Napongeza kwa matumizi ya neno "Tanganyika" badala ya Tanzania

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Napongeza matumizi ya neno "Watanganyika" msamiati unaokua kwa kasi kwa sasa kuliko kutumia neno "Watanzania".

Wenzetu visiwani ni ngumu sana kuacha neno ZANZIBAR au Mzanzibar ni ngumu kwa wao kujiita Mtanzania ila sisi tumeng'ang'ana na huo msamiati wa utanzania usio na faida huku tukisahau kuwa Tanganyika iliuawa mnamo tarehe 26/04/1964

Lazima Tanganyika yetu irudi kwa gharama zozote zile, sisi sio watanzania bara noo sisi ni watanganyika, sisi ni wazanzibar, hivyo ndivyo inavyopaswa kutumika
 
Zanzibar ilipata Uhuru Tarehe 10 December 1963,ikawa mwanachama wa kudumu wa Umoja wa Mataifa namba 112.

Pichani ni Mwakilishi wa Zanzibar Umoja wa Mataifa Balozi Hilal M.Hilal.

Wazanzibari wanajitambua.

IMG-20230530-WA0041.jpg
 
Hakuna cha kujivunia Utanganyika jitu likipata nafasi anatumia mamlaka kudhulumu, kufanya ufisadi, rushwa,kupachika vyeo ndugu zake au kabila lake nk.

Jina halitobadilisha chochote ikiwa sisi bado hatujitambui na ufisadi ukiwa unaendelea.
 
Si mlikuwa mnasema Zanzibar ni koloni lenu, kiko wapi sasa mnatia huruma?

Acheni kulialia sindano iingie vizuri.
 
Kwani ulikua hujui kuwa Tanganyika ni danga bora sana la Zanzibar? Kwa kinachoendelea sasa ina onyesha ni danga nono sana acha li chunwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom