Tangazo hili la "Hakielimu" sidhani kama litadumu

Tangazo hili la "Hakielimu" sidhani kama litadumu

Acheni utani hili siyo tangazo ni taarifa ya habari imechukuliwa shule moja kijijini kwetu jamani serikali ya CCM ni sawa na mbwa kibogoyo atapenda minofu tuu
 
Bos Wa 'hakielimu' Anangozi Ngumu Sana Ameshaonywa Mara Kibao Na Kuitwa Wizarani Pale Na Kukaripiwa Ukizingatia Yeye Ana Asili Ya Kiasia Lakini Wapi Kakaza Mbaya

Pole boss aka contry Director wa Haki Elimu ni MTANZANIA mwenye asili ya Iringa na Tabora.Ni mtanzania mwenzetu anayejuq shida na raha za kuwa mtanzania.Amesomea bongo sana tu.Anajua hali halisi ya shule zetu.Hivyo tumpe moyo anahitaji support yetu.
 
Sasa lisivumiliwe kwa sababu gani? Mbona hilo tangazo si la leo na lipo karibu televisio zote...?Acheni kutengeneza hisia zisizo za msingi hakuna mwenye mpango wa kulifungia!

Heshima yako mkuu,Mimi nilidhani ya kuwa wewe ni. Msemaji wa ACT kumbe hata na serikali? Hongera zako tutashukuru sana kama kweli hamna mpango wa kulifungia maana hujumbe maridhawa kwa wa na jamii wote so serikali tu hata wananchi wanahusika
 
Hili ndilo tatizo la Watanzania. Tunasubiri serikali ije ijenge. Au tunasubiri mfadhili. Watanzania tunalo tatizo kubwa sana kiutamaduni. Ni AIBU.

Sidhani kama uko sahihi kulaumu Watanzania wote.

Kama kuna Wizara ambayo inahusika, na haijaona kama shule kukosa vyoo ni tatizo unataka Wananchi wafanyeje?

Watanzania tunalipa kodi na ninaamini kama ingetumika vizuri ingetatua matatizo mengi ya aina hii!
 
Mkuu hiyo sheria sijaisoma; lakini kama habari ni ya kweli si ya kuzusha, na mtoa habari anaweza kuthibitsha kama akitakiwa, ni kipengele gani kwenye hiyo sheria kinaweza kumbana?!
Kuna hiyo video ambayo ndio tangazo lenyewe la Hakielimu iko kwenye post no.17 ya huu uzi.Hiyo video serikali wanaweza kusema ni ya kubuni hivyo hata wewe ulioisambaza unakuwa ni mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria ya cybercrime iliopitishwa na Bunge.
 
Kuna tangazo,binafsi nimeliona leo ITV, linaonyesha tatizo kubwa la vyoo katika shule zetu za msingi.

Tangazo hilo linasikitisha ukiliangalia. Tangazo linaonyesha jengo bovu na chakavu sana la choo huku wanafunzi wakipanga foleni ndefu na hapo hapo wakigombania kuingia chooni na kibaya zaidi mwalimu wa kike anaonekana awali akitoka katika choo hicho kabla ya wanafunzi kuingia kitu kinachomanisha kuwa walimu wanachangia choo hicho na wanafunzi wao.

Kwa waliona tangazo hilo bila shaka watakubaliana na mimi na huenda wakawa na mengi ya kuongeza kuhusu tangazo hilo.Mimi ndio leo nimeliona kwa mara ya kwanza sijui nyinyi wenzangu maana huenda lina muda.

Kwa ujumbe unaobebwa katika tangazo hilo,sidhani kama litavumiliwa.

Tusubiri muda utaongea.

Niliona hilo tangazo na nilisema halitadumu kabisa, halitarushwa tena.
 
Kwa kweli hili tangazo la HAKI ELIMU nimeliona leo kwa mara ya tatu na nafikiri kuwa linaonyesha kuwa kuna uhaba wa vyoo bora mashuleni. Hata hivyo kwa maoni yangu nafikiri chumvi imeongezwa sana na hii itasababisha lisitishwe muda si mrefu, isipokuwa kama serikali ilishirikishwa katika kuliandaa.

Chumvi imeongezwa wapi? Tatizo la vyoo hasa wakati wa break linakuwa kubwa kabisa kwa vile watoto wengi wanakuwa nje na kuongozana kwenda kumalizia haja kabla ya kurudi darasani
 
Kwa kweli hili tangazo la HAKI ELIMU nimeliona leo kwa mara ya tatu na nafikiri kuwa linaonyesha kuwa kuna uhaba wa vyoo bora mashuleni. Hata hivyo kwa maoni yangu nafikiri chumvi imeongezwa sana na hii itasababisha lisitishwe muda si mrefu, isipokuwa kama serikali ilishirikishwa katika kuliandaa.

Ndio matatizo yetu waafroka kwa jumla kitu cha ukweli maisha yote tunasingizia chimvi imeongezwa....halafu hatua itakyochuliwa ni kulifungia tanganzo sio kuboresha mazingira ya vyooo,hapo ndio tunaposhidwa wafrika hatuoni mambo vile yalivyo tunayaona tunavyotaka sisi
 
Shule za msingi Liwiti na Misewe ktk wilaya ya Ilala zimefungwa kutokana na ubovu wa vyoo.
 
Viongozi hawatumii akili kabisa, BRN sijui ni kitu gani hiki, hivi unawezaje kukiri upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati lakini huoni kuwa kuna upungufu wa vyoo pia? Unaongeza madawati, madarasa, ofisi za walimu lakini idadi ya vyoo ni ileile ya miaka ya 70? Halafu kuna wizara inashughulika na elimu, jamani nchi ngumu hii kila siku wakuu wako kwenye ziara za mafunzo nje ya nchi, wanajifunza kw faida ya familia zao mbona hawtoi mfunzo hayo kwa jamii? Hata la vyoo tunasubiri ufadhili wa hisani ya watu wa Marekani?
 
Hilo tangazo safi kabisa kwani litawaamsha wakaguzi wa shule wafanye kazi zao ikiwa ni pamoja na kuwaamsha wananchi waboreshe shule zao. Hivi ile sh 10,000/= inayotolewa kwa kila mwanafunzi inafanya kazi gani? Hata waalimu wenyewe wanatakiwa wajue cha kufanya hali inapofikia hali mbaya namna hii.
 
Back
Top Bottom