BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Meneja wa TANROADS Kigoma, Mhandisi Narcis Choma amesema Serikali imetoa fedha zaidi ya Tsh. Bilioni 567 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara yenye jumla ya urefu wa Kilometa 420 zinazojengwa kwa kiwango cha lami kwa wakati mmoja mkoani hapo.
Amesema: “Hiki kinachofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu hakijawahi kutokea, kuna Barabara 9 zinazojengwa Mkoa wa Kigoma, hilo ni jambo kubwa.”
Ameongeza kwa kusema “Tunawashauri Wananchi kutoka mikoa tofautitofauti waje kuwekeza Kigoma kwa kuwa mji unafunguka na kumekucha, fursa zipo nyingi na wanakaribishwa kwa ajili ya kufanya uwekezaji.”
Amesema wakati miradi hiyo ya barabara ikiendelea, pia itaambatana na miradi mingine ya ziada, jumla ya Tsh. Bilioni 23 itatumika kukamilisha kazi hiyo.
Ameeleza “Baadhi ya maeneo yatafaidika na vituo vya afya, visima, ukarabati wa hospitali, shule na stendi. Baadhi ya maeneo yatakayofaidika ni Kasulu, Makele na Kibondo.
Aidha, ameongeza kuwa kuna mchato wa uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma ikiwa ni sehemu ya miradi sanifu ambayo inatarajiwa kufanyika mkoani hapo.
“Kutajengwa jengo jipya ya abiria, sehemu ya kuegesha ndege, barabara za kuingia uwanja wa ndege, sehemu ya kuegesha magari, control tower mpya, ofisi ya Fire, kituo kidogo cha kupoozea umeme na uzio, pia kutawekwa taa sehemu ya ndege kutua ambayo itawezesha ndege kutua hadi usiku,” amesema Mhandisi Narcis Choma
Akielezea kuhusu mradi wote anaeleza umegawanyika katika hatua nne, kwanza ni Manyovu - Kasulu (Kilometa 68.25), pili ni Kidyama-Mvugwe (Kilometa 70.5), tatu ni Mvugwe – Nduta (Kilometa 59) na nne ni Nduta-Kabingo (Kilometa 62.25).
Hatua ya Kwanza (Lot 1)
Mhandisi Laurent Gervance Mtayangurwa ambaye ni Mhandisi wa Mshauri wa Mradi, amesema wanaongeza nguvu ya ujenzi licha ya kuwa kumekuwa na mazingira ya mvua.
Lot 1 inahusisha Barabara ya Manyovu-Kasulu (Kilometa 68.25) na kuna madaraja makubwa matatu na madaraja ya boksi karavati 8, kati ya hayo 6 yamekamilika ujenzi wake.
Ameweka wazi kuwa katika kipande hicho kuna madaraja mengine yanayofahamika kwa jina la caravan pipes yapo 68 na kati ya hayo 56 yameshakamilika.
Amesema maendeleo ya mradi huo unatarajia kuchukua miezi 36 ni mazuri na gharama ya mradi katika kipande hicho ni Tsh. Bilioni 76.1.
Kuhusu ajira, amesema jumla wapo Wafanyakazi 192 ambao wote ni Watanzania na pia kuna raia wa kigeni 12.
Hatua ya maendeleo iliyofikiwa ni 47.12%.
Hatua ya Pili (Lot 2)
Mhandisi Narcis Choma anasema kipande cha mradi huo ni unaoanzia makutano ya Kanyani na kuishia Mvugwe (Kilometa 70.5) una gharama ya Tsh. Bilioni 83.7.
Ameeleza kuwa hatua ya mradi ilipofikia ni 56.14%, ukiwa nyuma kidogo kwa kiwango cha 0.5 ya mipango ambayo iliwekwa awali kuhusu matarajio.
“Tungempa mkandarasi mmoja barabara yote kwa maana hawamu zote nne, isingekuwa na ufanisi na kasi kama ilivyo sasa ndio maana tumegawa katika vipande vinne, hivyo kasi ni nzuri na tunategemea utaisha ndani ya muda tuliopanga.
“Mradi huu una faida kubwa kwa kuwa Wakazi wa Kigoma wamekuwa na changamoto ya kutokuwa na barabara za lami kwa muda mrefu, hivyo barabara hii itarahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii,” anasema Mhandisi Narcis Choma.
Naye, Reginald Kaganga ambaye ni Mhandisi Mshauri wa sehemu ya pili anasema mradi huo unatarajiwa kukamilika Oktoba 23, 2023.
Amesema “Natoa wito kwa Mkandarasi aongeze vifaa ili aendane na mpango kazi ambao aliuwasilisha kwetu wakati anaomba tenda.”
Hatua ya Tatu (Lot 3)
Mhandisi Narcis Choma anasema mradi huo wa Mvugwe – Nduta una barabara yenye urefu wa Kilometa 59.3 na gharama ya mradi ni Tsh. Bilioni 84.7, ujenzi wake ukiwa umefikia katika kiwango cha 86%.
Kuhusu masuala ya kiufundi zaidi kuhusu mradi huo, Mhandisi Sebastian Kisandu anasema ulianza Oktoba 26, 2020 na unatarajia kukamilika Oktoba 26, 2026 ambapo tayari wamekamilisha kiwango cha lami kwa urefu wa Kilometa 20.
Kutoka Kibondo hadi Nyakanazi lami imeshakamilika