Tangu nihisi mume wangu ana michepuko sina hisia nae

angalia hizo hisia zako za ukiwa zitakufanya na wewe utafute mchepuko na hatimaye kupoteza penzi lenu kabisa, jitahidi ukae naye chini muongee acha habari za kuhisi
 
wanaume hawajuagi tuu, ni mbaya sana kwa mwanaume kufanya kuchepuka hadi mke au mpenzi wako akahisi au akaona dalili za mwanaume kuchepuka au akajua kabisa kuwa unachepuka. Kwa wanakwake wakorofi watakusakama na kukufanyia ukorofi wa tit for tat. Ila kwa wanawake wengine anaweza asitafute mchepuko pembeni kama kukulipizia kisasi la akakosa hamu ya kuwa na wewe. Yaani anakuwa anaishi na wewe kama haupo vile.

Najua wengine mtasema wanawake msiishi kwa hisia zitawaumiza, ila ni rahisi sana kuhisi kuw huyu mtu anaichezea rafu kwa tabia anazozionesha mfano, mtu kurudi usiku ananukia marashi ya kike, shati lina alama za lipstic au make up, akirudi usiku simu anaizima na kuiweka kwenye chaji kila siku wakati haikuwa utaratibu wake, anatoa sauti mlio wa simu yake ikiita au msg ikiingia husikii, simu ikiita anaweza itazama asipokee na kusema aah wasumbufu hao.

Au akipokea anaaza na kujibalaguza, hapo nyumbani hamjambo, mama hajamboa a kinachoongelewa hakieleweki ili yule wa upande wa pili anajua kuwa hapo mazingira si mazuri kwa kuongea hivyo atakata simu. n.k. n.k. huu uzoefu nimeupata kwa kaka zangu hivyo ...... ndo hivyo!!

Ila wale baadhi ya wanaume wanaojitambua na kujifahamu atafanya uchepukaji wake weeh wala hautakaa uje kuhisi wala kujua kama anachepuka na hapo maisha yatasonga barabara na utapata ushirikiano mia ya mia kutoka kwa mwanamke.
ole mtoa mada cha kufanya tafuta kitu kinachokufanya kuwa na furaha na ukifanye hadi pale hisia zako zikirudi.

Kasie.
 
Usipokuwa makini very soon na wewe utaanza kuchepuka. Ni mbaya sana kumuhisi mwenzako maana hata akichelewa nyumbani kwa sababu ya kawaida wewe hutataka kumuelewa kwamaana ushamuhisi
Fanya kumuita umuambie unaweza ukaokoa jahazi maana;
1> Kama anachepuka kweli atakuwa makini maana anajua ushamuhisi
2> Kama hachepuki atakupa maelezo ambayo kwa namna moja yatakufanya utoke kwenye mawazo ya kumhisi vibaya.
Nakutakieni maisha mema, Mungu anachukia kuachana na ndoa iheshimiwe na watu wote
 
Habari wana JF,

Kiukweli nashindwa kujielewa,tangu nihisi mume wangu ana michepuko sina hisia nae kabisa. Sijui hata nifanyaje na ninaishi nae ndani.

Wadau nipeni mawazo.
ulihisi kwa nini jamani umejitengenezea hofu mwenyewe sasa inakutafuna maana ya kukosa nae hamu utamsababisha hata kama hana michepuko achepuke mchangamkie mumeo mpe mapenzi teeeele

mpetipeti hata mchepuko atausahau lakini kwa hisia tu unampeleka rasmi kwa michepuko
 
Back
Top Bottom