Tanga,where,when and what time did you go wrong? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanga,where,when and what time did you go wrong?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KUNANI PALE TGA, Jul 26, 2010.

 1. KUNANI PALE TGA

  KUNANI PALE TGA Senior Member

  #1
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  habari za kutwa,
  Jamani,nalilia mji wangu,mji ambao upo kando kando ya bahari ya hindi,mji ambao ulikuwa mjii mkuu wakati wa ukoloni wa ujerumani,mji ambao una kila neema.lakini najiuliza wapi tulipokosea na kuufanya mji huo ambao miaka ya nyuma ulikuwa mji ambao umechangamka.sasa hivi ukitembea mjini tanga unaweza kuogopa kuona majumba ya zamani ambazo zimebomoka,kati kati ya mji,esp kwenye mitaa ya benki,yaani inatia huruma kama mji ulikuwa kwenye vita vile.najiuliza kama hayo majumba hayana mwenyeji,mbona NHC zisichukue na kushusha magorofa kwa ajili ya wananchi kukaa?majumba yote ya tanga yamechoka,imagine mgeni anapotembelea barabara hiyo ya benki na kukuta majumba yaliyoanguka bila kitu chchote kuendelea hapo?mbona mji mzuri kama wa tanga umelemaa?mbona serikali isiseme,investment dar es salaam basi,watu wa invest mkoani.na esp tanga ambapo kuna bandari?barabara hapo hapo mtaa wa benki ambapo ni katikati ya jiji,imechoka ile mbaya,yaani barabara ya kilometa kama mbili inashindwa kutengenzwa?jamani,nalilia mji wangu,mji ambao ungechangamka,ingekuwa sehemu moja safi kuishi hapa tanzania.jamani,naomba watu wa tga mliopo hapa,tuungane tubadilishe jiji letu liwe kwenye hadhi ya jiji haswa,na siyo jiji kwa maneno tu.angalau barabara za katikati ya mji zitengenzwe.barabara kutoka ghorofa la tanesco mpaka chumbageni ni hovyo sana.hapo ni centre of the town.mbona uchumi umekufa?what is the reason behind?taa za barabarani pia ni za kuhesabu.kuna tourist attraction nyingi tu,lakini hukuti watalii?why?pls god bless our beautiful town and make it once a heaven,god we pray tht the economy of the town revive again,our roads be repaired,old houses be refurbished,and those collapsed one have the final solution.god bless tanga,god bless tanzania.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Tatizo kila mtu na kila kitu kinataka kulundikana Dar. Na hii inasababisha the so called domino effect, wanaokuja nao wanataka kujenga na kulundikana Dar. Watanzania tuna nchi kubwa lakini watu wanajenga Dar na labda nyumbani kwao kijijini, ni vigumu kukuta mtu anaamua kwenda kukaa mji mwingine kwa sababu ya kazi na kujenga/ ku settle huko.

  Lakini wananchi wa Tanga wenyewe wamefanya nini kuhakikisha wanavutia maendeleo mkoani/ mjini kwao ? Maana kila mtu akitegemea mwenzake afanye kitu hamna kitakachofanyika.
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 3,997
  Trophy Points: 280
  Watu wa Tanga jaribuni upinzani, angalia Kigoma sasa hivi Kigoma itakuwa kama Mwanza na sababu nathani wote tunaijua! CCM wamepania kulinda majimbo maana wanajua watu wa huko hawajabweteka vile vile angalia Kilimanjaro pia CCM imelazimika kupeleka barabara ili kulinda majimbo pia Pemba huko naskia lami zinajengwa ili mradi tu kuwalainisha wana CUF huko! Maendeleo huletwa na kujititimua pia na si kuendelea kuwa watu wa NDIO! Mkwere ana mpango wa kuhamisha mradi wa Mwambani tanga kwenda Mbegani sasa jiulize unapigia CCM kura kwa manufaa ya nani? si ili kumwezesha kuhamisha miradi ambayo ingesaidia the whole of Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mara mpk Mwanza?
   
 4. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  ni kweli tanga nilizaliwa na kukaa pale majani-mapana,chumbageni,kisosola,raskazoni ulikua mji mwanana sana,mji ulikua na maendeleo viwanda lami amboni caves...serikali haiwezi fanya kitu adi sisi tusimame kama wanainchi wa (kunduchi) labda ndo itawezekana
  turudi tukajenge mji
   
 5. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Niweke uchokozi kidogo. Huko miaka kadhaa ya nyuma Tanga ilianza kuvuma zaidi kwa dunga (stori za warembo wenye kwato na wenye kuzima taa kwa mkono mita 10 bila kuinuka toka kitandani). Yumkini kwa mwelekeo huo ilibidi maendeleo yatoweke kupitia dirishani. Sehemu yoyote inayovuma kwa zaidi kwa sayansi mbadala daima haiendani na maendeleo ya usasa.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Once Nilienda tanga nilifurahi kuina kuna kuna baadhi ya majengo kuna parking special ya baiskeli. Kama meya na wadiwani wana kuwa creative wanaweza kuutangaza kama Green city na kuanzisha vitu tofauti na miji mingine. may be kusema mwenye baiskkeli/pikipiki ana haki kuliko mwenye gari kati katika barabara za jiji.

  Tanga haiwezi kusindana na Dar kwa majengo, Haiwezi kushdina na dar kwa bara bara za njia mbili mbili, etc

  There are some few "crazy things" that can be done but makes the town to stand out uniquely from other town/city.
   
 7. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inabidi wananchi wa mkoa wa Tanga wakake chini na kufikiara kwa kina jinsi gani wanaweza kubadilisha hali ya mkoa wao. Kwa kweli hali ya mkoa huu inasikitisha sana. Miaka ya late 80's na early 90's Tanga ilikuwa inatisha kama njaa. Kulikuwa na viwanda kama kumi, mfano viwanda vya maziwa, foma, chuma, sabuni za minara, mafuta ya kula, Cementi, Katani, alizeti n.k Ilikuwa ukikosa tiketi ya kwenda Moshi na Arusha, station Master anakwambia panda mabehewa yanayokwenda Tanga, na ukifika Mombo au Korogwe utapata nafasi. Hii ni kwa sababu kwenye reli ya kati, Mkoa wa Tanga walikuwa wanapewa zaidi ya Mabehewa 12. Lakini leo Tanga inapigwa darizi hata na mikoa ya South.

  Kwa mtazamao wangu, hili tatizo linasababishwa na wananchi wenyewe wa mkoa wa Tanga. Igeni mikoa mingine jamani!!! Wawajibisheni viongozi wenu. Mkoa unawasomi kibao, lakini hakuna anayejali hali ya wananchi wa maendeleo ya mkoa. Nakisia muheshimiwa Mwapachu ANAGOMBEA TENA, baada ya kuwa mbunge wa Tanga kwa miaka 15. Binafsi sielewi huwa anasema nini kwenye kampeni? au wazawa wa mkoa huo huwa wanauliza maswali gani kwenye hiyo mikutano ya KAMPENI za uchaguzi?

  Seriously, baada ya miaka 15 ya kuwa mwakilishi wa jimbo bila mafanyikio yoyote nadhani inabidi wapiga kura wafikirie mara mbili ni nani anastahili kura yao.:nono:
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Naona watu wanaongea meeengi, lakini sidhani kama tatizo ni la Tanga peke yake au tatizo ni wawakilishi, sidhani! Tatizo lipo kwene mambo ya upangaji wa mbovu wa mipango ya kimaendeleo ya serikali yenyewe. Kwanza serikali inasema wazi ilishaacha mambo ya kuwekeza kwenye uzalishaji na utoaji huduma, eti inadai shughuli hizo zifanywe na sekta binafsi. Hapo ndio tatizo linapoanzia. Yaani unakuwa na serikali ambayo unailipa kodi lakini inazidi kujivua wajibu siku hadi siku! Nimeshauliza mara kadhaa kwamba kwanini tui-maintain na kuilea hii serikali while it gives back SO LITTLE. Imekuwa kama ni mashine ya miujiza inaingiza sh mia na kutoa thumni!

  It is time we start question how this government operates, tuanze kuhoji maswali ya msingi why we should maintain them..itueleze kinagaubaga uhalali wa uwepo wake.
   
 9. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wananchi wanawakilishwa na WABUNGE huko serikalini. Hivyo basi, tuanze na hao wawakilishi, halafu serikali kuu itapata habari yake.
   
 10. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,990
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa Tanga Technical Secondary School (maarufu kama, Tanga School) kati ya 1984 - 1987 pale Makorora Tanga, kwahakika Tanga ya wakati ule ni tofauti kabisa na sasa. Kipindi kile barabara, huduma za afya, usafi wa mji, uzuri na ubora wa majengo, na hata ustaarabu ulikuwa ni mkubwa sana kwani ilikuwa waweza toka Makorola hadi Majani mapana bila hata ya kukutana na askari polisi yeyote yule na siyo leo hii.

  Tuangalie je, tulikosea wapi? Kwani binafsi Tanga ni Kwetu japokuwa sisi familia yote tumeifanya Dodoma kuwa ndo kwetu!
  Je, wale wa TA tunafanyaje sasa kurudisha hadhi ya Tanga? kwani hata soka sasa Tanga lipo chini. Enzi ile Tanga ilikuwa maarufu kwa soka na kulikuwa na timu zinatisha kama; African Sports, Coast Union n.k. Leo timu hizo ziko wapi wana-Tanga wenzangu?
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Nyerere aliona Tanga imeendelea sana akaamua kutopeleka ruzuku ili mikoa mingine ikechapu na Tanga....akaiuwa
   
 12. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nyerere hayupo madarakani tangu 1985. Wanatanga wakielekeza lawama huko (kwa Mwalimu) itakuwa sio sahihi. Tatizo ni la watu wa TA wenyewe. Amkeni!!!!!!:doh:
   
 13. bona

  bona JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  watu wa tanga uvivu wao ndio unauzorotesha mji, wamerithi tamaduni za kiarabu za kua ma mwinyi, kukaa tu barazani na kucheza bao huku wakifanyiwa kazi na wengine wao wale tu, wanawake wanajali kujiboresha miili tu ili wapendwe zaidi na wanaume!
   
 14. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  ni hao hao watakaoicxhagua CCM kwa kura nyingi
   
 15. K

  KISUKALI Member

  #15
  Aug 1, 2010
  Joined: Feb 28, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu,
  Je kuna ukweli wowote kwenye madai ya Safari?
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tanga pamoja na kila kitu bado ni pouwa sana!
  Hivi bado ni City au ilikuwa downgraded?
  Kila nikienda Tanga natamani kurudi tena na tena....

  Kinachotakiwa ni wenyeji kujizatiti kuboresha tu. Watu wa kuja siyo wa kutegemewa sana hasa ukizingatia shughuli za kiuchumi zimezorota sana.
   
 17. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Safari za kanda ya kaskazini? 100% ndugu yangu. Tanga ilikuwa balaa!! Yaani reli ya kati ni kama ilikuwa kwa ajili ya mkoa wa Tanga peke yake.
  Mambo leo hii ni :A S 112:. Unemployment nasikia imefikia 35%, just imagine!
   
 18. a

  alibaba Senior Member

  #18
  Aug 1, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  "Nyerere aliona Tanga imeendelea sana akaamua kutopeleka ruzuku ili mikoa mingine ikechapu na Tanga....akaiuwa"
  M kishori, hayo hapo juu ni madai ya safari ni safari, nawe kkachangia kuwa Nyerere hayupo toka 1995.
  Ni kweli, Kisukali akauliza je kuna ukweli kwenye madai hayo ya Safari?
   
Loading...