Tanganyika Law Society Wamenaswa?

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Ili kuhakikisha katiba mpya haipatikani,AG werema na Kombani wamechomeka kipengele ndaoi ya sheria ya mchakato wa kupata katiba mpya ambacho kitapingwa na hivyo kuchelewesha zoezi zima la mchakato wa kuandika katiba mpya. TLS wameonesha nia hiyo. Wanataka kwenda kupinga sheria hiyo mahakamani.
Mchakato wa katiba mpya ulipingwa na unaendelea kupingwa na AG Werema na waziri wa katiba Kombaoi.
Wamemshauri vibaya JK. Wamempotosha,amebaki kuumbuka mbele ya umma na nje ya nchi.
JK wasaidizi wako hawa wanakuandaa kuingia kwenye historia ya marais watakaotukanwa oa historia ya nchi yetu milele. E. Lowassa ameishaanza kutukanwa na historia. Elewa "Si kila asemaye bwana bwana yu upande wako"
 
Bora ujue huna mke kuliko kuwa na mke Malaya! Katiba mpya kupitia hii tume ni sawa kuoa Malaya anaye endeleza umalaya!
 
kirema na huyo mwenzake kombaini walishasema hawaoni haja ya kuwa na katiba mpya kwa sasa
 
Hivi kifungu hicho kilichowekwa wabunge hawakukiona? Vinginevyo kama TLS wakishindwa katika kesi hii wanayotaka kuifungua viongozi wengi wa kisiasa na hasa kutoka vyama vya upinzani watafungwa na uchangiaji wa wananchi utakuwa finyu sana kwa kuogopa sheria hii!
 
Mkuu, hivi unajua kuwa wabunge wanapochangia muswada wengine wanakuwa hawajausoma wote kwa makini? Wengine husama utangulizi tu na qwengine husikiliza hotuba ya waziri tu... na ndio maana wabunge wengi hutumia muda mwingi wa kuchangia kutoa shukrani au kurusha vijembe
 
Wangepata wapi muda wa kukisoma wakati si wasomaji wazuri wa miswaada, wachache wanaojitahidi huishia kusoma utangulizi tu.

Sasa ukizingatia kwamba wabunge makini wa chadema walisusia mjadala, basi waliobaki wakapoteza network ya muswada na kunasa kwenye network ya mipasho na matusi kwa Tundu Lisu na Chadema!!

Sasa matokeo yake ndio hayo Werema akachomekea "further schedule of ammendment" na wabunge wengi hawakuliona hilo, kuna wachache sana waliliona lakini walipohoji, werema akajibu kwa ufedhuli tu na muswada ukapita.
 
Mkuu, hivi unajua kuwa wabunge wanapochangia muswada wengine wanakuwa hawajausoma wote kwa makini? Wengine husama utangulizi tu na qwengine husikiliza hotuba ya waziri tu... na ndio maana wabunge wengi hutumia muda mwingi wa kuchangia kutoa shukrani au kurusha vijembe
Ni kweli Mkuu. Wengi kipindi hicho walikuwa wanafikiria nyongeza ya posho yao ya laki mbili!
 
Bora mchakato uchelewe lakini ipatikane itakayokidhi mahitaji ya watanzania, tena namkumbusha Jk katiba watanzania wanayoitaka itapatikana tu hata kama wengi watafungwa na muda mrefu kupita lakini mwisho wa yote ni katiba tunayoitaka na wakati itakapopatikana wale waliochangia kuichelewesha kwa makusudi watahukumiwa kwa hiyo katiba
 
Hivi kifungu hicho kilichowekwa wabunge hawakukiona? Vinginevyo kama TLS wakishindwa katika kesi hii wanayotaka kuifungua viongozi wengi wa kisiasa na hasa kutoka vyama vya upinzani watafungwa na uchangiaji wa wananchi utakuwa finyu sana kwa kuogopa sheria hii!

kwani wabunge siku ile walikuwa wanasoma mswada husika,wao kazi yao ilikuwa ni kutafuta mchawi na kukemea na kutukana kwa wale waliotoka nje,sasa hilo ni tatizo la kutokuusoma vyema mswada na kuupitisha kwa sauti ya wengi wape,

nachokiombea tu mauaji yasitokee
 
Thread haina kichwa wala miguu. Kipengele chenyewe hatuambiwi, watu wanalalama tu. This is highly dishonesty!
 
Ili kuhakikisha katiba mpya haipatikani,AG werema na Kombani wamechomeka kipengele ndaoi ya sheria ya mchakato wa kupata katiba mpya ambacho kitapingwa na hivyo kuchelewesha zoezi zima la mchakato wa kuandika katiba mpya. TLS wameonesha nia hiyo. Wanataka kwenda kupinga sheria hiyo mahakamani.
Mchakato wa katiba mpya ulipingwa na unaendelea kupingwa na AG Werema na waziri wa katiba Kombaoi.
Wamemshauri vibaya JK. Wamempotosha,amebaki kuumbuka mbele ya umma na nje ya nchi.
JK wasaidizi wako hawa wanakuandaa kuingia kwenye historia ya marais watakaotukanwa oa historia ya nchi yetu milele. E. Lowassa ameishaanza kutukanwa na historia. Elewa "Si kila asemaye bwana bwana yu upande wako"

Ni kifungu kipi hicho kilichochomekwa na Werema?
 
Back
Top Bottom