Tanzania bora ni baada ya CCM kupumzishwa

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,822
Yapo mengi yanayoweka matumaini ya Tanzania bora baada ya hawa ndugu kuondolewa madarakani.

Hawa ndugu wameshindwa kujifunza wala kubadilika pamoja na kupigiwa kelele mno. Kwamba ni lipi hawakuambiwa?

1. Ni hii misafara mirefu yenye kutuweka barabarani bila ukomo kuwapa wao nafasi ya kupita kwa starehe zao?

2. Ni hii misafara ya magari kibao, madege juu au wapambe kusimama nyuma yao wanapohotubu? Mbona kwa beberu au yule mwamba wa M23 siyo hivyo?

3. Nini uhalali wa gharama kubwa za matibabu au mortuary kwenye hospitali za umma?

4. Kulikoni familia zile zile kuwa wao ndiyo wenye haki na keki ya taifa hili?

5. Vipi ajira serikalini kutokuwa za mkataba usiokuwa wa kudumu usiozidi angalau miaka 8 ili kuwapa nafasi na wengine?

6. Vipi wananchi wote katika nchi kutokushirikishwa kikamilifu serikalini kwenye ujenzi wa nchi hii?

7. Kwanini raslimali zetu kutokuwepo kikamilifu kwenye kuchangia katika ustawi wa maisha ya watu?

8. Kwanini watu kupotea, kuuwawa, kuteswa au kukamatwa pasipokuwa na uhalali?

9. Kwanini dhuluma na vyombo vya Dola?

10. Kwanini vilio vya maisha magumu ya watu kuangukia kwenye masikio viziwi?

FolQpVRaEAEb4UX.jpeg

11. Nk, nk.

Upinzani ni muhimu kujitenga na ya namna hiyo mapema, ambayo ni kero kubwa kwa wananchi.

Viongozi wa wananchi hawawezi kujitenga kiasi cha kujidhania wao ni miungu na watu ni watuhumiwa ama eti ni wahalifu sugu.

Sheria za nchi haziwezi kuelekezwa kwenye kuwapora watu mali zao.

Upinzani mjitafakari kujitofautisha kabisa na hawa watu kwani biashara ni asubuhi.
 
Wapumzishwe na Nani?maana Bora CCM kuliko chadema.
Wapi unasoma CHADEMA mjomba? Huoni mkururo wa kero zetu pale?

"Anahitajika mwingine kwa dharura mno mwenye kuyaelewa hayo."

Kwanini Rungwe wa ubwabwa asiwe serikalini au bungeni badala ya hawa tunaowaona kuwacheza shere wananchi?

Kwanini gharama za hospitali kuwa juu hivi? Ni dawa au ujuzi operation kuwekewa Bei hadi 20m/-?

Angalia Ankara kwa wagonjwa hospitali za umma na hasa Muhimbili kujiridhisha.
 
Mwenyezi Mungu anijalie uzima ili siku moja nije kushuhudia anguko la hiki kikundi cha walaji, kinachoitwa ccm
 
Mimi sioni mbadala Wa CCM sasa hivi.

Hata CCM wanaona kama wewe. Macho yenu yana kufanana kama siyo kufaana.

IMG_20230215_122840.jpg


Gharama hizi kwa mgonjwa ni kutokana na utaalamu, dawa, vifaa au ni majengo?

Kunahitajika mwanzo Mpya.
 
Hao CCM wanatutawala kwa uoga na hasira kwetu kwasababu wanajua hawana ridhaa ya kutuongoza, wanachotufanyia hakina tofauti na huyo n'gombe anayekamuliwa na Mwigulu huku amefungwa kamba, Mwigulu nae hajiamini, kwasababu anajua anaweza kutandikwa teke na n'gombe dakika yoyote.
 
Back
Top Bottom