mwehu ndama
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 2,461
- 9,500
Kwa miaka mingi Mungu amekua akiitumia Taifa langu Tanganyika kama mapumziko na tumaini la wanadamu kutoka mataifa kadha wa kadha mbao tamaa na ukatili wa binadamu wenzao ziliwafanya wakakimbia nchi zao.
Tanganyika ndio nyumba ya shuhuda za mamilioni ya wakimbizi wa kiafrika ambao sasa wanaishi katika mataifa mengine baada ya kupata hifadhi na mapokeo ya kindugu katika ardhi yetu..Ni nchi yenye watu wakarimu kama ilivyo ardhi yake yenye rutuba!!
Tanganyika haijawa kimbilio la wenye uhitaji kwa bahati mbaya , la hasha isipokuwa ni mpango wa Mungu juu ya Taifa hili .Na kama Mungu / Allah aishivyo na ndivyo neno na mpango wake hutimilizwa.
Leo ni Siku ya 4 Tanganyika inalia machozi ya damu , Ardhi ya Tanganyika hivi sasa inapokea damu ya waTanganyika wasio na hatia . Tanganyika Iko mikononi mwa wenye nia ovu na kusudio la kuharibu mpango wa Mungu juu ya Taifa la kipekee.
Lakini kwa kua Mungu yu hai , nae amekisikia kilio cha waTanganyika. Damu ya waTanganyika inayomwagika imetiririka malangoni pa bwana wa majeshi , nae katika Siku isiyo tarajiwa ,atawafutilia mbali watesi wa Tanganyika na kuifanya kurudi kua tumaini la walio elemewa kama awali.
Mungu simama na Tanganyika na vijana wake shupavu.
Amen!!