Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,227
Si kawaida kuwasagia kunguni wahandisi wanzangu, lakini hii tunayoiona kwenye picha sijui niite uzembe, uhujumu aukukosa uelewa kabisa juu ya masuala ya barabara.
Lakini kwa vyovyote kichofanyika pale Mapinga kuelekea kilima cha Kerege , ni uharibifu ambao unaiondoa barabara ya Dar-Bagamoyo katika matumizi mazuri yanayotarajiwa.
Tunajua hapo nia ilikuwa kuweka vituta aina ya ndita.
Cha kusikitisha huyo mhandisi hajui aina ya lami iliyopo pale.
Lami iliyopo ni ile inaitwa Surface Dressing na inaweza kuwa layer moja au mbili.
Lakini kwa vyovyote lami hii ni nyembamba sana hata iliwa layer mbili, ukubwa wa 20-25mm(inchi moja).
Sasa kilichofanyika pale ni kuikata layer hiyo ili waweke lami sina nyingine(asphalt concrete). Lami hizo zimeshindwa kuumana na zimebanduka.
Kilichotokea na hasa baada ya mvua ni lami ya vituta kubanduka na layer za tabaka la chini ya barabara kuanza kulowa.
Kma kuna kansa , basi kwa barabara hii ni kansa, layer za chini zikiingia maji basi matengenezo ya barabara ni kila miezi sita.
Kansa hiyo.
Barabara imekatwa zaidi ya sehemu tano hapo Mapinga.
Sasa kwa Tanroads sijui weledi wa mainjinia wenu ukoje.
Injinia asiyeelewa mambo hayo kitaalam atafute sehemu nyingine kuajiriwa.
Hii barabara sasa hivi ndio mbadala wa Morogoro road, kwa uhujumu/uharibifu huu lazim vichwa vikatwe.