Tanzania inachukua msimamo wa kila nchi kuendesha TAZARA kivyake.
Kwa muda mrefu sana kumekuwa na urasimu usio na faida hasa toka upande wa Zambia linapokuja suala la uendeshaji wa TAZARA.Sheria na taratibu za uendeshaji TAZARA ni lazima mtendaji mkuu atoke Zambia na msaidizi ndio atoke Tanzania hii imesababisha TAZARA kuendeshwa kwa matakwa ya Zambia.Mfano Tanzania ilitaka kutumia miundombinu ya TAZARA kwaajili ya usafiri wa Dar Zambia wakagoma,Tanzania ilitaka kuongeza safari za treni za ndani kuanzia Dar hadi Mbeya baada ya route hiyo kubainika itaongeza faida maradufu Zambia ikakataa.Masuala ya fedha lazima yapate baraka toka Zambia matokeo yake unakuta fedha nyingi za TAZARA zimerundikana katika account za TAZARA Zambia na kusababisha uzorotaji wa utoaji wa huduma pasipo sababu za msingi.
Muundo wa sasa wa TAZARA umepitwa na wakati kwakuwa ulijikita zaidi katika masuala ya siasa badala ya biashara.Naungana na Dr Mwakyembe katika kuligawa shirika hili ili kuongeza ufanisi zaidi.
While the West is uniting, Tanzania is busy splitting from her neighbors. One day, you will regret Tanzania. You can not stand by yourself.
Upumbavu zaidi ni kuilalamikia Zambia wakati TZ ndiyo iliyoshika mpini. Fursa zote za kuiburuza Zambia katika TAZARA zipo, na ni za asili. Tatizo ni kukosa mawazo yenye muelekeo huo. Wakulima wana msemo kuwa ''mtu mvivu hatawahi shambani alfajiri na mapema akisingizia uwepo wa wanyama wakali njiani" Uvivu tu kuanzia kufikiri hadi kutenda!
Show me one nation which did stand on her own?Are you sure we cant stand on our selves?
Mkuu, watu wapumba.vu hawati kuona ukweli ulio dhahiri. Huu muundo wa Tazara umekuwa mwiba kwa Tz. Mfano mdogo ni usafiri wa mjini wa treni aka treni ya Mwakyembe. Wazambia wanapinga hata hilo.
Reli ilijengwa kimsingi kuwasaidia wao wakati ule lakini siku hizi wao ndio kikwazo kikubwa kwa sababu wana njia mbadala Afrika ya Kusini na Msumbuji.
Je Tanzania iendelee kufumba macho na kupata hasara eti ni ushirikiano?
Siku hizi lazima tuangalie maslahi ya kiuchumi zaidi si kisiasa. Tumesaidia sana watu kupata uhuru leo tunaambulia matusi.
Hakuna kitu kinafanyika tazara mpaka Zambia wakubali wakati huo huo hawana nia ya kuokoa hiyo reli. Bora tuende kivyetu na tuunganishe mikoa mingine kwenye mtandao. Mfano inaweza kutoka tunduma ikaenda sumbawanga. Njombe ikaenda ruvuma nk. Kwa mfumo wa sasa hilo gumu.