Tangu nioe sijawahi kuonja uchungu wa ndoa

JembePoli

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,324
995
Habari zenu wana Jamvi,

Ni miezi mitatu (03) tangu nifunge pingu za maisha (ndoa) takatifu nashukuru MUNGU nafurahia kuwa mume, na bado sijaanza kuonja chungu ya ndoa kama baadhi ya wanandoa wanavyolalamika ndio maana nikatumia kauri ya nafurahia kuwa mume.

Kilichonileta hapa Jamvini kabla ya kuoa nilikuwa na uhusiano na mabinti kadhaa wengine niliwataka lakini hawakunipa ushirikiano, wengine ndio vile walikuwa na visingizio kibao mpaka naingia mitamboni nilikuwa bado sijamega.

Lakini baada ya kuoa kila mwanamke niliemtaka (kipindi hicho) anataka tukamalizie nimejaribu kuwaeleza kuwa sasa nimeoa na nampenda mke wangu baadhi wamenielewa lakini kuna huyu mmoja ambae alikuwa hata simu yangu kupokea mpaka ipigwe mara 3 ndio apokee leo ananipigia na kutaka kwichikwichi nimekataa mara kadhaa lakini hii ya leo kali katishia ata forward msm kwa wife.

Ki ukweli sijui namba ya wife kapata wapi? Maana amenitajia, Sijawahi tuma msg kwake tangu nioe zote msm alizonazo ni za kabla ya mimi kuoa, mbaya zaidi anasema sio lazima mimi nighalamie yeye anamudu kila kitu nijifikilie kabla ya siku 2 niwe nimempa jibu.

Mimi mwanaume nimefikiliaaa nikaona huyu mpuuzi anaweza halibu ndoa yangu changa, nimeona jioni hii nimpelekee wife Simu mpya android na nisajili line nyingine alafu nimpe maana mtandao anaotumia mara kadhaa amelalamika upo slow kwenye net na hii itakuwa Gia ya kumaliza na kummaliza huyu fisadi anaetaka kuvunja utamu wangu kibwege Naombeni mnisaidie kama nimekosea.

Ahsante kama huta tukana au kukejeli.
 
Last edited by a moderator:
Naona unakaribia kufungua mlango na kukaribisha ukimwi kwenye familia yako changa.....kazi kwako
 
Vipi kama akiitafuta hiyo namba mpya ya mkeo akaipata?
Utambadilishia tena?
Mueleze mkeo ukweli wote, kweli siku zote itakuweka huru.
 
kama aliweza kupata hiyo bila wewe kujua.atashindweje kupata tena? be professional we dont deal with blackmailer that way.usimkubalie.utachuma majanga.mfahamishe mkeo kuwa kuna kidudumtu anataka kuvunja ndoa yenu
 
Mpk umekuja huku maana huna msimamo na ubongo wako. What u decide do it, walk the talk achana Na kuomba ushauri huku. We kama unataka ule mbunye sema tu
Mkuu soma taratibu utaelewa tu nimeomba msaada kusaidiwa kwenye maamuzi yangu.
Sina shaka na ndoa yangu ipo imara kwa mtu imara ndio maana wote nimewapa ukweli kuwa no more nimeoa.
 
Naona unakaribia kufungua mlango na kukaribisha ukimwi kwenye familia yako changa.....kazi kwako
Ahsante mkuu lakini hilo ni ngumu ndio maana nimejaribu kumkwepa kwa njia hiyo ya kumbadilishia wife # ili hata akituma msg zake kwa wife iwe hakuna majibu kwa kuwa line ya wife nitaipoteza mwenyewe
 
Pole mkuu,mueleze mkeo ukweli
Mmh shaka ni kutokueleweka tu hawa wenzetu (wanawake) % kubwa huwa hawaelewi zaidi atakuona chui kwa ngozi ya kondoo...ahsante kwa ushauri naomba nizidi kuufikilia
 
Vipi kama akiitafuta hiyo namba mpya ya mkeo akaipata?
Utambadilishia tena?
Mueleze mkeo ukweli wote, kweli siku zote itakuweka huru.
kama aliweza kupata hiyo bila wewe kujua.atashindweje kupata tena? be professional we dont deal with blackmailer that way.usimkubalie.utachuma majanga.mfahamishe mkeo kuwa kuna kidudumtu anataka kuvunja ndoa yenu
Ahsanteni sana wakuu kwa kweli hapo mmenifikilisha kuangalia upya wazo langu lakini kwa sasa acha tu nifanye hivyo,baadae nitumie mawazo yenu ili hata wazo langu la kumbadilishia line hii leo iwe sehemu nyingine ya ushaidi siku ninapoweka wazi kwake.
Heshima kwenu wakuu ahsanteni sana.
 
Ahsante mkuu lakini hilo ni ngumu ndio maana nimejaribu kumkwepa kwa njia hiyo ya kumbadilishia wife # ili hata akituma msg zake kwa wife iwe hakuna majibu kwa kuwa line ya wife nitaipoteza mwenyewe
Nawewe umebadili namba yako?
 
Kwanini usitumie hizo meseji za blackmail kama ushahidi? Simpro! I meant simple!
Mimi nilishazifuta kitambo sana.
Na hata kama nitatumia zile atakazofoward bado zitaonyesha tarehe ya siku aliyofoward sio tarehe hiyo niliyotuma mimi,mbaya zaidi hazijakaa poa zitamuumiza sana mke wangu najua atanisamehee lakini kiasi fulani hataniamini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom