Tanzania: Chanzo cha kuporomoka kwa Maadili katika Jamii na Hatma ya Taifa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Chanzo cha kuporomoka kwa Maadili katika Jamii na Hatma ya Taifa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, Feb 13, 2009.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nimekaa chini na kujaribu kukumbuka ni wapi watanzania tulianza kupotea kimaadili in gross terms na nimejikuta nikigota kipindi cha awamu ya pili. Pamoja na some good changes zilizofanyika kipindi hicho mfano re-introduction ya vyama vingi, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kushiriki/kushirikishwa, uhuru wa kuheshimu mawazo tofauti, kuondoa siasa mashuleni etc.

  Lakini ni kipindi hiki hiki maneno kama "Dili" ikimaanisha biashara au shughuli ya kuingiza pesa chap chap (Whether legal or illegal) yalianza. Mengine pia kama Watu kutoheshimu amri za serikali, Misheni town, Uvamizi wa maeneo ya wazi, Waajiriwa hewa serikalini, Wizi mkubwa mkubwa wa mali ya umma, Kutoheshimu shule na proffesions, Kutoheshimu sheria, Uingizaji na uuzwaji Counterfeits bila woga, Kuporomoka kwa elimu, kutokulipa kodi, Kuongezeka kwa ujasiri wa kutenda uhalifu, Kuongezeka kwa uongo uongo etc. yalikuwa kwa kasi katika kipindi hiki.

  Well najua kuna wengi watakuwa na maoni tofauti nadhani ni vema tujadili. Pia naomba nisieleweke kwamba hayo niliyoyataja hayakuwepo kabisa katika awamu ya kwanza. But it is the degree that do think should matter!


  ==========
  SOMA ZAIDI:
  ==========

  => Mbowe alia na kuporomoka kwa Maadili! Soma - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/105282-kuyumba-maadili-chanzo-cha-gulio-la-kura-mbowe.html

  => Maoni ya Mhe. Kigwangalla => https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/473843-kuanguka-kwa-nidhamu-na-maadili-kutasababisha-kuanguka-kwa-taifa.html

  ATHARI ZA KUPOROMOKA KWA MAADILI:
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nadhani kwa mawazo yangu, kujadili lini maadili yalianza kuporomoka si jambo la msingi sana.Wote tunakubaliana kwamba maadili yameporomoka.Kama kuna wasio kubali, basi hao wana ajenda zao za siri.Nadhani la msingi kujadiliwa ni jinsi ya kurekebisha hali hiyo, ili Tanzania isizidi kuelekea "to the abyss."
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Kichwa cha hoja yako kinasema "Maadili Tanzania yalianza kuporomoka". wakati huo huo kwenye ufafanuzi wako unasema "yalikuwa kwa kasi katika kipindi hiki". Ni dhahiri hujui, sijui na hakuna ajuaye maadili yalianza kuporomoka wapi na lini. Kama alivyosema Tikerra muda sio hoja, muhimu ni kuwa kutoka hapa tulipo tuende wapi kwa kutumia njia gani?
   
 4. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Nyambala kasema,maadili yalianza kuporomoka awamu ya pili ya uongozi wa Taifa letu.
  Hivyo,awamu ya kwanza ili kwanza ilikuwa shwari;kwa hiyo utamaduni wa awamu ya kwanza urudishe katika matumizi ya maisha yetu ya kila siku.
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Agreed!!
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Juzi nimemsikia Mzee Mwinyi akisema alileta sera za "ruksa" kuliua azimo la Arusha.
  Lakini alichokifanya ni kama mzazi kumwaga chini maji ya beseni huku mtoto akiwa ndani ya beseni. Arusha lilikuwa na maadili ya uongozi. Zanzibar likayafuta. Matokeo yake ni huu ufisadi uliokithiri hadi Ikulu
   
  Last edited: Feb 14, 2009
 7. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyambala anasema alijaribu kukumbuku ni lini maadili yalianza kuoromoka, nadhani akaishia nusu ya ufunuo na akanza kuandika je anakumbuka majina na maneno haya yalikuwepo wakati gani? RTC BOT NBC GAPEX UGAWAJI MADUKA YA USHIRIKA ULANGUZI MIKINGAMO nk na JOKERI la la kumalizia mchezo ilikua OPERESHENI ya marehemu SOKOINE??????
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Maadili yalianza kuporomoka pale walipo-dhulumiwa watu mali zao na kufanywa mali za umma.

  Nani ataewajibika ikiwa ni mali ya umma?
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nyambala,

  Inawezekana awamu ya pili ilikuwa ni mwanzo wa mambo mengi lakini hili la kuporomoka maadili nahisi halikuanzia hapa. Sioni haja ya kuzunguka sana kujaribu kutetea hoja yangu isipokuwa kama tutajuuliza awamu hiyo ilipochukuwa hatamu mashirika ya umma mangapi yalikuwa yakifanya kazi au kulikuwa hakuna waliokuwa na maisha mazuri kwa kutumia nyenzo za umma na kuwaacha wengine wakiwa na maisha duni.

  Aidha juu ya utajiri na nguvu za wananchi kuwepo mbona tulifikia hatuwa ya kula dona la Yanga? Pengine katika historia ya Tanzania hatujawahi kuwa na maisha magumu kama tuliyoyapat mwisho wa awamu ya Kwanza.

  Suala la kujiuliza hapa kuwa kuanzia 1961 hadi 1985 karibu miaka 25 chini ya utawala wa maadili ni nini kilitusibu hadi tukawa fukara mbali ya umasikini?

  Hata hivyo ushahidi ulikuwapo kuwa bado viongozi hawakuwa na matatizo ya maisha kama wananchi walivyokuwa na tabu za maisha, sasa uadilifu ulikuwepo wapi?
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kuna ushahidi wowote nkuwa hilo Azimio likifuatwa?
   
 11. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ili kupata ufumbuzi mwema na bora ni lazima tuanzie mwanzo: kwani miaka 25 ni muda mrefu kwa hali yeyote na katika fani yeyote. kwa hiyo swala la umaskini na ufukara tumetoka navyo awamu ya kwanza (Pamoja na SIFA NJEMA kwa Mwalimu za kutuachia zaidi ya 3/4 ya MALI ASILI ikiwa haijaguswa)
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,546
  Likes Received: 81,981
  Trophy Points: 280
  Maadili yatikisika ofisi nyeti nchini!

  Raia Mwema - Mei 20, 2009

  - Kuanzia Ikulu, Polisi hadi Magereza
  - Vigogo wabweteka, sheria zavunjwa


  HALI ya uadilifu miongoni mwa watendaji katika ofisi kubwa na nyeti za serikali kuanzia Ikulu, Ofisi ya Makamu wa Rais na hata katika vyombo vya ulinzi imetetereka, na hasa katika uzingatiaji wa matakwa ya kanuni na sheria za matumizi ya fedha.

  Kuyumba kwa uadilifu katika ofisi hizo nyeti za serikali kumethibitishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, katika ripoti yake ya ukaguzi wa hesabu wa hadi Juni 30, mwaka jana.

  Ikulu, ofisi ambayo ilipaswa kung'ara zaidi kimaadili mambo si swari ikibainika kuwa imekuwa ikifanya baadhi ya mambo shaghala baghala katika mipango yake ya ununuzi.

  Doa hilo katika Ikulu linatajwa na CAG kuwa limetokana na ofisi hiyo nyeti kukiuka kifungu cha 45 kipengele ‘a' hadi ‘e' cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.

  Sheria hiyo iliyowahi kuwa gumzo katika mjadala wa kununua au kutonunua mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans, inataka ununuzi ufanywe katika mpango mahsusi, unaokidhi mahitaji ya mwaka husika.

  "Ofisi ya Rais – Ikulu haikuandaa mpango wa manunuzi na kufuata kama sheria inavyoelekeza," anaeleza CAG katika ripoti yake hiyo, ambayo pia iliwasilishwa katika Mkutano wa 15 wa Bunge, uliomalizika Aprili 30, mwaka huu.

  Lakini si Ikulu pekee iliyobainika kukiuka sheria halali za nchi ambazo ofisi hiyo ilipaswa kuwa mfano katika kuziheshimu, bali hata Ofisi ya Makamu wa Rais.

  Katika ofisi hiyo nyeti pia imebainika kuwa kulifanyika ununuzi wa samani kinyume cha matakwa ya sheria ya manunuzi.

  "Manunuzi ya samani nje ya mpango wa manunuzi wa mwaka ya Sh 78,148,000 yalifanyika kwa kutumia njia ya moja kwa moja inayofaa kwa manunuzi madogo madogo, kinyume cha maelekezo ya kifungu namba 45 kipengele ‘a' na ‘d' cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 21 ya mwaka 2004," anasema CAG.

  Kuporomoka kwa maadili na kudharauliwa kwa sheria katika ofisi hiyo ya Makamu wa Rais pia kumebainishwa na CAG katika matumizi sahihi ya bajeti iliyotengwa.

  Katika hilo, CAG anasema; "Malipo ya madeni ya Sh 89,244,290 yalifanyika kwenye bajeti ya mwaka huu ulioishia Juni 30, 2008, bila idhini. Risiti za kukiri malipo ya Sh. 8,920,000 hazikuwasilishwa kwa ukaguzi."

  Mbali na hayo, CAG anasema kulikuwa na mali zenye thamani ya Sh. 191,124,623 ambazo hazikuingizwa kwenye rejesta ya mali za kudumu, hapa sababu za hali hiyo zikiwa hazijabainishwa japokuwa ni dhahiri kuwa kuna uzembe na utovu wa maadili.

  Katika hatua nyingine, kwa mujibu wa ukaguzi wa hesabu na katika hali ya kuzua maswali mengi, imeelezwa kuwa madeni ya Sh 208,058,691 hayakukaguliwa kutokana na kukosekana nyaraka ambatanifu.

  Hali hiyo inayotia shaka mustakabali wa Taifa kama itaachwa iendelee pia imeikumba Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali. Katika ofisi hii, inaelezwa kuwa mishahara ya jumla ya Sh 8,553,453.39 ililipwa kwa watu waliokwishaondoka katika utumishi wa umma.

  Utata wa kimaadili katika ofisi nyeti za umma pia imevikumba vyombo vya dola ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi na Magereza.

  Katika idara ya polisi malipo ya Sh. 74,110,000 yalifanywa bila kuwapo nyaraka sahihi.

  "Kufikia mwisho wa mwaka, Juni 30, 2008 kulikuwa na masurufu yasiyorejeshwa yanayofikia Sh 131,000,000. Huu ni ukiukaji wa kanuni namba 103 kifungu 1 ya kanuni za fedha za umma za mwaka 2001 (kama zilivyorekebishwa 2004)," anasema CAG na kufafanua kuwa;

  "Kanuni hizo zinataka marejesho yafanyike mara baada ya mambo yaliyosababisha masurufu hayo kulipwa kukamilika au ifikapo siku ya mwisho ya mwaka ambao masurufu yalitolewa.

  Jambo jingine la kutilia shaka ni kwamba taarifa za utendaji zinazoonyesha malengo mkakati, mafanikio yaliyotarajiwa na mafanikio halisi haikuwasilishwa kwa CAG pamoja na taarifa za fedha kinyume cha matakwa ya kifungu namba 8 kipengele cha 5 cha sheria ya fedha za umma namba 6 ya mwaka 2001.

  Katika Idara hii ya Polisi kashfa kubwa zaidi iliyoibuka wakati wa ukaguzi wa CAG ni kufanya matumizi zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  "Taarifa ya fedha ilionyesha huduma ambazo hazijalipwa za jumla ya Sh. 2,024,920,000. Hii ina maana ofisa masuuli alitumia kiasi hicho, zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge. Kama kiasi hiki kingelipwa na kuingizwa kwenye taarifa ya matumizi fungu hili lingekuwa na malipo ya ziada ya kiasi hicho hicho.

  "Taarifa ya fedha inaonyesha kiasi cha madeni ya Sh. 23,354,120,000 na hali hii ni uthibitisho kuwapo matumizi zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa" anasema CAG.

  Kwa upande wa Idara ya Huduma za Magereza, uongozi uliidhinisha matengenezo ya magari ya Sh. 205,404,964 bila kupitia kwa Wakala wa Ufundi na Umeme kinyume cha matakwa ya kanuni namba 59 (1) – (2) ya kanuni za umma za manunuzi za mwaka 2005.

  Kwa sababu hiyo, ubora wa matengenezo yaliyofanyika na thamani iliyopatikana kutokana na matumizi hayo haikuweza kuthibitishwa kwa vile magari husika hayahakikiwa na ofisa au fundi aliyeidhinishwa.

  "Malipo ya Sh 824,563,334 yalifanywa bila kuwapo nyaraka sahihi. Kiasi cha Sh 16,536,960 kililipwa kwa ofisa aliyeenda India kwa matibabu bila kuwapo rufaa iliyoidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

  "Manunuzi ya Sh. 119,875,376 yalifanywa kwa kutumia kinukua bei na bila ya kupitisha kwenye Bodi ya Manunuzi kinyume na kifungu namba 30 cha sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004," anaeleza CAG katika taarifa yake kuhusu ukaguzi wa hesabu za serikali kuu.
   
 13. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna sababu nyingi za chanzo cha kuporomoka maadili zinazotajwa na wataalamu wa masuala ya elimu jamii wewe binafsi unadhani mambo gani yamechangia maadili ya jamii hasa Tanzania kuporomoka kiasi hiki, hasa umalaya, kuvaa uchi, ulevi, utovu wa adabu, wizi, lugha chafu na mengineyo?
   
 14. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Rejea maandiko matakatifu. MATH24:3- Kaka huo bado ni mwanzo tu. Kama wadada wa university wanavaa masalawili na vipedo, unatarajia nani wa kurekebisha jamii. Na imani hata humu JF wamo wa dada wanavaa vibaya au kina kaka wanayapenda mavazi mabovu. Ingawa maadaili si mavazi tu, hata lugha. Wasomi nao wanachangia.
   
 15. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,646
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Watu wameachana na mafunzo yote ya mila zao achilia mbali dini zao ndo Tv,internet,simu zimekuwa walimu siku hz na huu ni mwisho wa dunia unaaproach kabisa..masharobaro,na masista du ndo ful kuiga akina justin biebier,kim kardashian,lil wyne na wamarekani weusi wakidhani ni UJANJA au ndo kwenda na wakati mi nawaonea huruma sana watu kama hawa hasa akina dada imagine mtu kavaa skin tight jua kali ama night dress kariakoo sa saba mchana? Wanapiga jeki manyonyo na kuyaacha wazi mi sipendi uhalo huu jamani..we acha tu hata humu Jf wamo lets wait for ther comments
   
 16. b

  black and white Senior Member

  #16
  May 21, 2013
  Joined: Apr 25, 2013
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashindwa kupata jibu hapa nani wakumlaumu kwa matukio yote machafu yanayofanywa na jeshi la police.
  je ni viongozi wa ngazi zajuu katika jeshi la police,raisi wetu kwauteuzi mbovu wa viongozi wa jeshi la police,katiba yetu iliyompa madaraka makubwa raisi au mmomonyoko wa maadili katika jeshi letu la police unaosababıshwa na ajıra za kındugu zılızopelekea jeshi la police kuwa jalala la wahuni.nasema jalala sababu jeshi la police limejaa vilaza,wavuta bangi na waliofake vyeti.

  Kwa maoni yangu mimi nailaumu katiba tuliyonayo sasa ımempa raisi madaraka makubwa sana ya uteuzi, waliyotunga katiba hawakukumbuka kuwa akili za wanadamu hazifanani matatizo yamekuja pale nchi ilipokabidhiwa kilaza namajuku yote muhımu ya nchi hususani uteuzı wa vıongozı yako chını yake wewe unategemea nını kıtafanyıka.

  WATANZANİA TUSIFANYIE MZAA KATIKA HAYA TUNAYOYAONA SASA HUNİMWANZO TU KTAKUJA KILAZA KINGINE KIFANYE MADUDU ZAIDI YA KILAZA ALIYETOKA. TUSIKUBALI KUBURUZWA KATIKA MCHAKATO WAKUPATA KATIKA MPYA.ASANTENİ ...... AMANİ NA UPENDO DAIMA.
   
 17. dada white

  dada white JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Polisi ni jamii part ya jamii yetu ila siku hizi hampendwi kila kona,Wakuu wa idara hii inabidi mchukue hatua vijana wenu wanawawakilisha vibaya huku mitaani.
   
 18. l

  lazima ukae JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2013
  Joined: May 15, 2013
  Messages: 708
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  serikali ndio yakulaumiwa sababu mishahara inayowalipa askari wa jeshi la polisi haikizi mahitaji yao ndomana wanatafuta njia nyingine za kuongeza kipato chao.Wanachojua viongozi wetu ni kujilimbikizia mali ya uma na si kuboresha maisha ya watumishi wao ndomana haya yote yanatokea.
   
 19. F

  Frekim JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2013
  Joined: Mar 29, 2013
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ilaumiwe ccm. Kwa swali la pili nini kifanyike ccm iondolewe madarakani... Over!!!
   
 20. W

  Wimana JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2013
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Swali hilo ukimuuliza Juma Nkamia, Mbunge wa Kondoa atakujibu Jamii Forums ndio walaumiwe!
   
Loading...