Mwizi aliyetoka gerezani auawa kwa kukatwa koromeo na Wananchi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,114
Sijawa Bakari (30) mkazi wa kijiji cha Nangumbu, Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, ameuawa kikatili kwa kukatwa Koromeo na watu wanaosadikika kuwa ni raia wenye hasira kali baada ya kumtuhumu kuwa ni mwizi wa mazao ya wakulima mashambani.
---
1686822517718.png
Sijawa Bakari (30) mkazi wa kijiji cha Nangumbu, Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, ameuawa kikatili kwa kukatwa Koromeo na watu wanaosadikika kuwa ni raia wenye hasira kali baada ya kumtuhumu kuwa ni mwizi wa mazao ya wakulima mashambani

Inaelezwa kwamba, kijana Sijawa alikuwa na Tabia ya wizi ambapo ni siku chache zimepita tangu atoke jela baada ya kutumikia kifungo kwa wizi wa korosho mashambani, Sijawa amerudi kutoka jela Mwaka huu mwezi wa 5.

Kutokana na zao la ufuta kuongezeka bei hadi shilingi elfu 4 kwa kilo, wezi wanaohujumu mazao ya wakulima shambani wamekithiri jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa matukio mengi ya wizi na mauwaji katika msimu huu.

Wananchi wanasimulia kwamba, walifahamu mienendo ya kijana huyo na kuamua kumfuata hadi nyumbani kwake ambapo walimkuta na shehena ya ufuta, licha ya yeye kutokuwa na shamba lolote.

Wananchi wanasema kwamba, kijana huyo alikuwa akivamia mashambani na kuiba masuke ya ufuta na baadaye kwenda nayo nyumbani ambapo alikamatwa akiwa anakafua ufuta huo (kutoa ufuta kwenye masuke yake).
 
Kama akikamatwa na kidhibiti amevuna alichopanda.
Kama alikuwa anapenda vya bure bora angeenda Mombasa huko akale na kulala bure.
 
Jf bhana!

Kama wameshindwa kutatua shida ya picha kwa tunaotumia app naamini wakishambuliwa na udukuzi ndio kwishnei kabisa
 
Hao wananchi waliomkata koromeo wasifumbiwe macho wachukuliwe hatu kwa mauaji. Ilitosha kumfikisha polisi akashitakiwe kwa wizi sheria ichukue mkondo wake
 
Je, katika maisha yako ya hapa duniani umeshawahi kuibiwa kitu chako cha thamani ulichokuwa ukikitegemea?

Endapo kama umewahi kuibiwa, Je, maumivu yake yalikuwaje?

Remember; "action and reaction are equal but opposite in directions".
Nimeibiwa mara kadhaa, vitu vya thamani kabisa kwangu na kiukweli niliumia japo maumivu hayo hayawezi kupozwa kwa kuondoa uhai wa mtu!
 
Back
Top Bottom