TANROADS na barabara za jimbo la Kibamba

Kwasenga

Member
Feb 24, 2021
50
52
TANROADS, kuweni na huruma aisee. Hivi huku kibamba mnajua mnamiliki barabara mbovu sana?

Je kazi mliyopangiwa ya kuassess barabara na kupeleka mapendekezo kwa Mh Rais mliifanya?

Ni lini mtaacha hii kwangua kwangua na kumwagilia maji barabara badala ya kutafuta suluhisho la kudumu?

Kwa kweli wananchi wa huku tunapata tabu sana tena sana. Jengeni basi barabara zenu alafu za huku mitaani tuendelee kupambana na hali zetu wenyewe.

Magari ya watu wanaoishi huku ni sawa na skrepa hata kama ni mapya, usafiri wa umma ni taabu sana kwa sababu ya ubovu wa barabara, tena za TANROADS.

Tunaomba majibu juu ya hili swala kwa kweli.

Kwa uchache wa barabara hizi ni pamoja na;

1. Mbezi mwisho via Makabe, mpigi magoe to Bunju.
2. Mbezi mwisho via Mbezi high school, mpigi magoe to Bunju.
3. Kibamba via kibwegere, mpigi magoe to Bunju. Nk.

Hizi ni barabara za TANROADS ambazo ni viunganishi vizuri sana hapa Dar es Salaam, ila zinaishia kukwanguliwa kwanguliwa tu.
 
.

Tutaacha kwangua kwangua baada ya serikali ya ccm uliyo ipigia kura 2020 kutoa pesa kwa ajili ya suluhisho la kudumu.
 
Nimepita juzi Jamaa wanazingua sana, barabara ya Mbezi Mwisho via Mbezi high school to Mpigi Magohe wanaikwangua kila Siku lami hawaweki...yaani nyumba zote za pembezoni mwa barabara zimechafuka kwa vumbi....mtu hata kuhamia kwako unaona uvivu.
 
Alafu hiyo ni barabara ambayo iko busy sana kuliko hata zile nyingine, wakikwangua baada ya wiki tabu inaanza upya. Sijui hii kwangua kwangua mjini inatoka wapi.
 
Mwaka 5 sasa wanakwangua tuuu lami hakuna wanatuchosha bana....hswa ni wazalendo au wachina? Sasa tumeambiwa tupewe kazi wazawa...sijui takuwaje watu wanefilisika miaka 6 hii imepita madeni hayalipwi hadi dhamana zinauzwa
 
TANROADS, kuweni na huruma aisee. Hivi huku kibamba mnajua mnamiliki barabara mbovu sana?
Je kazi mliyopangiwa ya kuassess barabara na kupeleka mapendekezo kwa Mh Rais mliifanya?
Ni lini mtaacha hii kwangua kwangua na kumwagilia maji barabara badala ya kutafuta suluhisho la kudumu?
Kwa kweli wananchi wa huku tunapata tabu sana tena sana. Jengeni basi barabara zenu alafu za huku mitaani tuendelee kupambana na hali zetu wenyewe.
Magari ya watu wanaoishi huku ni sawa na skrepa hata kama ni mapya, usafiri wa umma ni taabu sana kwa sababu ya ubovu wa barabara, tena za TANROADS.
Tunaomba majibu juu ya hili swala kwa kweli.
Kwa uchache wa barabara hizi ni pamoja na;
1. Mbezi mwisho via Makabe, mpigi magoe to Bunju.
2. Mbezi mwisho via Mbezi high school, mpigi magoe to Bunju.
3. Kibamba via kibwegere, mpigi magoe to Bunju. Nk.
Hizi ni barabara za TANROADS ambazo ni viunganishi vizuri sana hapa Dar es Salaam, ila zinaishia kukwanguliwa kwanguliwa tu.
Bado ndege 5 kwani wewe hutaki kuona tunapaki madege yetu pale uwanja wa ndege. Hizo billioni 500 kuliko tujenge barabara kilomita 500 za kibamba bora tununue midege mitano ikapaki pale chato
 
Barabara ya Kibamba - Kibwegere - Mpigi Magoe tayari wanechora X nyumba zilizopo ndani ya mita 22.5 na wametoa deadline zibomolewe na wamiliki mpaka ifikapo tarehe 26.01.2022, agizo ambalo limeanza kutekelezwa na wakazi. Hakuna malipo yoyote. Lami itajengwa kwa awamu, kila mwaka kilometa 2 ,mpaka ikamilike. Haya ndio maendeleo, kwa wengine furaha na kwa wengine vilio.
 
Nilichogundua hii barabara ni biashara ya watu. Haiwezekani ukwangue barabara tu alafu ulipe na baada ya siku tatu mashimo tayari. Tuwskwe wazi basi kwani wanaokwangua hawatakiwi kuweka vifusi?
 
Back
Top Bottom