Tani 6,740 korosho ghafi zauzwa

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1574341527153.png

Jumla ya tani 6,740 za korosho ghafi zimeuzwa katika minada miwili iliyofanyika katika wilaya za Kilwa na Ruangwa mkoani Lindi mwishoni mwa wiki katika msimu wa mwaka huu. Bei ya juu katika minada hiyo ilikuwa Sh 2,795 na chini ilikuwa Sh 2,675 kwa kilo moja kwa korosho ghafi.

Kaimu Msajili wa Vyama vya Msingi vya Ushirika Mkoa wa Lindi, Robert Nsunza aliyasema hayo jana wakati alipofanya mahojiano na gazeti hili ofisini kwake katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini hapa. Nsunza alisema korosho za daraja la pili ziliuzwa juu ya Sh 2,297 na chini Sh 1,850 kwa kilo moja, na kwamba mnada wa Wilaya ya Kilwa unaosimamiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao kinachotoa huduma zake wilayani Kilwa, Lindi na Manispaa ya Lindi, uliuza korosho ghafi tani 3,700 wiki iliyopita.

Alisema bei ya korosho ghafi iliyouzwa ya juu ilikuwa Sh 2,729 na chini Sh 2,645 kwa kilo moja kwa daraja la kwanza. Aidha, la pili iliuzwa Sh 2,297 bei ya juu na chini Sh 1,850 kwa korosho ghafi tani 130.58 zilinunuliwa katika mnada uliofanyika katika Kijiji cha Miteja katika Chama cha Msingi cha Ushirika cha Sisi kwa Sisi wilayani Kilwa.

Alisema Chama Kikuu cha Ushirika cha Runali kinachotoa huduma zake katika wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Liwale kiliuza tani 3,040.8 katika mnada uliofanyika Jumapili wiki iliyopita.

Alisema bei ya juu ilikuwa Sh 2,795 na chini Sh 2,700 iliuzwa katika mnada huo uliofanyika wilayani Ruangwa. Naye Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao, Nurdini Swalaa alisema kampuni 13 ziliomba zabuni katika mnada wa Miteja uliofanyika wilayani Kilwa mkoani Lindi.

Chanzo: Habari Leo
 
Back
Top Bottom