Tanganyikanism tukutane hapa

Zanzibar vs Tanzania kwa nini isiwe Zanzibar vs Tanganyika????
View attachment 2702773
Tunazidi kuchanganyana! Mimi nilifikiri Tanzania inapotajwa na Zanzibar inakuwa imejumuishwa. Kumbe kuna nchi ya Tanzania na nchi ya Zanzibar!

Kwa kuwa Tanzania ni nchi na Zanzibar ni nchi, Tanganyika nayo ni nchi.

Kwa hiyo tuna nchi tatu: Tanzania, Tanganyika na Zanzibar.

Kama ndivyo, tujulishwe Tanganyika imepangwa kucheza na nchi ipi kati ya Tanzania na Zanzibar?
 
Maana yake hakuna Tanganyika.
 
Kila binadamu ana wazazi wawili. Kukataa uwepo wa Tanganyika ni sawa na kuikana uwepo wa Tanzania.

Tanzania ni mtoto aloyepatikana kutokana na ndoa ya Tanganyika na Zanzibar.

Tanganyika will never die.
Kama ipo tunadai nini??
 
UBAGUZI na UKABURU
 
Inawezekana Kwa Wakati huo na waliokuwa wanausimamia ulikuwa na umuhimu na ulikuwa hai, lakini waloptoweka Muungano nao ulivunjwa na waliofuata kuongoza nchi. Mfano:
Wakati tukiwa wamoja hatukuwa na Zanzibar kama ambavyo Tanganyika haipo. Tulikuwa na Tanzania bara na Tanzania visiwani. Wahuni wakavunja Muungano Kwa kurudisha Zanzibar. Kwa hilo lazima Tanganyika irudi.
Wazanzbari wanaruhusiwa kumiliki ardhi Tanganyika, kuteuliwa kuwa hadi wakuu wa wilaya,wakurugenzi, mawaziri Kwa yasiyo ya Muungano. Wanamiliki vitambulisho hadi vya Tanzania Wakati mtu kutaka Tanganyika haruhusiwi hata kuwa shea, achilia mbali kugombea uongozi huko Zanzibar.
Huu siyo Muungano unaofaa kuwepo Kwa sasa. Turudi mezani ili kuondoka dhuruma Kwa watanganyika.
 
Kama ipo tunadai nini??
Tunadai haki ya nchi yetu Tanganyika kutambuliwa kama nchi ya Zanzibar inavyotambuliwa.

Tunadai haki ya Watanganyika kufaidi vya Tanganyika kama Wazanzibar wanavyofaidi vya Zanzibar.
 
Naam, umenena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…