Tanzania: Chanzo cha kuporomoka kwa Maadili katika Jamii na Hatma ya Taifa!

Umenikumbusha .mjadala wa jana usiku mimi na washkaji zangu ulioenda hadi saa tisa usiku. Tulikuwa tunajaribu kuangalia ni kwa namna gani jamii yetu ilipo. Mawazo ambayo yalikubaliwa na wengi ni kuwa..
1. Wazazi wawalee watoto wao katika misingi ya dini tangu wakiwa wadogo. Hii itasaidia hata wakiwa watu wazima wawe na hofu ya kufanya vitu vingine ambayo jamii yetu ni viovu.

2. Wazazi wasiwafungulie dunia mapema watoto wao, kwa maana ya kuwa wasiiwaache watoto wakaanza kuyaona ya dunia wakiwa bado wadogo. Kuwapeleka watoto wadogo maeneo kama day care ni kutaka kumharibu mtoto tu. Mtoto kaa naye akue akiwa nawe. Akifika umri wa kwenda shule mpeleke.

3. Vijana wajitahidi kupata elimu yenye uwoano sawa kwa upande wa elimu ya dini na elimu ya dunia. Hii itawasaidia wao kujua pande zote za dunia hivyo kutokuwa rahisi kwao kuyumbishwa hovyo.

4. Na kila mtu awe na misingi yake binafsi ya kuifuata kwa moyo wake wote as long as inakubalika na jamii yetu.
 
Kama ulisoma lugha, neno lolote ambalo halimo kwenye lugha yako iwe mama au ya shuleni, ujue tendo au nomino ile ni ya kuletwa. Naanza na neno Safari, limo kwenye kamusi ya kiingereza na lugha nyingine nyingi lakini walitohoa toka kiswahili sababu hawakuwa na tabia ya kutembelea wanyama maana hawana.

Neno Jumbo linatokana na neno Jambo ambalo alipewa Tembo mkubwa sana aliyepelekwa England 18 something. Alikuwa ni yatima akawa anakua haraka mpaka wakasema ni mnyama ambaye alikuwa mkubwa sana. Baada ya yeye kugongwa na train Canada, jina lilibaki na ndiyo mwanzo wa Jumbo jets, Jumbo Burger and so on.

Nakuuliza sasa neno Usagaji, ushoga, mabasha, wasenge ni lugha gani? Je kuna lugha ya makabila ya bara???? Ukipata jibu utajua kuwa hizi mila zilikuwepo saana tu ila siyo bara sana sana Pwani na yawezekana tokana na mwingiliano wao na watu wa Middle east na far East. Nikosoe kama nimekosea.
Asante sana, kwenye mila zetu mambo hayo, ni miiko na laana
 
Nimekaa chini na kujaribu kukumbuka ni wapi watanzania tulianza kupotea kimaadili in gross terms na nimejikuta nikigota kipindi cha awamu ya pili. Pamoja na some good changes zilizofanyika kipindi hicho mfano re-introduction ya vyama vingi, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kushiriki/kushirikishwa, uhuru wa kuheshimu mawazo tofauti, kuondoa siasa mashuleni etc.

Lakini ni kipindi hiki hiki maneno kama "Dili" ikimaanisha biashara au shughuli ya kuingiza pesa chap chap (Whether legal or illegal) yalianza. Mengine pia kama Watu kutoheshimu amri za serikali, Misheni town, Uvamizi wa maeneo ya wazi, Waajiriwa hewa serikalini, Wizi mkubwa mkubwa wa mali ya umma, Kutoheshimu shule na proffesions, Kutoheshimu sheria, Uingizaji na uuzwaji Counterfeits bila woga, Kuporomoka kwa elimu, kutokulipa kodi, Kuongezeka kwa ujasiri wa kutenda uhalifu, Kuongezeka kwa uongo uongo etc. yalikuwa kwa kasi katika kipindi hiki.

Well najua kuna wengi watakuwa na maoni tofauti nadhani ni vema tujadili. Pia naomba nisieleweke kwamba hayo niliyoyataja hayakuwepo kabisa katika awamu ya kwanza. But it is the degree that do think should matter!


==========
SOMA ZAIDI:
==========

=> Mbowe alia na kuporomoka kwa Maadili! Soma - Kuyumba maadili chanzo cha gulio la kura - Mbowe

=> Maoni ya Mhe. Kigwangalla => Kuanguka kwa Nidhamu na Maadili Kutasababisha Kuanguka kwa Taifa!

ATHARI ZA KUPOROMOKA KWA MAADILI:
Maadili yanaendana na highest potential energy katika maisha, yaani kutekeleza mambo ambayo watu wengi hawapendi kwa hiari. Watu wenye maadili hufanya mambo yao kwa mujibu wa sheria hata kama hawayataki; kusimama kwenye red traffic lights wakati hamna gari nyingine kwenye junction hiyo ni mfano mmojawapo. Kuporomoka kwa maadili katika jamii kunatokana na serikali kutosimamia sheria zake, na kuruhusu kila mtu ajifanyie mambo kivyakevyake.

Ni kweli mwishoni mwa miaka ya themanini na mwanzozi mwa miaka ya tisini, maadili yaliporomooka sana kwa vile kila kitu kilikuwa ni ruksa, hakukuwa na sheria. Baada ya lile jamaa lilofuata kuanza kukazania sheria tena katika hiyo miaka ya mwishoni mwa tisini nidhamu ikarudi tena, ila lilipokaribia kuondoka likajua nalo linahitaji madili, kwa hiyo likalegeza kidogo na kuachia ndoo yote ya maadili kuanguka tena bondeni. Yule kaka aliyefuatia akawa ni mtu low energy kabisa wala hakujali kabisa kuvuta tena ile ndoo as long as kwa kila safari yake ya nje alikuwa akirudi na kibaba. Watuhumiwa wa wizi walikuwa wanaombwa warudishe walichoiba kwa hiari yao, siyo kwa sheria kufuata mkondo wake.

Sasa hivi kunapokuwa na hili lijamaa ambalo linasema sheria ni msumeno ambo watu hatukuzowea basi maadili yanajijenga tena pole pole, ila watu tuna hasira kwa vile hatukuzowe, hivyo tunataka lijitu hili liondoke mara moja ile turudiea maisha yetu ya kusubiri kibaba kotoka nje (lowest potential energy). It is a very complex situation.

Niliwahi kuandika hapa mwaka 2006 (enzi za JamboForums) kuhusu namna ya kuunda mfumo wa serikali thabtii isiyoyumbishwa na mabadiliko ya raisi, ila kwa vile forum imepitia mabadiliko mengi siwezi hata kupata linki yake. Jambo la kwanza ilikuwa ni kupunguza madaraka ya rais katika hali inayotenganisha kabisa utendaji Wizara za Mambo ya Ndani, na ile ya Sheria kuwa ni wizara independent kabisa ambazo haziogopi mtazamo wa rais bali zinaogopa sheria tu.
 
thabdi isiyoyumbishwa na mabadiliko ya raisi, ila kwa vile formu imeptia mabadiliko mengi siwezi hata kupata linki yake. Jambo la kwanza ilikuwa ni kupunguza madaraka ya rais katika hali inayotenganisha kabisa utendaji Wizara za Mambo ya Ndani, na ile ya Sheria kuwa ni wizara independent ka
Mchango adhimu mNo mno mnoooo, asante, hasa hicho kipande cha mwisho
Asante sana ndugu
 
Ni post effect ya globalization, however we can't justify it,kwa mfano kisiwa cha Cuba wameweza ku control western effect, ikiwa ni pamoja na hiyo pornography. Sera, na promotion ya mila na desturi zetu ni factor pia,lakini unaanzia wapi, wakati kanisa limehalalisha ndoa jinsia moja?
*Do you remember Padre Sixtus Kimaro???? Yuko salama anapunga hewa vatican
lakini shekhe wa juzi aliyebaka mtoto amefungwa maisha
 
26113863_1302005513239493_16743660876745699_n.jpg
 
Nashindwa kupata jibu hapa nani wakumlaumu kwa matukio yote machafu yanayofanywa na jeshi la police.

je ni viongozi wa ngazi zajuu katika jeshi la police,raisi wetu kwauteuzi mbovu wa viongozi wa jeshi la police,katiba yetu iliyompa madaraka makubwa raisi au mmomonyoko wa maadili katika jeshi letu la police unaosababishwa na ajira za kindugu zilizopelekea jeshi la police kuwa jalala la wahuni.

Nasema jalala sababu jeshi la police limejaa vilaza,wavuta bangi na waliofake vyeti.

Kwa maoni yangu mimi nailaumu katiba tuliyonayo sasa &[HASHTAG]#305[/HASHTAG];mempa raisi madaraka makubwa sana ya uteuzi, waliyotunga katiba hawakukumbuka kuwa akili za wanadamu hazifanani matatizo yamekuja pale nchi ilipokabidhiwa kilaza namajuku yote muh&[HASHTAG]#305[/HASHTAG];mu ya nchi hususani uteuz&[HASHTAG]#305[/HASHTAG]; wa v&[HASHTAG]#305[/HASHTAG];ongoz&[HASHTAG]#305[/HASHTAG]; yako ch&[HASHTAG]#305[/HASHTAG];n&[HASHTAG]#305[/HASHTAG]; yake wewe unategemea n&[HASHTAG]#305[/HASHTAG];n&[HASHTAG]#305[/HASHTAG]; k&[HASHTAG]#305[/HASHTAG];tafany&[HASHTAG]#305[/HASHTAG];ka.

WATANZAN&[HASHTAG]#304[/HASHTAG];A TUSIFANYIE MZAA KATIKA HAYA TUNAYOYAONA SASA HUN&[HASHTAG]#304[/HASHTAG];MWANZO TU KTAKUJA KILAZA KINGINE KIFANYE MADUDU ZAIDI YA KILAZA ALIYETOKA. TUSIKUBALI KUBURUZWA KATIKA MCHAKATO WAKUPATA KATIKA MPYA.ASANTEN&[HASHTAG]#304[/HASHTAG]; ...... AMAN&[HASHTAG]#304[/HASHTAG]; NA UPENDO DAIMA.

MKUU JESHI LA POLISI WALIKUTEKENYA NINI? naona umeamua kuchepuka kabisa kwenye mada na kuanza kushabulia Jeshi letu. Aidha usitegemee uwepo wa katiba mpya ukadhani ndio itakua suluhisho la makando kando yoote, unahitaji taifa lenye MORAL ETHICS ambazo zitazaa PATRIOTS tutaoweza kuwakabidhi majukumu ya kuiendesha nchi, hiyo katiba unayoiabudu ikikosa watu wenye MORAL ETHICS na PATRIOTS ni kitabu cha hadithi za abunuasi tu!
 
Wanabodi Habari

Wazo kuntu
Maneno haya ni maaru sana kwa watu wa kada hizi: Watu wa magari utawasikia ENGINE OVERHALL, moja mbili mafundi wa simu utawasikia KUFLASH na tatu mafundi kompyuta utawasikia KUFOMART COMPUTER.

Sasa ni wakati KUFOMART kizazi chetu japo hili litachukua muda kati ya miaka 17-20.

Kivipi?
Tunahitaji kuufumua mfumo wetu wa malezi na elimu ili tuu usuke upya.

Tatizo liko wapi?
Hatuwezi kubadilisha mfumo wa malezi kwa atu wambao hawakupata malezi hayo.

Sasa tunafanyaje?
Tuchague watu ambao wata execute hii mission iwe ni kutoka TISS au JWTZ/JKT waanzishe shule ambazo zitawafua vijana.

Pili tuwe na shule zenye kuwalea watoto kiimani lakini kwa kuandaa mtaala ambao ni shirikishi.
 
Ni hali ya kidunia, effect of globalization,lakini sio sababu kwetu kutojitetea..kwani kisiwa cha Cuba kimeweza my control western influence hadi hiyo pornography

kwani mlikuwa mnamaadili mazuri..hasa kwako mwananamke unaona maadili ya kabla ya utandawazi ungeweza toa hoja apa ikathaminiwa sawa na wanaume

minaona sasahivi tuna uhuru zaidi wakuongelea vitu tunavyopenda na tusivyovipenda bila kujali jamii itakufikiriaje na hii ndo highest form ya maadili.

enzi za kukeketa , umaskini uliopitiliza, mi naamini asilimia 70 ya watu walio zaliwa chini ya miaka ya themanini wana upungufu wa akili sababu ya lishe duni kwaiyo hoja zao ni shortsighted

ata mtu aliyezaliwa miaka ya hamsini wazazi wake walimwambia anapungukiwa maadili kwa kujifunza vitu vipya
 
Hii mada ni pana sana na naona wadau wengi wanachangia kutokea pande tofauti tofauti. Ningekuwa najua chiingereza ningesema from different perspective sijui ndo hivi haya tuendelee. Nionavyo mimi hoja hapa ni mabadiliko ya tabia na mwenendo mzima wa mtanzania. Mtoa mada amejaribu kuonyesha kuwa mporomoko huo wa maadili ulishamiri zaidi wakati wa utawala wa awamu ya pili.

Msisahau lakini awamu ya kwanza askari walikuwa wanatembea na chupa ya bia na wakikukuta umevaa sarawili nyembamba sana kiasi cha ile chupa kushindwa kupita cha moto utakiona.

Haya ngoja niakae vizuri ili niweze kuchangia sasa.. NNionavyo mimi mabadiliko haya ambayo mengine ni chanya na mengine ni hasi yamechangiwa na factors lukuki lakini kuzitaja mbili kuu ni mosi ni utandawazi kwa ujumla wake ndo kinara cha uharibifu au ujenzi wa twabia zetu za leo.

Sasa wakati wa awamu ya kwanza watu hawakuwa na exposure ya kutosha juu ya jamii zingine. Watanzania walikuwa kama viumbe tu flani waliofungiwa ndani ya chumba hata mwanga wa jua hawauoni. Lakini la pili sisi watanzania na waafrika wengi sijui ni kwasababu gani, tumekuwa tu na utumwa wa kifikra.

Tunapoona yanaoendelea ulaya na amerika basi huwa tunaona ya kule yooote bila uchambuzi ni mazuri tu kushinda yetu. Tulipopata uhuru wa habari tukawa marimbukeni na kuiga kila tukionacho kwenye senema bila kujua kuwa hata wenyewe wa Ulaya na Amerika hawaishi maisha hayo ya kwenye senema.

NAOMBA KUUNGA MKONO HOJA
 
Back
Top Bottom