Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,244
- 113,628
Jana tarehe 23, Novemba 2023 ilikuwa ni sikukuu ya Thanksgiving nchini Marekani.
Kama hujui sikukuu hiyo ina maana gani huko Marekani, zama Google au YouTube [zote hizo ni kampuni za Kimarekani 😉 🇺🇸] ufute ujinga.
Thanksgiving huwa ni siku ya Alhamisi ya mwisho ya mwezi Novemba kila mwaka.
Siku ifuatayo, yaani Ijumaa, huwa inajulikana kama Black Friday.
Black Friday ni siku ambayo madukani kunakuwepo na mapunguzo makubwa ya bei za vitu/ bidhaa.
Zamani kabla ya masoko ya mtandaoni hayajaenea na kuzoeleka, watu walikuwa wanaenda kupiga kambi kabisa nje ya maduka kama Best Buy ili kuwahi kuwa wa kwanza kuingia madukani humo pindi milango inapofunguliwa.
Ilikuwa ni vurugu sana. Watu walikuwa wanapigana. Wengine walikuwa wanakanyagana hadi kuuana kabisa.
Siku hizi hakuna sana hizo vurugu maana manunuzi watu wanafanyia kwenye mitandao.
Sasa cha kushangaza, eti hata Tanzania leo ni Black Friday!
Ina maana Tanzania nako wanasherehekea Thanksgiving siku hizi?
Wameanza lini kusherehekea sikukuu za Marekani? Na July 4th nayo wanaisherehekea?
Kubalini, kataeni, chukieni, oneni wivu, jibamizeni ukutani, mwisho wa siku Marekani ndo taifa bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya uhai!
Kama mnaiga hata black Friday, basi Marekani imewakamata panapo vizuri sana.
🇺🇸🇺🇸🇺🇸🇺🇸🇺🇸🇺🇸